Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Nianzishe Biashara gani ambayo inaweza kunisogeza mbele Kwa mtaji wa laki 2 ?
Pitia nyuzi hzo hakika utapata chochote kitu


 
Naomba tuwasiliane boss unipe muongozo vizuri
 
Mimi machinga wa kutengeneza wadada kucha na rangi,mtaji wangu ni elfu20,siku mbaya napata15 ikiwa nzuri 20 au 25.
Naunga hoja![emoji106][emoji106]Kupaka rangi na kutengeneza kucha hadi elfu 40 kwa siku unalaza!
 
Usitumie nguvu nyingi kumwelewesha mtu kama huyu, watu kama hawa always huwa wapo kupinga mawazo ya watu wengine! Hawataki watu waujue ukweli ili wajikwamue kiuchumi kiufupi ni wabinafsi! Yaan mtu atumie laki 2 ashindwe kuingiza elfu 20 kwa siku??? Wakat kuna watu ninawajua kwa mtaji wa laki 3 wanatengeneza laki 1+!!
 
Natamani kuijua hii biashara!

Japo kiuhalisia haiwezi kuwa biashara halali
 
Sawa
 
NAOMBA KUULIZA NI BIASHARA GANI INAYOWEZA KUKUA KWA HARAKA KWA MTAJI SH.10000?
Uza mayai ya kuchemsha.
Mtaji tray 8500/=
Mkaa 500.
Chumvi chukua nyumbani.
Jumla 9000/=
Unauza 500*30pcs jumla 15,000/= faida 6000 per tray.

Mchana nenda kwa bakresa ongea nao chukua ice cream pita juan haukosi 25k hadi 30k n ujanja wako wa kujua location za madada au wahitaji.

Ni rahisi ukijikana uwezo wa kutengeneza 30k per day n mkubwa baada ya muda fulan unaachana na utumwa unahamia kivulini.
 
Sijui akauzie wapi, nipo kkoo, nawaoneaga huruma wauza mayai. Kiasi kwamba huwa nanunua mengi nikiwakuta wanapita, ila bado, kazi ngumu sana hiyo kumaliza trey.
Vijana wapambane tu.
 
Sijui akauzie wapi, nipo kkoo, nawaoneaga huruma wauza mayai. Kiasi kwamba huwa nanunua mengi nikiwakuta wanapita, ila bado, kazi ngumu sana hiyo kumaliza trey.
Vijana wapambane tu.
Hakuna kazi rahisi ndg yangu,mambo yangekua mepesi kila mtu angekua bilionea akiwa mjanja tena tray mbili siku ya kwanza yanaisha.

Nakufungua macho ukishaona vijana wengi wanazungusha jua kuna soko kubwa na lililotayari,kikubwa usafi,uchangamfu na kuvua aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…