Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Watu kama nyie mnaoandika ujinga Sina muda wa kuwajibu ....wauza pweza ,wauza upupu na chapati ,karanga njiani ....ndio wanatengeneza faida ya 20k Kwa siku ? Yaani kwa mwezi wanapata laki 6 mshahara ambao hata mwalimu Hana ??? Harafu Bado wanaishi mazingira Yale ,? Mtanzania anayepata laki 6 kwa mwezi ni WA kukaa Yale mazingira Unaakili sawa wewe ....


Endelea kudanganya wajinga na wapumbavu humu humu jf ....
Shida ni matumizi , ila uwezekano wa kuingiza hio hela upo.
Ushakutana na wabeba zege? kwa siku anaingiza 20 - 30k mambo yakimnyookea shida matumizi.
Wakitoka hapo anaenda kulewa na kuhonga bar
 
Mpaka Kuanza Kupata Faida Forex Si Mchezo Maybe Uisome Uielewe Sana,Napo Utatakiwa Kutumia muda Wako Mwingi Ili Uunde pesa La sivyo Utaishia Kuburn account Na Kusema Forex Ni Uhuni
hata ukiisoma haisaidii, maana ime base on predictions.. which makes it diffucult to win, yani uwe na unachezea pesa ambazo zipo tu ndio utaona faida coz huna mawazo na upo teari kuwa patient wating for profit.
Most important thing uwe na kismati ndio maana forex ipo kundi la kamali
 
Skin Jeans za kike tunaenda Tandika na Kariakoo tunanunua kwa Tsh. 3000/= kwa kila PC 1.

Hiyo laki mbili yako unapata hizo skin jeans 50,baada ya hapo unazifanyia modification kwa Tsh1000/= kwa kila skin jeans na laki mbili yako inakuwa imeisha na unakuwa umetumia 4000/= kwa kila jeans

Huku kwetu Mbagala kila jeans unauza Tsh 10000/=,hii ina maana umepata faida ya Tsh 6000/= kwa kila jeans na ili upate faida ya Tsh 20,000/= inabidi uuze PC 4 za skin jeans na lengo lako linakuwa limetimia ila huwa tunauza hadi PC 5-8 kwa siku.

Wengi watadharau ila wengine ndio tuanishi mjini kwa style hizo

Wanangu wa Tudo watakuwa wanaelewa nilichokiandika hapa
za mtumba hizo au dukani?
 
Najua watanibeza sanaa ....lakini hio pesa yako haiwezi kukupa faida ya 20,000 kwa siku......

Yaani mtaji wa 200,000. Upate faida ya 20,000 Kwa siku unaota wewe sio bure kama hivyo watu wasingekuwa masikini ...

Mtu wa boda boda karisk 2,500,000 na anapata faida 10k Kwa siku ...

Mtu wa bajaji kanunua 7million Ndio anapata faida ya 20k kwa siku....


Harafu unakuja na mtaji wako wa 200k et upate faida ya 20k kwa siku[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Maisha sio rahisi kiasi hicho ....
Mkuu mtu wa boda anapata faida ya 10k tu! kwa siku??? Wapi huko?

Aise mwambie huyo boda aache matumizi mabaya ya fedha zake
 
Habari za mida hii wana JF,
Naomba kuuliza, kwa mtaji wa Tsh 200, 000 naweza kuanzisha biashara gani hapa Dar itakayoniwezesha kutengeneza faida ya Tsh 20, 000 kwa siku!!
Msaada wenu tafadhari!!
Tafuta kwenye Bar au eneo lililo changamka uza supu ya utumbo wa ng'ombe, supu ya mbuzi au kongoro kwa asubuhi/jioni.
 
Uza mitumba, utatoboa, anza na mtaji wa 150k ili hiyo 50k ikulinde kwa msosi wa wiki ya kwanza ya msoto.
 
Kwa 200'000 ushauri labda ufanye vitu kwa order lakini inafaa ujue unaweza kufanya nini kwa ufanisi mfano vitafunwa, lunch, bites au utafute nafasi ya kua shopper kwa baadhi ya watu.
Kingine muhimu ni forex lakini iyo 200K inaweza ishia katika mafunzo.
Au endelea kufanya kazi ukiendelea kuwekeza pesa zako either utt au fixed bank.
Habari za mida hii wana JF,
Naomba kuuliza, kwa mtaji wa Tsh 200, 000 naweza kuanzisha biashara gani hapa Dar itakayoniwezesha kutengeneza faida ya Tsh 20, 000 kwa siku!!
Msaada wenu tafadhari!
 
Nina mtaji wa laki mbili na nusu, niko Dar, 20 to 24 yrs, Naombeni ushauri kuhusu biashara ya kufanya, hasa hasa iwe ya chakula, mboga na vitoweo ambayo baada ya wiki mbili nitaanza kushuhudia mafao ya kumwaga! Nawaombeni wakuu, nisije jikuta naipeleka bar au nampa sister X, Ushauri tafadhari!
 
Nina mtaji wa laki mbili na nusu, niko Dar, 20 to 24 yrs, Naombeni ushauri kuhusu biashara ya kufanya, hasa hasa iwe ya chakula, mboga na vitoweo ambayo baada ya wiki mbili nitaanza kushuhudia mafao ya kumwaga! Nawaombeni wakuu, nisije jikuta naipeleka bar au nampa sister X, Ushauri tafadhari!
Uza mboga za majan
Nenda bunju huko jumua peleka city center sehem yyt utauza tu
 
Back
Top Bottom