Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Mabibo ni nachoona kufanya ni kufungua biashara ya chips

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok sasa fanya hivi :
1. tafuta sehemu nzuri ya kufunya hiyo biashara kwanza usilipie wala kuanza kusema utafanya hiyo biashara ila zunguka angalia hilo eneo ulilolichagua kwa kulifanyia utafiti kama watu hapo wakiwekewa chipsi wataonyesha mwitikio.

2. angalia nani mwingine hapo jirani na yeye anafanya biashara ya chipsi na je anafanikiwa wapi na anashindwa wapi?

3.ww ukifungua hapo biashara ni nn ufanye kuboresha biashara yako zaidi ya mwenzio na kama hakuna mwingine hapo, basi ni vipi utawafanya watu waanze kuja kwako.

4. ubora wa huduma je utauweza kulingana na hayo mazingira yako.

Mwisho ufanye tathimini je ! mtaji wako utatosha ? na nguvu kazi yako ? huo sasa ndo uchambuzi yakinifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu mambo vipi

Nina mtaji wa laki tatu , ila sijui nifanye biashara gani, naomba ushahuri wenu..

Nipo dsm , Kimara hapa.


Karibuni
 
Back
Top Bottom