kisanganyakiswata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2014
- 1,299
- 552
kama upo karibu na madeleva wa bodaboda.
tengeneza kibox cha wavu wa chuma chenye ngazi tatu pamoja na myororo wa chuma ili kufungia akikisha unabagain na fundi chuma akutengenezee kwa bei isiyozidi laki moja na hamsini. kisha tafuta sehemu ya kuweka hilo box. nunua box moja la oil kwa sh 115000 na oil ya dumu kwa ajili ya kupima kwa sh 60000 pamoja na Dumu empty la Lita 30 hili utalitumia kwa kununua petrol.kisha ongea na muokota makopo ya maji awe anakuuzia makopo ya Lita moja na nusu Lita sio mbaya ukiongeza kiasi kidogo kutoka kwa bei anayouzia kwa kilo kwa wafanyabiashara ya kununua makopo. theni Pima oil katika kipimo cha Lita moja na nusu Lita pia petrol katika vipimo hivyo. pesa itakayobakia nunua spare ndogo ndogo kama Bolt nut. bulb za indicator, break pad na stika mbalimbali.
mchanganuo
box=150,000
oil za kopo=115,000
Oil ya kupima= 60,000
petrol Lita 30=66,000
spare ndogo ndogo=109,000
JUMLA=500000
Laki moja hifadhi ili ikusaidie pale majanga yakitokea
Mapato
Oil ya kopo 6,000*24=144,000
oil ya kupim 4,000*20= 80,000
petrol ya kupima 2,500*30= 75,000
spare (109,000)*1.75= 190,750
jumla = 489,750/=
kama kwa mwezi ukauza mizunguko mitatu kwa kila bidhaa
mauzo 489,750*3= 1,469,250
manunuzi 350,000*3=1,050,000
faida kabla ya gharama=419,250/=
gharama
usafiri 20,000*3=60,000/=
Chakula 5000*30=150,000/=
jumla ya gharama= 210,000/=
Faida kuu
419,250-210000= 209,250
Fanya biashara hii huku ukisave 200000 kwa mwezi baada ya miezi kumi tafuta fremu ya jirani na eneo lako fungua duka la virahinishi na spea ndogondogo pia nunua compressor ndogo ya laki mbili tafuta fundi pikipiki mshawishi ahamie mbele ya duka lako na wewe uwe unaziba pancha na kujaza upepo pikipiki na bajaji kama nguvu unayo ya kutosha ziba ata pancha za gari
Asante umefafanua vizuri sana