Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kuna kampuni moja ha kukopesha.sasa hivi hawakopeshi wanasubiri walipwe Kwanza.
Na kila siku wanafungua ofisi ila hela ya kukopesha HAWANA ZOTE ZIPO KWA RAIA
Biashara nzuri hii, ila wakopaji hawana woga yaan mtu anachukua na mnaandikishiana kbs ila changamoto muda ukifika utapigwa danadana za kila namna

Aingie akiwa na tahadhari maana kuna uwezekano wa kupoteza mtaji maana huku mtaani wakisikia unakopesha wanafanya kuambiana waje kukopa ila shida ndio kwenye malipo
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kuna kampuni moja ha kukopesha.sasa hivi hawakopeshi wanasubiri walipwe Kwanza.
Na kila siku wanafungua ofisi ila hela ya kukopesha HAWANA ZOTE ZIPO KWA RAIA
Ogopa Raia
Biashara ya kukopesha ni kama kama kamari kuunguza mtaji kitu kidogo tu
Ingawaje wanasema mfanya biashara lazima uchukue risk kama hizo
 
Wakuu Habari baada ya kuonekana kuna shida ya ajira mtaani

Nimeweza kupata kiasi cha Tsh laki Moja sasa Hapa nilikuwa naomba msaada wenu wa Mawazo Shughuli gani ninaweza kufanya maana hii hela niliyonayo ni ya mkopo wakuu natakiwa kurudisha mwezi wa 4.
Chupi za kike na vi blauzi vitakutoa haraka sana
 
Mkuu wewe huwa ni mjuzi wa Nini?
Maana KILA uzi unasema ngoja wajuzi waje!
Hata nikikwambia Profession yangu sijui kama itakusaidia kitu...

Halafu hiyo ya kusema kila uzi nitake radhi maana sio kila uzi nasema ngoja waje
 
Biashara nzuri hii, ila wakopaji hawana woga yaan mtu anachukua na mnaandikishiana kbs ila changamoto muda ukifika utapigwa danadana za kila namna

Aingie akiwa na tahadhari maana kuna uwezekano wa kupoteza mtaji maana huku mtaani wakisikia unakopesha wanafanya kuambiana waje kukopa ila shida ndio kwenye malipo
Hivi hiyo id na avatar yako vinaakisi kilichomo ndani yako?...
Najaribu kuwaza tu
 
Tatuta hata sehemu ya kukodi mtaani uweke meza uanze kupiga mpunga
Nakubaliana ushauri wako mkuu.

Naweza kuongezea njia nyingine ya kuuza matunda; achanganye matunda tofauti kwenye vifuko vidogo na kuuza sehemu yenye foleni kwa watu wanaoenda kazini asubuhi na kurudi nyumbani jioni.

Matunda yawe ya kumtosha mtu mmoja ili bei iwe rafiki kwa mfuko mmoja.

Watu wengi wanajua umuhimu wa kula matunda siku hizi na hii ni njia nzuri kuwafikia wateja badala ya wateja kuja kwake.
 
Wakuu Habari baada ya kuonekana kuna shida ya ajira mtaani

Nimeweza kupata kiasi cha Tsh laki Moja sasa Hapa nilikuwa naomba msaada wenu wa Mawazo Shughuli gani ninaweza kufanya maana hii hela niliyonayo ni ya mkopo wakuu natakiwa kurudisha mwezi wa 4.
Kwakua umesema upo dar.. Ngoja nikipe idea mbili ukishindwa basi...

Idea ya kwanza kesho wahi pale ilala boma langua suruari za buku hadi buku jero ingia mle ndani kuna mafundi cherehani kibao zimodify zen shuka pale karume ziuze kwa buku tatu tatu...

Idea ya pili nunua meza ya elfu 30 then tafuta eneo lenye mkusanyiko weka karanga utapiga hela kua mvumilivu halafu uje unipe mrejesho... Eneo huwezi kosa maranyingi wanakodisha kwa elfu mbili hadi elfu tatu kwa siku ila kam unajua kujitetea utapewa bureeeee kabisa...
Kila lakheri mkuu
 
Biashara ndogo ndogo kuna biashara ya nguo mainly ,inauzwa ilala boma na karume kwa ilala boma quality jeans za kike na kiume ni 4000 kwa mnada, kuna top na blauzi za kike na tshrt na visweta hivi huuzwa buku 2 tu......ukinunua unatembeza tu kitaa vyuoni pia utapata pesa.....

Kuna biashara ya matunda hapa unanunua vimatunda vyako unaweoa kwa aina fulani la contena dogo na sahani sahani ya matuna unauza elfu 1 tu mkuu.....

Kuna biashara ya nguo za ndani za kike kwa kufuata kariakoo (idea hii niliiona kwa dada ana id ya Pisi kali
..hizo nazo unatembeza kitaa, saloon chuo....

Kuna biashara ya kukaanga kuku na mihogo....tafuta eneo lenye shighuli zingine frames au garage karibu au chuo anza kukaanga mihogo na kuku wa kisasa unatoa vioande vingi....unakaanga vizuri na chachandu baada ya mda utapata faida maana muhogo 1 200 hadi 100 alafu kipande cha kuku 500 tu shingo, kichwa, miguu utumbo 300 au utakavyoona inafaa maeneo jama kidari upaja weoa 1000 nk......

Biashara ya kahawa, karanga na kashata zile pia ipo vizuri......biashara ya ice cream pia ipo vizuri inategemea kama una fridge au bei mtakayokubaliana na mwenye fridge....

cha msingi uwe smart, uwe mcheshi, uwe na story story nzuri za kufanya mteja arudi tena.....ili mradi mteja awe comfortable akija kwako
 
Mkuu wewe huwa ni mjuzi wa Nini?
Maana KILA uzi unasema ngoja wajuzi waje!
😀😀😀Ila Mimi namkubali Sana jamaa , mwamba yupo humble Sana , anachofahamu anachangia asichokijua bas anakarbisaha wanaojua wasaidie , ni mtu wa watu Sana humu JF , sijawah ona comment yake hata ya kutukana , kimsingi ni Kati ya watu naowa-respect Sana aisee Joseverest
 
Mkuu Nenda Sokoni Kisutu kuna Korosho nzuri safi zilizokaangwa(Rosted and Salt) zinauzwa Elfu 9 hadi 10 Kwa Robo kilo nunua vifuko special vile vidogo vinauzwa elfu Tano kwa pcs 50 yaani kimoja ni Mia Korosho unaweza nunua robo kilo unajaza kwenye kifuko kwa kutumia Mzani ile midogo digital gram 20 ukimaliza kujaza vifuko vitatoka vifuko 25 kila kifuko kilichojaa Korosho utakiuza kwa bei ya Shs 1,000/= so ukifanikiwa kuuza vyote mauzo yatakuwa elfu 25,000/= gharama za Matumizi ya kuandaa bidhaa itakuwa 5000/=vifuko,Korosho 9,000/= Jumla 14,000/= Faida itakuwa 11,000/= Hapo unaweza tumia akili zako kama umezaliwa nazo ukaenda kwenye maduka ukawauzia kwa bei ya jumla kifuko komoja ukawauzia mia 600 au 700 upate faida ya 400 au mia tatu kwa kila kifuko au unaweza omba mwenye duka akuuzie faida mgawane n.k but unatizama mauzo yakiwa fresh unaongeza mzunguko wa kutafuta masoko ila hakikisha Korosho zile Tamu na Safi ikiwezekana unachambua unaondosha zile mbaya ukiendlea unaweka na namba yako ya simu kwenye vifuko maisha yataenda... ukiwa na mkono wa Biashara hiyo pesa unaweza rudisha mkopo ndani ya siku kadhaa tu. Nimekupa Mtaji mdogo kabisa wa kuanzia ambapo ni robo ya ulichonacho.

kama Umependa Gonga Like. Utashukuru ukifanikiwa
 
Kopesha watu hapo hapo ulipo weka na riba ya elf mbili kila baada ya siku saba.
10,000×10+2000×10=120,000 kwa siku saba. ila jipange mkuu.
Hiyo biashara si mshauri hakuna biashara yenye high risk kama kukopesha watu, kwanza chance ya kuipata hiyo pesa inaweza kukuchukua muda sana au usipate kabisa
 
Back
Top Bottom