Endeleza mkuu usafirishaji hapo mpaka maswala ya kodi na tbs na vingine
...inaendelea
Hapa kabla ya kugusia namna ya usafirishaji na kadharika,naomba nikumbushie lile swala la laki 300,000/-Tshs kama ndio mtaji (kama kiasi cha chini kuanzia ukiwa kama importer).
Kama unayo zaidi,murua kwako...lakini katika izo category nilizozitaja,baadhi tu na nyingine nyingi zilizopo kwenye io mitandao,hakikisha unafocus zaidi kwenye category ya biashara utakayo hitaji ifanya ili upate somo na picha nzima.
Hakikisha unachagua vitu hivi vidogo vidogo,ata kama una wazo lakufanya mabiashara makuuubwa,anza na uagizaji mdogo then naamini mara mbili tatu,ya nne unachip in katika uo mpango wako mkubwa,mfano chagua biashara za kununua maua,au saa za ndani au mikononi,nguo za kike au kiume au watoto,kofia mbalimbali,au viatu,au vitu vya mapambo,vyombo mbalimbali n.k usianze na mimashine yenye kuhitaji pesa nyingi.
( kumbuka ununuzi huo unafanya kwa supplier ambae ana video katika kurasa yake usinunue kwa ambae hana video,ukizoea ndio utafahamu namna nyingine ya kutambua truly supplier ambae sio tapeli).
Zingatia haya na yafahamu haya pia ufanyapo ununuzi hasa katika masoko ya china;
*masaa 24 (isipo kuwa kipindi cha sikukuu kwao) wapo attention kumsubiri mnunuaji hivyo wewe ni lulu kwao
*hii inaambatana na point ya kwanza,kutokana na kwamba wewe ni lulu kwao mara nyingi hayupo tayari kukupoteza so negotiate kadri uwezavyo,atakulinda usipotee,mfano kitu cha dola 20,wewe muanzie unataka kwa dola 7,ili bandika bandua mtakoma kwenye dola 10-12,kwani akikuambia dola 20 wewe ukapunguza kidogo inakula kwako.
*jinsi mtakavyo anza kufanya biashara mwanzoni ndio mtakavyo zoea maisha yenu yote ya wewe na yeye ivyo mantain mwanzoni,mnyonye mwanzoni.
*usistuke kwamba kitu unachotaka kakupa kwa bei ndogo ivyo yaezekana ukikiacha mwingine atakuwahi atakinunua,HAPANA,vipo viiingi kama hivyo so stick katika kumlalia.
*unachonunua kwa supplier wa alie na video katika kurasa yake,ndio halisi kitakavyo kuwa kwa macho yani hakuna tofauti ya picha na bidhaa,so usinunue sample,save io pesa ya sample.
Nadhani...inatosha kwanza,nimeona haya ni muhimu zaidi kuyaeleza kabla sijafika katika namna ya usafirishaji na kadharika. ..hivyo uandishi ujao ni namna ya kuufikisha mzigo wako TZ baada ya manunuzi, zingatia hii
😀ELIVERY ATAIFANYA CHINA ONLY,sio TZ,so akupe bei FOB ya china,na atafanya delivery ndani ya china kwa maelezo utakayo mpatia.
Itaendelea. ..