Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

habari /wakubwa shikamooni!!mimi ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa Dar es salaam !!naombeni ushauri biashara gani naweza nkafanya kwa kiasi cha laki tano na nusu!!frame la duka lipo maan ni la mzazi wangu (anafanya biashara nae pia katika hiyo frame ,biashara ya nguo,eneo mbezi beach)nmemwomba hivyo kakubali niweke biashara yangu pia!!sijajua nifanye biashara gani nzuri ya kukuza mtaji wangu!
 
Soma kwanza, biashara baadae. Ila kama unaweza kumpata mwaminifu anza na MPesa, Tgo Pesa, ZPesa na Airel money. Hata wewe mwenyewe unaweza kuifanya hapo chuo ukawapunguzia wenzio muda wa kwenda kwenye vibanda.
 
unaweza fanya biashara ya kuuza vocha, nunua za jumla na kuziuza kwa rejareja.
 
Kama uko maeneo ya joto unaweza fuga kuku, au uza nguo, na pia fanya kitu ulikuwa unataka fanya siku zote anza kidogo kidogo
 
Laki tano?
  • Samaki kama uko bongo.
  • Mama ntilie
  • Vinywaji baridi
  • Genge
 
Broo huwa naagiza mikoba ya kina mama na kwa bei ya jumla naiuza 36000 sasa kwa laki tano unaweza pata mikoba 13 na kwa mikoa ya mwanza na dar unaweza kufanya online business kwa kupost pics kwenye social network na mahali pengine kwa marafiki na ndugu kwa 44000 na kupata faida tu brother
 
Jamani ndugu tujaribu kupendana sisi wote ndugu matusi na kushafiana haifai kabisaaa na haileti picha nzuri so sio vizuri ndugu zangu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
ushauri hakuna sasa pamekuwa uwanja wa vijembe!
 
Back
Top Bottom