Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kama upo sehemu nzuri kibiashara fanya biashara ya vocha
 
Hapa nilipo mkuu kuna hyo biashara kila konA

Sasa kama kuna biashara kila kona si ucheki kati ya hiz biashara ipi inalipa kulingana na mtaji wako ?

Unajua mara nyingi cha kufanya sio mtaji tu bali ni attitude ya mtu pia, Kuna mambo hayaitaji hata mtaji kama ni muaminifu
  • Mali kauli.., kama ni muanifu unaweza ukaongea na watu wakakupa mali ukauza ukiuza uwape chao
  • Magazeti ukienda kwa wakala anakupa unauza, yakibaki unarudisha ukiuza unakula chako (hence hakuna hasara)
  • Vocha, pipi, viroba na bidhaa zote ndogo ndogo unanunua jumla unauza rejareja
  • Mboga mboga na bidhaa nyingine kama kuku samaki n.k. (uchuuzi) unanunua vijijini au nje ya mji na kuleta mjini
  • Kata kata matunda na kuuza., as kamua juice na kuuzia watu
  • Nenda mitumbani wanakufungua marobota chagua zile nguo kali zipige pasi na tembelea maofisini kwa watu wenye pesa.., hapa ukipata wateja kama 20 tu wa kuaminika unaweza ukawa unawapa bidhaa kila siku unaweza kujikuta umejenga nyumba within no time...

Na mengine mengi.., kumbuka hapa issue sio mtaji tu ni wewe kujituma na kutokudharau kazi na kauli nzuri
 
mtaji wa laki 5 ni biashara gani naweza kufanya na ikanilipa?

Kama upo dar , unauwezo wa kuongea na watu vizuri nipm tupige biashara pamoja, ukifanya vizuri huwezi kosa faida laki na nusu kwa wiki . Na kwa yeyote mwenye laptop na mtaji wa laki anaweza ni pm siwezi funguka hadharani watu hawachelewi copy and paste .
 
Soze==umesema vyema sana naam vijana TUPO tunaona lakn wengi wanafharau kazi ila pouwaa kila mtu NA akili zake ...naam namimi nina zangu nakushukuruuu ..
 
Kama upo dar , unauwezo wa kuongea na watu vizuri nipm tupige biashara pamoja, ukifanya vizuri huwezi kosa faida laki na nusu kwa wiki . Na kwa yeyote mwenye laptop na mtaji wa laki anaweza ni pm siwezi funguka hadharani watu hawachelewi copy and paste .

Acha Uchoyo Wewe Kwani Kila Kitu Hadi Tuku PM Sasa Ili Iweje? Funguka Na Jimwage Hapa Hadharani Nasi Tujifunze Na Tufaidike!
 
Ahsnte mkuu hao mbuzi wa elf 30 ninunue wapi mkuu yan wanauzwa wapi...me nipo dar

hiloo wazo la kununua mbuzii kwa 30000 dar liondoe ungekua mikoan labda hapa dar mbuzi wanaoingia si kwa ajili ya kufugwa ni special kwa biashara ya kuchinjwa na mbuz wakawaida ukiendaa kununua utaambiwa laki labda ukute skuio wamechoka ndioo wakuuuzie 80 ila kambuz hKaelewek hapo huna sehem ya kumuhifadhi na chakula cha uyooo mbuzii si umetuambia unaishi manzese hapa fai kwa ufugaji pale labda ungekua tabata,makongo,tegeta,kimara n.k
 
Kama upo sehemu nzuri kibiashara fanya biashara ya vocha

biashara ya vocha unapotezaa mdaaa hakuna faida unasaidia makampuni tu kwa mfano vodacom wanatoa asilimia 6 kwa kila aina ya vocha niambie ili upate faida lazima uhuze sana je kwa siku unauwezo wakuuuza vocha za laki2 ili upate 12000??????? pigia gharama za chakula usafiriii vinginevyooo unakula mtaji unarud pale pale ulipotoka mi nahisii bora ufanye biashara ya matunda karibu na vituo vya basi au mtaaani inaripa ile
 
Kama upo dar , unauwezo wa kuongea na watu vizuri nipm tupige biashara pamoja, ukifanya vizuri huwezi kosa faida laki na nusu kwa wiki . Na kwa yeyote mwenye laptop na mtaji wa laki anaweza ni pm siwezi funguka hadharani watu hawachelewi copy and paste .

mimi hapa
 
fungua banda la chipsi uswahilin me niko kwnye mchakato huo uswahili kwetu laki tano inaweza tosha kwa kuanzia
a.location 60000
b. aluminium frame 80000
c.meza ya kibishi 80000
d.vyombo jiko karahi 100000
e.kuku 5,vianzi nusu gunia , mafuta lita 20 180000
mengineyo mambo ya nyanya kabage 50000
 
Naomba uwakala wa kukuletea kuku
fungua banda la chipsi uswahilin me niko kwnye mchakato huo uswahili kwetu laki tano inaweza tosha kwa kuanzia
a.location 60000
b. aluminium frame 80000
c.meza ya kibishi 80000
d.vyombo jiko karahi 100000
e.kuku 5,vianzi nusu gunia , mafuta lita 20 180000
mengineyo mambo ya nyanya kabage 50000
 
Wadau,

Nipo katika mchakato wa kutengeneza orodha ya biashara ndogo ndogo zenye kuhitaji mitaji midogo isiyozidi 2,000,000/=, ambazo unaweza zungusha mtaji wako na kupata faida kati ya 20% na kuendelea ya mtaji wako ndani ya mwezi mmoja.

Kwa mfano, biashara ambayo mjasiriamali anaweza zungusha 1,000,000/= na kuwa na uwezekano wa kujipatia kipato cha 200,000/= kwa mwezi, baada ya kutoa ngarama zote za kufanya biashara.

Hapa sizungumzii biashara ambazo unahitaji uwekezaji mkubwa mwanzoni (mfano kama kujenga banda, au kulipia kodi ya mwaka mzima).

Hapa nazungumzia biashara kwa mfano uchuuzi, mtu anaweza kununua bidhaa sehemu moja na kwenda kuuza sehemu nyingine. Mfano mzuri ni kama mtu anaenunua samaki, kisha kwenda kuuza kwa reja reja. Au biashara kama ya mitumba, ambayo unaweza kununua "bale" na kuliuza ndani ya mwezi mmoja.

Orodha hii nitaichapisha rasmi kwenye PDF ambayo itawekwa hapa JF.

Pia, nitakua na kipindi cha ujasiriamali ambacho kitakua kinafanyika kwenye radio mara moja kwa wiki. Nina nia ya kutumia orodha hiyo hiyo kwa ajili ya kutoa mawazo ya ujasiria mali na kupata mikopo kwa wasikilizaji.

Nitawafahamisha pale vipindi vitakapoanza kwenye redio.

Natumaini kupata mawazo toka kwenu.

Ram

UPDATE: 22th Sept, 2014
Hadi sasa, biashara ambazo nimeweza kuzifanyia kazi ni biashara ambazo zina return nzuri kwa mwezi, ila capital yake ni kubwa kidogo. Hapa tunazungumzia kuanzia 25Mil - 30Mil kama startup capital.

Ila ni biashara ambazo unaweza pata gross profit ya 35 - 40% ya capital kwa mwezi. Hivyo unaweza pata return ya investment yako ndani ya Miezi 4 - 5 kwa makadirio ya haraka haraka.

Kwa namna nyingine, unaweza ona kuwa wajasiriamali wadogo wanahitaji kuunganisha nguvu pamoja ili kuweza kufanya biashara zinatohitaji mitaji mikubwa.

Tutaendelea kujuzana hapo majaliwa.


UPDATE: 24 Oct, 2014
Lengo la kuanzisha uzi huu ni ili watu wenye uzoefu tofauti tofauti kwenye mambo ya biashara tuweze kuchangia mawazo na kuweza kuangalia kama kuna namna ambayo tunaweza kuwasaidia wale ambao wangependa kuanza biashara, ila hawana uzoefu, taarifa, au mitaji.

Tofauti na wengi wanavyofikiri, lengo hapa haikuwa kwa mimi kutafanya tafiti, na kukusanya taarifa huku na huko, kisha kumpa yule ambae hayuko tayari kutoa mchango wowote.

Hili ni jukwaa la wote, na kila mtu ana uwezo wa kuchangia wazo lolote lile alilo nalo - liwe zuri ama liwe baya.

Asante kwa wale wanaochukua muda wao kuchangia.

Kwa wale wanaopenda kulishwa (spoon feeding) kwenye kila kitu, kila laheri.
 
Ramthods ..... you are always an inspirational if member ....

nitakuunga mkono kimawazo and technically

Very very good idea
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom