Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Uko wrong vibaya mnooo, kuna watu wana vibiashara mpaka vya laki laki na wanapata faida.. ishu ni kulenga tu.. unadhani wale wauza vijipweza kando ya barabara, wauza ice cream za bakhresa, vijana wanaouza matunda,wale wanaopoint nguo, wale wa viatu? Mzee kuna wauza kahawa mjini hapa n.k n.k, unadhani mitaji yao imezidi hiyo laki 2? Kuna wamama wanauza supu za mapupu na chapati na wanagonga hela mbaya. Kuwekeza hela nyingii,sio kigezo cha kupata faida kubwa saana.

Muhimu tu ajue si rahisi kuanza biashara leo leo kisha upige hiyo faida japo inawezekana. Muhimu awe na subira.
 

Watu kama nyie mnaoandika ujinga Sina muda wa kuwajibu ....wauza pweza ,wauza upupu na chapati ,karanga njiani ....ndio wanatengeneza faida ya 20k Kwa siku ? Yaani kwa mwezi wanapata laki 6 mshahara ambao hata mwalimu Hana ??? Harafu Bado wanaishi mazingira Yale ,? Mtanzania anayepata laki 6 kwa mwezi ni WA kukaa Yale mazingira Unaakili sawa wewe ....


Endelea kudanganya wajinga na wapumbavu humu humu jf ....
 
Sijasema wanatengeneza faida ya 20k kila siku(costant), lakini nina uhakika wanapiga faida ya 10k,15, mpaka 20k bila tabu,

Unaishi wapi mkuu, isije kuwa naongea na mtoto wa masaki, kwako utaona ni maajabu ila wa mbagala mbagala,temeke huko,tandale,mwananyamala yake huko.. uswazi hivi vitu ni kawaida.
Mtu ana mke watoto wa3 wanasoma, alipe kodi nakadhalika unategemea aishi vipi.. hizo hizo biashara siku zinasogea.
 
Sikiliza bro, usijifanye mjuaji. Mtafute muuza pweza mmoja kaa naye muombe kistaarabu akupe PROFIT STORY ya pweza wake kila siku.
Mimi nina uhakika kabisa muuza pweza anapata faida ya 20,000 mpaka 30,000 kila siku atakayokwenda mzigoni.

Wewe una tatizo moja. Unapiga kwamba anapata laki 6 kwa mwezi. Ukumbuke kwamba anapata hiyo laki 6 lakini anaitumia kila siku pia. Ana familia kijinini anaitumia pesa (wazazi) anasomesha, ana familia yake mwenyewe, ana demu n.k

Wewe ulitaka waishi maisha gani? Laki 6 ni ya kuishi vizuri? Au kwa sababu waalimu wanavaa vizuri? Wanavaa vile kwa sababu ya mazingira yao ya kazi. Mimi personally nina mshahara mzuri tu lakini hutawahi nikuta nimevaa vizuri (hasa nikiwa kazini) sababu kazi yangu haifai kabisa kuvaa nikapendeza. Nikipendeza saa 2 asubuhi, kufikia saa 6 tu nishachafuka jasho, vumbi.

Laki 6 sio kupanga nyumba ya laki 1 na nusu ila wengi mmepanga hivyo sababu ya show offs tu. Hamna hata kiwanja Bagamoyo wakati wao wanavyo.
 
Laki 2, amka alfajiri sana nenda Ilala pale kapoint viatu vya mtumba vikali. Visafishe vizuri, tafuta eneo zuri lenye vijana wengi kama Makumbusho, Mwenge, karibu na vyuo. Ukiuza pair 3 tu ushapata hiyo elfu 20.

Ntakuja kukupa ufafanuzi zaidi.
 
Laki 2, amka alfajiri sana nenda Ilala pale kapoint viatu vya mtumba vikali. Visafishe vizuri, tafuta eneo zuri lenye vijana wengi kama Makumbusho, Mwenge, karibu na vyuo. Ukiuza pair 3 tu ushapata hiyo elfu 20.

Ntakuja kukupa ufafanuzi zaidi.
Tena hiyo 20k ni faida tu bado mtaji upo palepale

Hawa madogo wanaokaa kwa shemeji hawawezi jua hili
 

Acha kudanganya umma wewe etuuza pweza anapata faida ya 20 k kila siku 🀣🀣🀣...unaijua faida wewe au hujui hata maana ya faida ,unavosema hio faida inatumika kila siku maisha ya wale watu ni ya kimasikini hali ya chini kabisa Kwa siku hawatumii zaidi ya 8000 na ile meza yao ukikusanya mazaga yote mezani ambayo abakusanya watu na kuwauzia haizidi 18k na huwa biashara zao ni za barabarani kuanzia jion ........

Faida ni mauzo yote utoe gharama ya uendeshaji unayopata ndio faida ...Sasa hao wauza pweza mzee ndio wa kupata faida 20k Kwa siku au mnafikili sisi hatupo barabarani tunateseka huku field sio mchezo ...

Narudia Tena nitajie biashara ya mtaji wa 200k harafu unipe mchanganuo wa faida ya 20000 Kwa siku .....labda hujui maana ya faida .....
 
Mkuu wewe endelea kubet tu
 
Si kwamba haiwezekani Mkuu...ila kitakachotokea ni aina ya dili na namna ya kuisotea kuitimiza.

Vipi kama akapata zali akakutana na Mtu akampa dili ya kumtafutia Jongoo bahari kilo mia kila siku naye akaweza kuzipata kwa gharama ya shilingi laki moja na akasafirisha kwa sh elfu 50 na Tajiri akawa ananunua hizo kilo mia kwa sh laki na hamsini?.

Nasisitiza nimetoa tu mfano kupingana na hoja ya kwamba haiwezekani, ila ni kubahatisha 1 kwenye 100.
 
Mimi nasema hivi jf wanajua kuandika matumaini hewa .....ni hivo tu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Laki mbili hata genge hutengenezi Sasa sijui hio faida ya 20k kwa siku utaipata wapi .....

Labda mauzo yote yawe 20000 harafu kesho anaenda kununua vitu na matumizi mengine anajikuta kabaki na elfu mbili kama faidaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 

Kumbe unasema kubahatisha ohoooooπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…


Kama ni hivo amupe Leo arsenal ,Chelsea ,psg ,Madrid aweke hio laki mbili ....si mnataka kubahatisha πŸ˜…
 
Laki 2, amka alfajiri sana nenda Ilala pale kapoint viatu vya mtumba vikali. Visafishe vizuri, tafuta eneo zuri lenye vijana wengi kama Makumbusho, Mwenge, karibu na vyuo. Ukiuza pair 3 tu ushapata hiyo elfu 20.

Ntakuja kukupa ufafanuzi zaidi.
Viatu ni kweli kuna ndugu yangu alikuwa anachukua mzigo hapo karume anaenda kuuza Simu 2000,kiatu ananunua elf 3-4 anakiuza elf 35,30,mpaka 25...faida ni kubwa sana kama una wateja ila kwa sasa aliacha mambo ya yaliyumba wateja hamna...miaka kabla ya anko MAGu alikuwa analala na faida hadi ya laki na nusu mpaka laki 2.
 
Nimekwambia mtafute muuza pweza.
 
CONTROLA kummentor mtu ada yako ikoje mkuu
 
CONTROLA kummentor mtu ada yako ikoje mkuu
It depends Boss, mtu awe willing tu (mambo mengine yanakuja)

nafanyaga vitu ili wengine wainuke,sijawahi waza kupata pesa toka

kwa mtu asie na kitu,kama ni mganga mimi ni yule mganga anaekwambia

Nakutatulia tatizo lako, Nenda nyumbani baada ya wiki tatizo lako litakua limeisha

ukiona kweli limeisha Basi urudi kutoa shukurani, Mimi ni aina hiyo wa waganga Mkuu (sijui kama umenielewa)
 
nmekupata πŸ’―
 
Kweli Huyo Jamaa Pain killer Ni Mtu wa Kupuuza La Sivyo Aliyetoa Uzi Atapotea Akimfata.Wanaishi Maisha Yale Kwa Sababu Wanahudumia Familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…