Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Mkuu fungua genge zuri la kisasa uweke na samaki pia utatoka . Kwa dar-es -salaam genge linalipa sana kuliko hata duka la rejareja la mitaani.
 
Mkuu fungua genge zuri la kisasa uweke na samaki pia utatoka . Kwa dar-es -salaam genge linalipa sana kuliko hata duka la rejareja la mitaani.
Tatizo kitaa genge kila mru analo
Hivyo siyo kitu vizuri kugawana wateja
 
Anza na viatu vya mitumba nenda pale Ilala nunua viatu vya mitumba classic. Vitayarishe vizuri tembeza maofisini kwa wafanyakazi, inalipa sana ila usione aibu na usichoke dhihaka na kutembea
Aisee ni wazo zuri...nilienda pale Karume kufanya utafiti nikagundua vitu vya mitumba ya kike mfano viatu vinauzika nasikia laki 3 hadi 5 inatosha kununua balo na siku hizi mgambo hawasumbui
 
Uliwahi fanya biashara hapo awali au ndio mara yako ya kwanza ?
Maan kila biashara ina changa moto zake .

Kitu cha kwanza angalia maeneo unayo kaa yapoje kibiashara.
 
Uliwahi fanya biashara hapo awali au ndio mara yako ya kwanza ?
Maan kila biashara ina changa moto zake .

Kitu cha kwanza angalia maeneo unayo kaa yapoje kibiashara.
Sijawahi kufanya Biashara..nimemaliza chuo nimechoka kutembeza bahasha ndo nataka kujiajiri
 
Ahsante kwa ushauri

Mkuu hongera kwa kutoa michango mzuri bila Shaka unaelewa biashara za masokoni vizuri.
Mimi najihusisha na utayarishaji wa dagaa safi wa kukaanga toka kanda ya ziwa natafuta wauzaji wa jumla watakaochukua wengi kwa wakati mmoja kama debe 10 kuendelea.

Sababu ya bei yangu kuwa ya chini zaidi nauza debe elfu 35,000 kawaida huuzwa elfu 50 na kuendelea hivyo kama unajua mtu au unataka anayejihusisha na kuuza dagaa hawa naomba uniunganishe nae Tafadhali.

Natanguliza shukrani za dhati.

Weka Namba ya simu basi
 
tafuta nguo za kike na urembo wowote unaowahusu wanawake bila kusahau perfums,lotions na creams alafu cha muhimu zaid tafuta spot nzuri ya biashara iyo, yani hakikisha wakipitia njia wanaiona biashara yako

wanawake wanasoko sana na mahitaji yao na kwa hela yako nadhani unaweza kuanza pazuri tu!
 
Back
Top Bottom