Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Mwasalemba je naweza kusafirisha kifurushi kidogo majini, kwa mfano vitu vya wanawake kama jewels?


Inategemea boss...

1.wasafirishaji wa maji wanakupimia kadri ya ukubwa wa kiboksi chako,hivyo yawezekana...nenda kwa ao jamaa ofisini kwao town,au chukua namba yao kwa instagram chat na jamaa mueleze ukubwa wa mzigo wako atakwambia gharama (natumaini supplier wako kakueleza uzito wake na dimensions zake)
2.au kama kidogo saaana huna aja ya kusubiri mwezi mzima wakati kuna wabeba vifurushi,kikubwa kubalance gharama za manunuzi nunua vitu vizuri lakini kwa supplier amabe yupo cheap zaidi au ambae gharama zake zipo na free shipping,manake nini?lets say umenunua bidhaa zako chini ya dola moja so ata ukija piga hesabu baadae gharama za usafiri kwa ndege ni sawa na kila item umesafirisha si zaidi ya dola 2 au 3,bado unakaa vizuri,kikubwa nenda pugu road waone aramex au skynet...dhl weka pembeni kwanza,unaulizia tu kwamba unamzigo wa uzito fulani watakupa gharama,alafu pia nadhan kuna option yakuweza kulipia uku,so ktk ofisi yao ya uko wata confirm tu uzito wewe utalipa uku.
3.njia ya posta ambayo nayo ni uhakika...na ipo kawaida sio bei juu wala sio chini lakini naamini inafaida pia.

Nakuwekea screen shot apa nimepiga kwa simu yangu...kama mfano;

Nimekuwa kama nataka nunua bracelet pisi 50
ambazo jumla yake pamoja na usafiri imekuja dola 68.80
68.80×1840=126,592/- (dola 1=tshs 1840)...hivyo bracelet 50 ni sawa na Tshs 126,592/-
126592÷50=2531.84,hivyo ni sawa na kusema kila bracelet moja ni Tshs 2531.84
Kumbuka kuna makato yakutuma io pesa wakati wa malipo,lets say kutuma io dola 68.80 utachajia dola 8-10,hii nayo lazima iingie katika manunuzi,so 10×1840=18400...18400÷50=368,hivyo ni sawa na kila moja ulilipia 368,so gharama za jumla ni 368+2531.84 =2899.84...hivyo adi inafika dar io bracelet takuwa nimenunua 2899.84 sasa wewe ukiuza kila moja elfu 8 adi 12 apo umekosa nini? ioio bracelet angalia watu apa bongo wanauza bei gani?adi elfu 15...okay poa boss

NB:kumbuka uo ni mfano tu,jewels za kike zipo nyingi sana.
 

Attachments

  • 1424627446185.jpg
    51.9 KB · Views: 1,146
Mkuu Ndg.MWASALEMBA. pole na majukumu na hongera kwa elimu hii unayotuelimisha, nimetembelea mtandao wa alibaba na kuona products nyingi, ninachoomba unifafanulie ni kuwa nawezaje kukusanya mizigo yangu kutoka suppliers tofauti tofauti na kuwa mzigo mmoja, mfano naagiza nguo za watoto kutoka supplier A, jewelry kutoka supplier B, saa za mkononi kutoka supplier C. Nisaidie ufafanuzi hapo mkuu. Ubarikiwe sana
 
Last edited by a moderator:


Asante sana mkuu, ubarikiwe. nikiwa na swali lingine nitakuuliza.
nimewahi kuimport kwa kutumia njia hii ila nilitumia dhl charges zilikuwa kubwa sana na bidhaa nilizoleta sikuwa nimefanya research ya kutosha hazikutoka nikawa disappointed nikaacha sikuagiza tena. nilisearch for suppliers na kucheki prices kwenye sites tofauti aliexpress, alibaba na madeinchina nikampata mmoja kwenye made in china he is a good supplier kwa kweli na bei zake nikicompare na wengine pia ni nzuri.

anyway, umenifanya nifikirie kuanza kuimport tena. Thankx much Mwasalemba.
 
Mpangamji
Sorry kiongozi for late reply,majukumu kaka! Aaah,kwa alibaba either kila supplier mpe apeleke kwa uyo forwarder mizigo itakutana uko then itakaa pamoja,maana kwa alibaba hakuna kapu la manunuzi kama aliexpress n.k...kila supplier apeleke kwa msafirishaji basi,ikifika uko unaweza mwambia jamaa wapo friendly kwamba asikilizie siku kazaaa mzigo mwingine atapelekewa achanganye thats all,au acha kila supplier akifanya delivery mzgo itakuja na itapimiwa gharama tofauti kulingana na vipimo,uzuri unalipia kulingana na ukubwa wa mzigo.sorry bhana nilikuwa na mishe mingi
 
Last edited by a moderator:

:thumbup::thumbup::thumbup:
 
Nimemaliza form 4 nipo tu nikipewa mtaji wa laki moja au mbili nifanye kazi gani?
 
Nimemaliza form 4 nipo 2 nikipewa mtaji wa laki moja au mbili nifanye kazi gan??

Kama uko kijijini, nunua kuku majike wa kienyeji 12, madume 2. Pesa itakayobaki iwe kwa ajili ya chanjo, hao kuku watunze kama mboni ya jicho lako, baada ya mwaka mmoja utakuwa na kuku 100. Hapo uwezi kukosa milioni moja. Endelea kufaga kwa miaka miwili ukiwa serious, utakosa milioni 2. Baada ya hapo tafuta mahala pazuri ufungue hata duka, au biashara ambayo utaipenda. Nimekuwekea miaka 2 kwa sababu kama umemaliza form 4 bado una umri mdogo kwa hiyo huna cha kupoteza kama ukijipa muda
 

Nimeipenda idea yako.
 
Nimeipenda idea yako.

Umeipenda sawa ila mbona huulizi kama upo mjini je? au umeamua kuhamia kijijini kabisa?

Nb: ukiwa mjini hiyo hela ni ndogo sana ila ukiwa huna aibu za kijinga hiyo ni kubwa sana, unaweza ata anzisha biashara za kuuza matunda, hasa huku mjini, utapata sana, nenda stereo nunua nanasi (japo msimu umeisha), tikkiti na maembe, hata ndizi na tango, tafuta eneo huku town, ila fanya research kwanza, utauza hayo matunda sana mda wa lunch,

ila usiwe mvivu kumenya na kuwakatiakatia wateja, bei ya matundamjini ni nzuri sana na faida utapata tu. ukiwa serious utashangaa umeongeza mtaji zaidi, huo ni mfano tu vitu ni vingi sana mjini.

Plz usionge, wala kuvuta sigara, bangi na kunywa pombe..... utafanikiwa. mdogo wangu.
 
cha kwanza aibu tupa huko,
Hayo ni maisha yako si ya yule atakayekuchekaau kukudharau,
Pili fanya juhudi kwa kile unataka kufanya
Usijiingize kwenye makundi ya kijingajinga ikibidi kuwa karibu na muumba wako,ulevi makundi ya kijinga yanapoteza dira ila laki mbili kama utakuwa mtulivu ma mwenye nidhamu itakutoa,pia uangalie mahali ulipo kuna uhitaji ya bidhaa gani ili uwe wa kwanza kuleta bidhaa hiyo!?????
 

Mjini na hawa mgambo wa jiji wanaweza kukuulia biashara yako...
 

Mkuu umetokomea wapi tena?
 
Kama sehemu ni nzuli biashara Ya genge la mboga na matunda mtaji haufika 1.5ml na return monthly ina zaidi Ya 40% kama faida na kama ni sehemu nzuli yenye biashara utapata zaidi
 
RED: Chief Elungata... Hebu nisaidie maarifa hapo tafadhali..
 
Starring kafia kwenye maua ya kwa azizi ally(mtoa mada) hadi leo hajaonekana tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…