Wadau,
Nipo katika mchakato wa kutengeneza orodha ya biashara ndogo ndogo zenye kuhitaji mitaji midogo isiyozidi 2,000,000/=, ambazo unaweza zungusha mtaji wako na kupata faida kati ya 20% na kuendelea ya mtaji wako ndani ya mwezi mmoja.
Kwa mfano, biashara ambayo mjasiriamali anaweza zungusha 1,000,000/= na kuwa na uwezekano wa kujipatia kipato cha 200,000/= kwa mwezi, baada ya kutoa ngarama zote za kufanya biashara.
Hapa sizungumzii biashara ambazo unahitaji uwekezaji mkubwa mwanzoni (mfano kama kujenga banda, au kulipia kodi ya mwaka mzima).
Hapa nazungumzia biashara kwa mfano uchuuzi, mtu anaweza kununua bidhaa sehemu moja na kwenda kuuza sehemu nyingine. Mfano mzuri ni kama mtu anaenunua samaki, kisha kwenda kuuza kwa reja reja. Au biashara kama ya mitumba, ambayo unaweza kununua "bale" na kuliuza ndani ya mwezi mmoja.
Orodha hii nitaichapisha rasmi kwenye PDF ambayo itawekwa hapa JF.
Pia, nitakua na kipindi cha ujasiriamali ambacho kitakua kinafanyika kwenye radio mara moja kwa wiki. Nina nia ya kutumia orodha hiyo hiyo kwa ajili ya kutoa mawazo ya ujasiria mali na kupata mikopo kwa wasikilizaji.
Nitawafahamisha pale vipindi vitakapoanza kwenye redio.
Natumaini kupata mawazo toka kwenu.
Ram
UPDATE: 22th Sept, 2014
Hadi sasa, biashara ambazo nimeweza kuzifanyia kazi ni biashara ambazo zina return nzuri kwa mwezi, ila capital yake ni kubwa kidogo. Hapa tunazungumzia kuanzia 25Mil - 30Mil kama startup capital.
Ila ni biashara ambazo unaweza pata gross profit ya 35 - 40% ya capital kwa mwezi. Hivyo unaweza pata return ya investment yako ndani ya Miezi 4 - 5 kwa makadirio ya haraka haraka.
Kwa namna nyingine, unaweza ona kuwa wajasiriamali wadogo wanahitaji kuunganisha nguvu pamoja ili kuweza kufanya biashara zinatohitaji mitaji mikubwa.
Tutaendelea kujuzana hapo majaliwa.
UPDATE: 24 Oct, 2014
Lengo la kuanzisha uzi huu ni ili watu wenye uzoefu tofauti tofauti kwenye mambo ya biashara tuweze kuchangia mawazo na kuweza kuangalia kama kuna namna ambayo tunaweza kuwasaidia wale ambao wangependa kuanza biashara, ila hawana uzoefu, taarifa, au mitaji.
Tofauti na wengi wanavyofikiri, lengo hapa haikuwa kwa mimi kutafanya tafiti, na kukusanya taarifa huku na huko, kisha kumpa yule ambae hayuko tayari kutoa mchango wowote.
Hili ni jukwaa la wote, na kila mtu ana uwezo wa kuchangia wazo lolote lile alilo nalo - liwe zuri ama liwe baya.
Asante kwa wale wanaochukua muda wao kuchangia.
Kwa wale wanaopenda kulishwa (spoon feeding) kwenye kila kitu, kila laheri.