Kila Biashara inaweza kuwa endelevu.., Wachina wana msemo hata safari ndefu inaanzia kwa hatua moja.
Kwa maana hiyo tafuta chochote kinachoweza kununulika sehemu ulipo kwa bei nafuu na uza kwa bei yenye faida kidogo, baadhi ya hivyo ni:-
- Kukata matunda kuweka kwenye containers na kuuza
- Kuuza voucher pamoja na vingine vidogo vidogo (nunua vitu vya jumla uza reja reja)
- Pita kwenye mahoteli na migahawa chukua tender nenda nje ya mji nunua kuku, samaki, mboga mboga n.k. uzia hizi hoteli na migahawa kwa faida ndogo
- Uza magazeti (hii huitaji mtaji) nenda kwa wakala atakupa magazeti, ukiuza faida yako, yakibaki unarudisha, (hakuna hasara)
- Nunua Boda boda endesha mwenyewe au kama kuna kijana muaminifu akuendeshee
- Nenda kwa wanaofungua robota za mitumba chagua nguo nzuri nzuri zifue na zipige pasi utembeze maofisini
Utaona kwamba vitu vya kufanya ni vingi issue ni kwamba location yako kuna mahitaji yapi na wewe upo tayari kufanya kipi, kumbuka sio kila anachokifanya huyu..., yule anaweza kukifanya hulka za watu na salesmanship zipo tofauti fanya kile ambacho wewe upo comfortable na kwenye vyote fanya SWOT analysis uone kipi kitakufaa wewe, usiige kwamba fulani kafanya kafanikiwa ukadhani ni given na wewe ufanikiwa