Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Biashara nyingi Tanzania huwa zikianza hazidumu sana zinakufa kwa kuwa sisi tunaenda kinyume nyume. Unakuta mtu amefumania milioni 10 ndio anaanza kufikiria biashara gani afanye.Yaani ilimradi tu na yeye afanye biashara. Kule kwa wenzetu unakuta mtu hana hata dollar 100 mfukoni anatengeneza wazo la biashara ambayo inahitaji mtaji wa mamilioni ya Dollar na biashara inaanzishwa na kutengemaa na kumfanya yeye awe millionaire baadae. Tuache kwenda kinyume nyume kwenye biashara.

Kuna materialists na idealists. Materialist anaanza kuwa na kitu then anatafuta wazo, mfano kama ni biashara afanye ipi wakati tayari ana mtaji. Idealist anaanza kuwa na wazo then anaangalia atafanyaje ili apate mtaji. Kwa hiyo nategemea na falsafa ya muhusika.
 
mimi ni mwanachuo mwaka wa kwanza ruaha university (ruco) iringa mjini, naomba ushauri wakubwa nifanye biashara gani niko serious ktk hili nina laki 5 ya uhakika, likizo huwa nakuepo dar, nilifikiria kufanya biashara ya nguo bt ckupata washaur wazur na sehemu ya kupatia mzigo, so nko tayar kwa ushaur abt any pocblbe business.

uza vocha haitokuumiza kichwa kwa mtaji huo
 
mi nafanya biashara ya mkaa,join na mimi nikuletee,uuze au umweke mtu auze,kama huwezi nanunua mzigo nakulllllllllletea unauuza kkwea jumla,Mkaa mpaka ufike hapa unakuwa umecost 28000 per bag,Ukiuza hapa dar unauza kwa tsh 37000 per bag,hiyo ni whole sale,,,,retail ni 40000 up to 45000 per bag,,nina kibali kabisa,,,Au kama uko ruaha tafuta shamba kama heka moja,lima vitunguu.Lima kwa kisasa,heka moja ukitumia vibarua na ni umwagiliaji unapata bag 50 mpaka 90 or 100 bag,,ukiuza kila bag sh 60000,unapata kuanzia 3m ,5m to 6m,,hiyo ni ndani ya miezi mitatu,,unakua umevuna

Jaribu hiyo ya mkaa, ya vitunguu usithubutu, utalilia chooni
 
Mishkaki ya mbwa inalipa kwa wenye mitaji midogo

kama umeshindwa kutoa ushauri unakaa kimya sio kila kitu lzm uchangie sawa mkubwa!!

Kwa mtaji huo unaweza ukawekeza hata kwenye mpesa tafuta kijana kwa hapo hapo Iringa maeneo ya chuoni kwenu awe anafanya hy ishu pole pole itakuzalishia pesa na kupata hasara sio rahisi na ni easy to manage it!
 
Fanyia utafiti zaid hiyo ya mkaa, itakulipa na ni mali isiyosumbua uuzaji wake endapo utatafuta sehemu nzuri, haiharibiki na hivyo huna wasi wasi wa kupoteza hela yako

sio kirahisi hivyo.
mali asili na idara ya msitu wamekuwa pilipili kweli.
wakikudaka unasifirisha mkaa, faini yao ni kichefuchefu!
labda uwe na vibali vyote
 
mimi ni mwanachuo mwaka wa kwanza ruaha university (ruco) iringa mjini, naomba ushauri wakubwa nifanye biashara gani niko serious ktk hili nina laki 5 ya uhakika, likizo huwa nakuepo dar, nilifikiria kufanya biashara ya nguo bt ckupata washaur wazur na sehemu ya kupatia mzigo, so nko tayar kwa ushaur abt any pocblbe business.
kama vp nunua vitabu vikusahidie katika masomo yako
 
Biashara nyingi Tanzania huwa zikianza hazidumu sana zinakufa kwa kuwa sisi tunaenda kinyume nyume. Unakuta mtu amefumania milioni 10 ndio anaanza kufikiria biashara gani afanye.Yaani ilimradi tu na yeye afanye biashara. Kule kwa wenzetu unakuta mtu hana hata dollar 100 mfukoni anatengeneza wazo la biashara ambayo inahitaji mtaji wa mamilioni ya Dollar na biashara inaanzishwa na kutengemaa na kumfanya yeye awe millionaire baadae. Tuache kwenda kinyume nyume kwenye biashara.

Sioni kama we ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea duniani, ni kama ulikariri zamani kuwa ulaya hawafirisiki, yaan daily watu wanasema biashara kubwa zinakufa ulaya, umoja wa ulaya unadidimia, af bado unabaki kusema waTz akili hazifanyi kazi kibiashara
 
jf naomba mnipe mawazo kama kichwa cha habari kinavyojieleza,nina laki 3 nataka nijumue nguo za dukani then nipeleke vijijini nikauze kwa rejareja,kwa wale wazoefu wa biashara hasa za minadani hiyo pesa inaweza kunitoa kimaisha? mimi nipo sumbawanga mjini nataka kwenda mbeya mjini kujumua huo mzigo kwa hiyo pesa,naomba msaada wa mawazo
 
ungekuwa town zingekutoa, hasa ukianzisha genge la chakula maeneo ya stendi au yeyote yenye watu wengi wa kipato cha chini na kati.

Nguo?? Sina hakika, labda mitumba lakini nikifikiria nauli?? Au uwe wale wanaouza vijijini kwa kufuata siku za minada.
 
vijiji vya sumbawanga sivifahamu,chochote kile nitakachofika kama unavifahamu naomba unipe data ya vijiji ambavyo angalau nitauza
 
Back
Top Bottom