Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inalipa?Usikopeshe hapo utalipwa penzi. Na biashara itakuwa mbaya.
Wauza Urembo wanahonga sana
Nina mtaji wa Tsh.600,000. Nataka nianze kilimo. Naomba mawazo yenu.
Nipo dar (mbezi beach).. Wazo la kulima limekuja tu, na sijui nilime. Nisaidie kwa mawazo.Uko wapi? Wewe kwa mtazamo wako uliwaza ulime nini?. Tuanzie hapo ili tuweze kushauriana.
Mkuu ungetuambia alifanya biashara gani mkuu hapo umetuacha njia panda tu funguka na sisi tuzame kwenye hiyo biasharaNgoja nitoe kaushuhuda kadogo.
Nakumbuka mwaka 2013. Kaka yangu alinifata home akaniambia mdogo wangu nina shida ya pesa ya mtaji.
Nilishangaa sana nikamwambia mimi sina pesa ya Mteja kaka.Akaniambia nina wazo la biashara mtaji wake ni sh 50,000/= Nipe leo ndani ya siku 3 nitakurudishia sh 60000/=.Niwe mkweli mimi ni muislam nikamwambia hiyo riba, nilipe sh 50,000/-= kama unanipa sh 60,000/= unanipa kama mdogo wako. Pia nikampa sharti hii pesa nimeiweka niongeze , kwa ajil ya kulipa kodi akaniambia usijali wazo langu nimelifanyia kautafiti.
Basi nikampa ile pesa. Jamaa ajafanya ajizi kaenda kufanya michakato ndani ya siku 3 akanilipa ile pesa na +10,000/=
Toka mwaka 2013 hadi leo jamaa amebadil maisha yake.
Mwaka 2015 mwezi january kanifata home kipindi iko nimekaa mtaani sina kazi nimemaliza chuo ( 2013).AKaniambia mdogo wangu kuna milion 3 kama unawazo la biashara njoo uchukue ufanye utarudisha kidokidogo.
Nikawa natafuta wazo la biashara ili nisipoteza pesa za bro.milion 3 kubwa sana nisikurupuke nitaipoteza.Mungu mkubwa ndani ya muda huu nikapata kazi.nikamwambia kaka ebu ngoja nikapambane na jasho langu.Yeye sasa ana nyumba ,nimesema nyumba ya maana usifikiria kajumba na ana biashara imara hata mimi namuogopa
KWA NINI NIMESIMULIA HILI JAMBO.
Ni hayo tu.
- Unapotaka kuanza biashara usiwaze kuwa na mtaji mkubwa ndio utafanikiwa
- Wazo la biashara ni jambo kubwa sana linakufanya uwe huru kuendesha biashara husika
- Utayari na kujitoa huleta mafanikio makubwa sana
- Tuwe wavumilivu na uaminfu ktk biashara
JF ni mahali salama kupita mitandao yote ya kijamii Tz.Mungu ibariki /wabariki JF, Uongozi wa JF na wajumbe wa JF.
Nasikia njugu mawe zinalipa kuliko maharage.Kodi shamba.
Nunua mbegu za maharage
Lima katika maeneo yanayostawi.
Baada ya siku miamoja kauze
dah kiongozi una motoKutokana na msimu uza nguo za chrismass pitisha kwa watu maeneo ya ukonga hasa za watoto ikifika mwaka mpya badilisha nenda uniform utachanganyikiwa na faida
Tafuta mwanvuli kanunue urembo Helen, Bangir n.k nenda maeneo ya sokoni weka meza uzaHabari zenu ndugu,Nipo dodoma , nina mtaji wa laki mbili (200000) nimefanya kazi ngumu hadi kuupata ikiwa ni pamoja na kubeba zege na kuchimba mitaro.
Kwa wale wajuzi wa maswala ya biashara nipeni msaada wa wazo la biashara .japo nipumzike na mimi na hizi kazi ngumu .
Na mungu awabariki
AiseeeeKutokana na msimu uza nguo za chrismass pitisha kwa watu maeneo ya ukonga hasa za watoto ikifika mwaka mpya badilisha nenda uniform utachanganyikiwa na faida