Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Habar wana Jf nina laki tano mfukon nataka nifanye biashara je naweza fanya biashara gani?

Anzisha biashara ya kutengeneza mkaa wa kisasa ambayo soko lake si la kutafuta lipo na pia unaweza anza na mtaji hata wa sh elfu tano nipigie nikupe maelezo zaidi 0758 308193
 
Jiunge na biashala ya ufugaji
1. Kuku
2. Sungura
3. Mbuzi
Hio yote hapo juu ni mfano tu


Weks hapa kama ni biashala halali
 
Kila la kheri mkuu ucjali mwanzo mgumu lakini ipo siku pesa itakuwa inajiendesha yenyewe,kumbuka usipothamini kidogo ulichonacho hata kikubwa pia ukijakukipata utasema bado ni kidogo,mfano mzuri ni kwangu mwenyewe nilikuwa na milion moja,nikaomba msaada kutoka kwa wadau wakaniongezea kidogo(kwa mkopo) nikaanza na kununua bodaboda moja iliyokuwa inafanya kazi nje ya maeneo ya city centre dar.

Na leo hii namshukuru Mungu si haba nina uwezo wa kuongeza bodaboda moja kwa kila mwezi na nikabakiwa na hela ya matumizi,na Mungu akijalia natamani sana kuanza kumiliki mashine za kusaga na kukoboa mikoani.naweza kusema sasa nimejiajiri mwenyewe baada ya kumaliza ka elimu kangu ka chuo kikuu,hivo na wewe nakutia moyo simama usikate tamaa,hakuna milion 200 bila laki tatu. ni hayo tu mkuu kwa leo
 
Nenda Mwenge au Karume chagua nguo za kike zile grade A kisha tembeza kwenye hostel na vyuo. Hakika hutajuta
 
Mwana komaa, Ww upo wapi? Inategemea na location,
 
nakushauri ujifunze kupaka rangi na kutengeneza kucha akina dada. ni kabiashara kazuri sana kwa hela uliyonayo itatosha kwa kuanzia

Na Pia Atafaidika Na Kupata au Kupewa PAPUCHI Kwa Bwerere ILA Avumilie Tu Kwa Yatakayomkuta Akifumaniwa.
 
Mbona sikuelewi.. Niianze mimi kivipi. Nina biashara zangu ambazo mtaji wake ni zaidi ya 200m wewe ndiye ulieanzisha thread ukaomba ushauri wa aina ya biashara kwa mtaji wako wa laki 3 na kuna mtu ukamjibu kwa unataka kufanya biashara kuhusiana na vitu vidogovidogo vya wanawake. Napenda nikutaarifu wewe moyo wako kwamba sijafurahi na majibu yako kwenye thread yangu, pia nakuona wewe si mwelewa, na kwa taarifa yako biashara ya kupaka rangi na kusafisha kucha akinadada inayofanywa na vijana wengi wanaozungukazunguka na wengine wameweka vijiwe sehemu mbalimbali ambazo sio rasmi sana inalipa sana na mtaji wake ni mdogo sana. Fanya uchunguzi na usikurupuke kutoa majibu ya hovyo kwa watu usiowajua.

Misifa Camp! Waswahili Bhana...............Taaaaabu Tupu.
 
Kuvunja moyo kivip mkuu? Nenda kinondoni uone watu vitumbua na maandazi vinavyowatoa!! Au kama vp ngoja tumshauri kama unavyotaka wewe,moyo wangu agiza magari japan uwe unauza hapa bongo yanalipa sana!!

Labda Wakati Anayauza Na Hayo Magari Na Yeye Pia Ajipige Bei au Mnada.
 
mwanajamvi mwenzangu mbona tunakashfiana! Naami nilimpa ushauri mzuri mwananchama mwezangu aliyeomba ushauri nashangaa sana akanijibu sivyo kwamba nikafanye mimi mwenyewe, nikamjibu ukweli mimi ninabiashara zangu ambazo ninazifanya za zaidi ya 200,000,000/= . sasana wewe sijui umetokea wapi unaanza kunikashifu. sijafurahishwa kabisa na kitendo chako kuwa mstaarabu DullyJr

Kumbe Hujamkaribia Hata Idrisa Sultan Mshindi Wa BBA? Bado Ni Choka Mbaya Japo Unajitutumua...Big Up Lakini!
 
Nafanya kazi wakuu na kila mwezi nalipwa laki tano, sasa nahitaji kufanya biashara na kutokana na eneo nililopo nimepanga kuanzisha duka la kawaida... Sasa najua huku kuna washauri wazuri kwakua nina wazo hilo na wazo la kuwa na duka la nguo nitakazokua nachukulia Uganda...kinachonisumbua ni kwa uzoefu wenu nianze na biashara gani?

NB:Namweka MTU kwenye biashara Mimi ntabaki msimamizi.
 
Mshika mbili moja humponyoka. Kama unataka kufanya biashara acha kazi uliyonayo au ajiri mtu ktk biashara utakayofungua.
Duka la nguo linalipa kwani kuna jamaa yangu hakuenda hata ile elimu ya msingi lakini kwa sasa maisha yake yako juu. Jamaa alianza na biashara ndogo ya kuuza vitenge nyumba kwa nyumba baadae mtaji ulikua na mpaka anamiliki duka la nguo la jumlajumla, nyumba tatu kubwa za makazi, anasomesha watoto wake watatu international schools, ana gari (cars) tatu za kufanyia safari zake na hela ya kutosha kwenye akaunti zake bank.
Ukithubutu utafanikiwa. Ujumbe, maisha ni falsafa.


M


M
 
Sikukatishi tamaa bali amua moja. Biashara au kazi? Mtaka yote hukosa yote.

Kama ni kazi, then kazia fikra kujistawisha kazini na utafanikiwa sana tu.

Kama umeamua biashara, kwanza anza kuweka akiba kulinga na mtaji anzilishi unaotaka. Wakati huo endelea kufanya upembuzi kujiridhisha kuhusu hiyo biashara ya nguo na jinsi bora ya kuifanya upate faida na biashara iwe endelevu.

Kuna maduka mengi sana ya nguo. Fikiria na ulizia nini kitafanya ukubalike sokoni. Pembua hasa.

Unapoanza biashara, uwe ushajipanga na huna wasiwasi na unachokifanya. Hata kikifeli, unapaswa kujua kilichosababisha ili ukianza upya ujue pa kurekebisha.

Sina uzoefu sana na biashara ya nguo ila kwa yoyote ile, jua soko ulitakalo, mahitaji yake na linakopatikana ndipo uifungue huko. Nguo toka Uganda ndo bidhaa unayofikiria. Je soko unalotaka kuhudumia linataka hizo? Kiasi cha mtaji anzilishi ni gani?

Kama utafanyia dukani, ujue pia na ukubwa wa duka na namna ya kuliseti. Wengi wanaremba tu bila kujua eneo alilonalo ni dogo linamnyima fursa. Viduka vingi vya nguo vinaboa havina sehemu ya kujaribia.

Usijaribu kufanya kazi na biashara kwa pamoja. Utawapa watu mtaji na hutapata fursa bora ya kujifunza hiyo biashara. Wengi wameumia hapa na hawakomi.
 
nafanya kazi wakuu na kila mwezi nalipwa laki tano, sasa naitaji kufanya biashara na kutokana na eneo nililopo nimepanga kuanzisha duka la kawaida...sasa najua huku kuna washauri wazuri kwakua Nina wazo hilo na wazo la kuwa na duka la nguo nitakazokua naxhukulia Uganda...kinachonisumbua ni kwa uzoefu wenu nianze na biashara gani?
NB:namweka MTU kwenye biashara Mimi ntabaki msimamizi.

Je umeshatunza akiba kiasi gani mpaka sasa kwaajili ya biashara?

Je una muda kiasi gani wa kufatilia biashara yako kwa siku?

Matumizi yako kwa mwezi ni kiasi gani? Fanya ulinganifu wa mapato na matumizi kwa mwezi.

Baada ya hapo sasa fatilia gharama za kuanzisha hiyo biashara ujue itakuchukua mda gani kupata kiasi hicho.

Angalia fursa na vikwazo vinavombanata na hiyo biashara, je vipi utakabiliana na vikwazo hivyo?. Angalia uwezo wako binafsi na udhaifu wako, je vipi utarekebisha udhaifu wako?

Changanua upatikanaji wa faida kutokana na hiyo biashara, baada ya hapo anza biashara na uwe mvumilivu
 
Back
Top Bottom