Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

nenda arusha sehemu inaitwa ol kokola kachukue bange ,halafu zungukia maeneo yote ya ofizi za chadema ni wateja wakubwa wa hayo makitu
 
Fuga kuku wa kienyeji anza na Jogoo 2 na kuku majike 3 Kuku hawa wafuge kienyeji waache watembee wenyewe kutafuta chakula kila kuku atawanunua kwa sh. 10,00o jumla sh. 50,0000 pesa zitakazobaki atanunua madawa na kuwatunza. Hesabu ya ongezeko kila mwezi kuku 3 watataga mayai 30x6 anaweza kuwa na vifaranga 180 pamoja na kuku wakubwa watakuwa 185. Baada ya miezi 6 wale vifaranga watakuwa wakubwa nao wataanza kutaga nao ambapo hali itakuwa hivi nusu ya wale vifaranga inaweza kuwa majike baada ya mwaka 1 utapata kuku 95x mayai 10x6= utakuwa na kuku 5700. ukijumlisha na hao wa mwanzo utakuwa na kuku 5700 +185= 5885 ukiwauza utapata 5885 x bei ya 10,000= sh. 58,850,000.00. Faida ya kuku wa kienyeji ni wavumilivu wa magonjwa hawana ghrama kubwa kuwatunza wanajitafutia chakula. Unaweza kuuza mayai na nyama hasa majogoo kwa kuwa yanakua haraka.

Daah ngoja nifanye mpango nianze kufuga kuku....
 
Hivi kuku 5885 unaweza kuwatuza / kuwafuga kwa kuwaachs wazi wajitafutie chakula???? Jameni tuwe wakweli labds kama unataka atowe sadaka mtaani
Kwa mimi nionavyo hao kuku 5885 itabidi awafuge kisasa yaani ndani ya banda ambako kuna wastani wa usalaama kuliko kuwaachia wajitafutie chakula
 
mkubwa, kukupa ushauri wa jumla juu ya biashara ni vigumu sana, ungesema upo wapi, unajishughulisha na nini kwa sasa (kwa maana ya kwamba je utakua na muda wa kuendesha biashara fulani ama la). Tuanzie hapo
 
Me nauza natural juices!! Hasa hasa ya ukwaju!!! Iko poa sna bt yahtaj kujituma sana!! Ona sasa pindi laisha saa 12:45 yanibid nitoke mapema kwenda kwenye maandalzi!! Ikifka saa 1 kamil uck naanza sambaza mpka saa tatu na nusu nimesha,alza!! Naoga nala then napiga msuli!! Nimeulza mkuu yuko chuo gan?
 
Hakuna hela ndogo.....kuna kipindi maisha yalinikaba sana nilikuwa sina mbele wala nyuma...wakati natafakali ni jinsi gani nitajikwamua...siku moja nilipata kibarua pale mtaani cha kuchimba shimo la choo..ambapo nilipata kama tsh 40,000/= kwa kuwa shimo lilikuwa refu kidogo....baada ya kupata ile hela nikaanza kujichana machipsi...na masoda mpaka ikabaki kama elfu kumi hivi na mia tano....wakati nipo geto nikawa najiuliza sasa hii hela ikiisha nitapata wapi tena nyingine maana sina kazi wala kibarua...hapo hapo nikapata wazo la kuuza nguo za wadada...kikwazo kikawa hela haitoshi...lakini nikaamua na hela hiyo hiyo yaani elfu kumi.....
Kesho yake asubuhi na mapema nikadamkia ilala sokoni....kwa hela yangu nilipata kama nguo nne tu...nikaenda kwa fundi nguo akanirekebishia vizuri, nikazifua zikawa zina ng'aa...nikazipiga na pasi ndio kabisa yaani kama nimezitoa dukani muda huo...
Basi mchana mwanaume nikaingia mtaani nikaanzia mitaa ya sinza, nilikuwa naingia kwenye masaloon ya wadada mpaka nafika maeneo ya kwa remi..nilikuwa na brauzi moja tu mkononi....na mfukoni nina kama elfu 45,000/=
Ile iliyobakia nilienda kuuza mwenge maeneo bamaga pale kwenye foleni kwa bei ambayo niliiropoka na mdada wala hakubisha...yaani mpaka narudi geto nina kama 60,000/= hivi...tangia hapo ndio nikawa nauza nguo za kike nikaongeza na viatu....lakini nikahamia maeneo ya posta...niliifanya hiyo biashara kwa muda mrefu na nilifanya mambo mengi ya maendeleo....mpaka siku askari wa jiji waliponifirisi...ndio nikaachana na umachinga......
Ninachotaka kusema ni kuwa hakuna mtaji mdogo kwenye biashara isipokuwa inategemea unataka kufanya biashara gani....??
 
Me nauza natural juices!! Hasa hasa ya ukwaju!!! Iko poa sna bt yahtaj kujituma sana!! Ona sasa pindi laisha saa 12:45 yanibid nitoke mapema kwenda kwenye maandalzi!! Ikifka saa 1 kamil uck naanza sambaza mpka saa tatu na nusu nimesha,alza!! Naoga nala then napiga msuli!! Nimeulza mkuu yuko chuo gan?

Niko cbe apa town mkuu
 
Nunua vocha za simu afu kaa hapo stand uuze.
 
Wadau habari zenu; hodi ktk jukwaa.

Kwenye elimu ya ujasiriamali wanasema mtu si lazima uanze biashara na mtaji mkubwa,unaweza anza hata na elf 10,nami na Tshs laki 1, nipo mwanza naweza fanya baishara gani???

Lima bustani wauzie watu utatoka
 
Njoo changia. SITI. FOUNDATION TANZANIA
 
Fikiria kama mtu anakudhulumu laki 1 utajisikiaje? kwa jicho la kijasiriamali laki 1 ni hela nyingi mno. tulia jipange uanzishe biashara kama wadau walivyokushauri utawini. baada ya hapo uje ulete mrejesho
 
acha kujitia stress....nenda arusha, fanya kazi ya tour guide....utapiga tip hadi za dola 100 kwa siku. sasa hiyo laki moja si ni kama dola 54 tu....fanya kazi bro.laki moja si mtaji mtu asikudanganye
 
Hivi kuku 5885 unaweza kuwatuza / kuwafuga kwa kuwaachs wazi wajitafutie chakula???? Jameni tuwe wakweli labds kama unataka atowe sadaka mtaani
Kwa mimi nionavyo hao kuku 5885 itabidi awafuge kisasa yaani ndani ya banda ambako kuna wastani wa usalaama kuliko kuwaachia wajitafutie chakula

Hata mimi nimeshangaa labda uwe kijijini....imagine unaishi ubungo
 
Fikiria kama mtu anakudhulumu laki 1 utajisikiaje? kwa jicho la kijasiriamali laki 1 ni hela nyingi mno. tulia jipange uanzishe biashara kama wadau walivyokushauri utawini. baada ya hapo uje ulete mrejesho

Endelea tu kumfariji!!! laki 1 ni hela ndogo sana kufungulia mtaji
 
Back
Top Bottom