Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kuna mdau alishauliza kuhusu biashara endelevu hapa..

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-gani-hapa-tanzania-una-faida-sana-wadau.html

Na kwa ushauri nikamjibu kama ifuatavyo

Kila Biashara inaweza kuwa endelevu.., Wachina wana msemo hata safari ndefu inaanzia kwa hatua moja.

Kwa maana hiyo tafuta chochote kinachoweza kununulika sehemu ulipo kwa bei nafuu na uza kwa bei yenye faida kidogo, baadhi ya hivyo ni:-

  • Kukata matunda kuweka kwenye containers na kuuza
  • Kuuza voucher pamoja na vingine vidogo vidogo (nunua vitu vya jumla uza reja reja)
  • Pita kwenye mahoteli na migahawa chukua tender nenda nje ya mji nunua kuku, samaki, mboga mboga n.k. uzia hizi hoteli na migahawa kwa faida ndogo
  • Uza magazeti (hii huitaji mtaji) nenda kwa wakala atakupa magazeti, ukiuza faida yako, yakibaki unarudisha, (hakuna hasara)
  • Nunua Boda boda endesha mwenyewe au kama kuna kijana muaminifu akuendeshee
  • Nenda kwa wanaofungua robota za mitumba chagua nguo nzuri nzuri zifue na zipige pasi utembeze maofisini

Utaona kwamba vitu vya kufanya ni vingi issue ni kwamba location yako kuna mahitaji yapi na wewe upo tayari kufanya kipi, kumbuka sio kila anachokifanya huyu..., yule anaweza kukifanya hulka za watu na salesmanship zipo tofauti fanya kile ambacho wewe upo comfortable na kwenye vyote fanya SWOT analysis uone kipi kitakufaa wewe, usiige kwamba fulani kafanya kafanikiwa ukadhani ni given na wewe ufanikiwa

Hizo nyingi nilizoweka hapo juu haziitaji mtaji mrefu.., ILA /KUMBUKA katika kitabu chako usisahau kuwaambia wadau kitu chochote kama kina faida kubwa na mtaji mdogo (yaani ni rahisi kwa mtu yoyote kufanya) basi mwisho wa siku wengi watafanya na demand itakuwa ndogo kulingana na supply.

PILI Investment sio Pesa peke yake, mtu anaweza akafanya biashara yenye mtaji mdogo ila ikabidi uweke muda wako mwingi hence gharama zikawa kubwa zaidi sababu muda ni PRICELESS..., unless unatumia leverage.., yaani making other people work for you.., mfano kama unasambaza chakula maofisini unaajili watu wakusambazie hata kama unawalipa 95% ya faida ila 5% inayobaki ni bora sababu unakuwa hujatumia muda wako na pesa imeingia..
 
watu kama nyie mungu awanyoshee rehema ukipatacho ukala na wenzanko mungu kamwe hakutupi wazo zuri tunalisubiria mkuu asante sana.
 
Kukiwa na biashara kama hyo. You must be a genious.
 
Kukiwa na biashara kama hyo. You must be a genious.

Kaka, zipo, ila sio kwa mitaj ya 2mil

Mimi napata 30% monthly ya capital, and I am not a genious

You dont need to be a genious, just a risk taker
 
kama uko eneo kuna wakulima wakopeshe kwa kurejesha kwa magunia mfano tsh 30000 kwa gunia la mpunga ambalo ukiliuza ni tsh 70,000 au zaidi
 
kama uko eneo kuna wakulima wakopeshe kwa kurejesha kwa magunia mfano tsh 30000 kwa gunia la mpunga ambalo ukiliuza ni tsh 70,000 au zaidi

MBONA VOCHA ZA ELF50 ZINAINGIZA FAIDA GHAFI YA EL2500 KILA SIKU?
Je kwa siku 30 haitakuwa elf 75 na kwa mwaka si ni lak9?-
biashara za mtaji kidogo faida kubwa zipo ila zingine za kishenzi
 
Back
Top Bottom