Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

geofreyngaga
Ni kweli tupu...simu ifanye kazi hiz:
1.iwe chanzo cha kupata taarifa toka vyanzo mbalimbali za kibiashara
2.iwe chanzo cha kuwafikia wateja,tena wengi kwa wakati mmoja uku wewe ukiwa umekaa sehem moja tu,so njia ya usafirishaji malighafi
3.iwe daraja la matangazo la bidhaa yako
4.iwe chanzo cha kipato chako
5.iwe nukuu ya database ya wateja wako,masoko yako n.k
6.iwe secretary yako

NB:inawezekana...ndio maana kuna point awali niligusia umuhimu wa simu yenye android kwani utazipata apps nyingi kwa urahisi,miongoni mwa izo app ni jamiiforums,aliexpress, e.t.c

Itaendelea...
 
Last edited by a moderator:
Angalizo lingine...

Hii ipo sana katika soko la alibaba,wauzaji wa bidhaa,machines,na vinginevyo wengi wana minimum order ya bidhaa wauzavyo,hii isikukatishe tamaa,wa'janjawanja'...io ndio ngao kupunguza kukutana sana na wateja wa retail,maana target yao kubwa ni wholesale customers,so wewe muingie fanya maongezi na maulizo kadri uwezavyo,zaidi katika yote hayo unamdadavulia as if akikubali tu unafanya manunuzi muda uouo yani una place order right a way,kumbe nawe ni m'janjamjanja'.

Zaidi...hakikisha kabla ujaanza kufanya mawasiliano uwe umeupitia vema mtandao husika katika category zote zilizopo,pitia kwa msingi wa suppliers au products e.t.c vyovyote uwezavyo.Kumbuka kuwa na taarifa zaidi juu ya vitu asa utakavyo penda kuanza navyo kununua kwa ajili ya biashara,naamini ndani ya siku 14 kama umeipitia kwa makini utakuwa na vitu kichwani.

NB:jikite zaidi katika supplier mwenye kiambato cha video katika home page yake,kuepusha risk ya kukutana na tapeli (kila supplier asaivi ni lazima awe na video kuonesha sehem yake ya kazi) ingawa wapo ambao bado hawajaweka,wazuri tu...lkn kwa sasa waache,dili kuwafatilia zaidi wenye video maana naamini kama ukija kuamua kuanza ndio utaanza na miongoni mwao.

Itaendelea. ..
 
Nukuu muhimu. ..

Katika masoko hayo kuna kila bidhaa,mfano;-
*nguo na kofia;za kike,za kiume,za watoto,za shughuri kama harusi n.k
*viatu;vya jinsia zote na wakati wote
*mikanda na mikoba;ya jinsia zote
*vifaa vya simu na simu
*vifaa vya nakirishi na umeme
*vifaa vya thamani na nyumbani
*mitambo ya shughuri mbalimbali kama uchimbaji madini,ushonaji,na vinginevyo
*vifaa vya ofisini na mashuleni
*zana za kilimo na ufugaji
*mitambo ya uzalishaji malighafi
*na mengine meeengi

Sasa,pindi unapokuwa unafanya tathimini ya kile unachofikiria kukifanya,hakikisha katika vipaumbele vitatu utakavyochagua viingie kwa kina zaidi,fulsa ipo apo.

Wakati ukifanya hayo,toa hofu kwamba utasafirishaje,ni rahisi tu...taeleza hili nukuu ijayo

Itaendelea. ..
 
Endeleza mkuu usafirishaji hapo mpaka maswala ya kodi na tbs na vingine

...inaendelea

Hapa kabla ya kugusia namna ya usafirishaji na kadharika,naomba nikumbushie lile swala la laki 300,000/-Tshs kama ndio mtaji (kama kiasi cha chini kuanzia ukiwa kama importer).
Kama unayo zaidi,murua kwako...lakini katika izo category nilizozitaja,baadhi tu na nyingine nyingi zilizopo kwenye io mitandao,hakikisha unafocus zaidi kwenye category ya biashara utakayo hitaji ifanya ili upate somo na picha nzima.

Hakikisha unachagua vitu hivi vidogo vidogo,ata kama una wazo lakufanya mabiashara makuuubwa,anza na uagizaji mdogo then naamini mara mbili tatu,ya nne unachip in katika uo mpango wako mkubwa,mfano chagua biashara za kununua maua,au saa za ndani au mikononi,nguo za kike au kiume au watoto,kofia mbalimbali,au viatu,au vitu vya mapambo,vyombo mbalimbali n.k usianze na mimashine yenye kuhitaji pesa nyingi.
( kumbuka ununuzi huo unafanya kwa supplier ambae ana video katika kurasa yake usinunue kwa ambae hana video,ukizoea ndio utafahamu namna nyingine ya kutambua truly supplier ambae sio tapeli).

Zingatia haya na yafahamu haya pia ufanyapo ununuzi hasa katika masoko ya china;
*masaa 24 (isipo kuwa kipindi cha sikukuu kwao) wapo attention kumsubiri mnunuaji hivyo wewe ni lulu kwao
*hii inaambatana na point ya kwanza,kutokana na kwamba wewe ni lulu kwao mara nyingi hayupo tayari kukupoteza so negotiate kadri uwezavyo,atakulinda usipotee,mfano kitu cha dola 20,wewe muanzie unataka kwa dola 7,ili bandika bandua mtakoma kwenye dola 10-12,kwani akikuambia dola 20 wewe ukapunguza kidogo inakula kwako.
*jinsi mtakavyo anza kufanya biashara mwanzoni ndio mtakavyo zoea maisha yenu yote ya wewe na yeye ivyo mantain mwanzoni,mnyonye mwanzoni.
*usistuke kwamba kitu unachotaka kakupa kwa bei ndogo ivyo yaezekana ukikiacha mwingine atakuwahi atakinunua,HAPANA,vipo viiingi kama hivyo so stick katika kumlalia.
*unachonunua kwa supplier wa alie na video katika kurasa yake,ndio halisi kitakavyo kuwa kwa macho yani hakuna tofauti ya picha na bidhaa,so usinunue sample,save io pesa ya sample.

Nadhani...inatosha kwanza,nimeona haya ni muhimu zaidi kuyaeleza kabla sijafika katika namna ya usafirishaji na kadharika. ..hivyo uandishi ujao ni namna ya kuufikisha mzigo wako TZ baada ya manunuzi, zingatia hii😀ELIVERY ATAIFANYA CHINA ONLY,sio TZ,so akupe bei FOB ya china,na atafanya delivery ndani ya china kwa maelezo utakayo mpatia.

Itaendelea. ..
 
Inaendelea. ..

Sasa ukisha m'mudu supplier wako katika makubaliano ya bei ya bidhaa yako n.k kumbuka ulimwambia atafanya delivery ndani ya apoapo Dubai au China au Thailand,and ofcoz apa jifanye kama hato weza kukufanyia delivery kwa forwarder wako basi dili inakuwa imekufa,nakukuakikishia atakubali lkn anaweza kukutingisha kidogo kwamba ooh labda mm nipo mbali na uyo forwarder wako so changia pesa kidogo labda dola moja kwa kila item mgomeee,kwanini? Hii gharama lazima aibebe yeye coz gharama za office delivery ndani ya io miji ni ndogo saaana so sio tatizo kwake,hivyo atafanya delivery tu...mostly (97%) suppliers hawana shida na hilo.

Kumbuka apo tayari wewe unataarifa za kutosha juu ya kampuni hizi za usafirshaji,ambazo sasa ndio tutazizungumzia kwa uchache,kampuni hizi zipo zinazosafirisha kwa anga na zipo zinazosafirisha kwa maji,so uchaguzi ni wako kulingana na mzigo unaosafirishwa.

Kwa anga wanazingatia hivi vitu; uzito+vipimo vya mzigo yani dimensions,wakati
Kwa maji wanazingatia hii tu;dimensions (urefu×kimo×upana)

So wewe ndio wafahamu kitu gani umenunua na unakihitaji kwa muda gani,mara nyingi kwa anga haizidi siku 5 mpaka 15 wakati majini ni siku 30-34 mpaka mzigo ukufikie wewe...

Sasa hapa kabla ujafikiria juu ya usafirishaji,zingatia juu ya kile unachotaka kusafirisha...kwani kila namna kati ya izo mbili inafaida na changamoto zake.mfano;anga mara nyingi ni gharama lakini ni haraka zaidi wakati maji mara nyingi ni nafuuu zaidi lakini mwezi mzima unasubiri. Hivyo basi kwa mfanyabiashara wa kweli asa anae anza binafsi napendekeza usafiri wa maji kwani utakusaidia kukuza mtaji kwa kiasi kikubwa mno kuliko ndege,pia kumbuka apa nakupa option yakuanza biashara ya wewe kuwa importer bila ya kusafiri hivyo ni njia inakayo kukuza kimapato pia,ukisha kuwa ndio anza safari ata mara moja kwa mwaka,unamit na wale supplier wako kwa kuweka mazingira mazuri zaidi,na kufamiana.(nauli kwenda na kurudi+maradhi ni mtaji mkuuubwa uo).

Naomba nitaje kampuni hizi kwa uchache,hizi ni miongoni unazoweza zitumia bila shaka nakuakikishia mzigo wako utakufikia hapa pasi na shaka,nadhani tutaziingia kidogo nukuu ijayo;

a.DHL
b.ARAMEX
c.Silent Ocean (sky sea)
d.skynet
e.posta na kadharika

Kumbuka hizi ni forwarders hivyo baadae takuja kuelezea pia namna ya kuimport ww mwenyewe bila kutumia forwarder alafu utapima,lakini kwa uzoefu naona kwa kuanzia bora utumie forwarder.

Itaendelea. ..
 
Tunaendelea. ..

Sasa,hatua ya kwanza ilikuwa upembuzi wa kina juu ya nini unataka au unapendelea kufanya,pia baadae ikaja kukoncetrate kwa category zile ambazo ndio ungependa kudili nazo zaidi,hapa naamini ata kama sikugusia uliweza au utachukuwa namba za simu ya mkononi ya supplier anaeuza vitu unavyotaka (namba zao mara nyingi zipo whatsapp au wechat ) ndio umuhimu mwingine wa android phone apa,maana namba ya simu ni rahisi zaidi kuwasiliana na ni muda wowote,kama sample mbalimbali anakutumia kwa simu unaona n.k pia wewe unakuwa na uwanja mpana pia wakumuomba sample mbalimbali zaidi.

Kama ujaweza fanya hivyo basi bora ufanye (chukua namba za simu za mkononi za supplier wengi kadri uwezavyo). Kama ufahamu namna ya kuchukua namba,bora uliza na utaelekezwa. Ikaja ngazi ya wewe na supplier wako kuchat adi unafikia hatua ya kuingia katika makubaliano ya kutaka kununua,then akakutumia picha mbalimbali ya kitu unachotaka nunua lengo likiwa kujiridhisha muonekano na ubora maana ni picha halisi na za ukaribu,mwisho ndio tupo katika namna ya kufikisha mzigo wako bongo,maana tulimwambia atafanya delivery apo apo nchini mwake...sasa ayo makampuni niliyoyataja hawali yapo miji io mikubwa yote (Thailand, Dubai na China) i mean miji ya izo nchi.

Sasa nikianza na usafiri wa anga,umeshafanya upembuzi wa kile unachonunua unafikiria je hiki nasafirishaje? Uzito wake?dimensions zake?n.k kwa kifupi kampuni nyingi za usafiri wa anga ukitoa posta,kusafirisha 1kg gharama ni 10USD,zikipishana labda 1USD au 2USD hivyo unaona kabisa jinsi mzigo wako unavyoweza kuwa gharama kuusafirisha kama ni mkubwa,watu wengi hasa akina tomaso (wapo hawa-ambae anaogopa ununua kitu A akaletewa bidhaa B) utumia kampuni hizi kusafirisha sampo. Kumbuka ukiwa kama beginner nilikusisitiza kununua kwa supplier alie na video ili ukwepe swala la sample,hawa 100% ni wauzaji kweli na picha zao ni halisi (pesa ya kununua sampo ongezea katika mtaji).

Hivyo basi ukiona utaitumia moja ya kampuni hizi unamuagiza supplier wako akafanye delivery kwao yeye akupe tracking number tu ya mzigo (apo tayari umempatia supplier wako address yako full). Yani namba ya simu,jina,mkoa n.k...

Uzuri wa hizi kampuni za anga ni maharufu zaidi,so kila supplier anafahamu ofisi zao,kama hafahamu ingia google tafuta office ilipo (google hivi làbda 'dhl office in Guangzhou' itaĺeta location adi namba ya simu,mpe namba yeye awapigie,hakuna shaka juu ya hilo.
Tutaendelea na namba ya kusafirisha kwa njia ya maji na gharama zake+tra+tfda kama inatakiwa+tbs kama inatakiwa n.k

Itaendelea. ..

NB:waeza kwenda kwenye izo office apa Dar,ukawaambia kuna mzigo wako kwa address flani nao watakusaidia,they after Mr Benjamin, mind you that...
 
Alert...nduguzi nikipata muda tena,nitamalizia mwisho katika usafirishaji kutumia maji,na nitaeleza case study ya kampuni moja unayoweza itumia kukusafirishia mzigo,then naamini kuanzia apo wewe binafsi ni juhudi zako kusaka taarifa zaidi,kwani ingekuwa vema ingepatikana na muda wa maswali niweze kuyajibu lakini naona imekuwa changamoto, though ol is good,so natumaini nimeeleweka kwa haya machache,sorry kwa nitakae kuwa nimemuacha na ajanielewa kwa namna ya uandishi,na hongera kwa ambae atakuwa amenielewa na akafanyia kazi,zaidi...maisha ndio haya haya yakija mengine tunayaita maendeleo au kupyaya...tafuta mali ukiwa kijana (29yrs-39yrs) zaidi ya apo usimamizi tu wa mali na kuziendeleza mali si utafutaji tena...aksanteni
 
Back
Top Bottom