Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Naomba ushauri na uzoefu wa biashara ya kukata balo za viatu za mtumba na kuzungusha minadani.kwa yeyote anaefanya hata kama itakua wazo lingine tofauti na viatu karibu!

Note: nilipo sio mjini kivile ila kun minada
 
Naomba ushauri na uzoefu wa biashara ya kukata balo za viatu za mtumba na kuzungusha minadani.kwa yeyote anaefanya hata kama itakua wazo lingine tofauti na viatu karibu!

Note: nilipo sio mjini kivile ila kun minada
Niliwaza nifanye hiyo biashara but nilibadilisha mawazo saivi nna ishu nyingine
 
Kwa wadau Wanaohitaji kuingia kwenye biashara hii nzuri nawakaribisha Sana ,hasa wadau wa mikoan miez hii biashara inahitajika Sana Ndo miez ya kuvaa Unaweza ukabuni kusambaza kwenye masoko,magulio, Stand,kuwasambazia kwenye maduka,kuuza kwenye vijiji huko fashion mbalimbali zinazitoka wanapenda Sana so wenye interesting tutazidi kupeana Mbinu Machimbo Mimi ntarahishisha Hilo
Dhumuni Ni Kukurahisishia Mteja Wetu Machimbo Kukuletea Bidhaa Bora Original Kwa Bei Nzuri , Fashion Mpya,Mpya Zinazotrend, dizain Tofaut Tofauti, Kama;
*YEBO YEBO
*SLIPPERS, SANDALS,
*Shoes & Clothes
*Tunatuma Mikoa Yote Kwa Oda
*Tunauza Kwa Rejareja na Jumla Kwa wafanyabiashara wa Dar na mikoani Tunatuma Kwa Oda
*Bei zinaanziaTsh 3000,5000,8000,10000,15000+
*Piga no 0716898393 , Whatsapp 0714994833
*Links Whatsapp group Uone update za dazain tofauti MHINA SUPER Discount SHOES SANDALS, SLIPPERS,YEBO YEBO, CLOTHES
 
Wakuu,

Kutokana na wadau kadhaa kuja na mijadala anuai inayoonyesha kuwa wanayo mitaji yenye kuanzia kiasi cha TZS 100,000/= hadi TZS 999,999/=, tumeona ni vema tukawa na mjadala mmoja endelevu ambao utatoa mawazo mbalimbali ya jinsi ya kutoka kimaisha ukiwa na mtaji huo.

Aidha, tunashauri usome maoni mbalimbali ya wadau kuweza kupata kujua wengine wametokaje kwa viwango hivi na unaweza kufikiria namna unayoona inafaa kwako. Tumejitahidi kupangilia posts humu kukurahisishia usomaji kwa ufanisi wako.

Asante

View attachment 1482167

Biashara za kuanzia 100,000 - 200,000


-----

----

----

----

----

----

----



Biashara za mtaji wa kuanzia 300,000-500,000



-----

----

----



Biashara za mtaji wa kuanzia 600,000-900,000



----
Mimi Nina laki 9 je naweza fanya biashara ya urembo kama vile kuuza rasta ,hereni ,cheni ...?
Nipo dodoma lakn cha kusikitisha cjui chochote kuhusu hii biashara ya urembo, cjui mahali pa kufungasha mzigo wala siri za hii biashara ila ndio biashara ninayoipenda sana.
Msaada wenu wakuu
 
Mimi Nina laki 9 je naweza fanya biashara ya urembo kama vile kuuza rasta ,hereni ,cheni ...?
Nipo dodoma lakn cha kusikitisha cjui chochote kuhusu hii biashara ya urembo, cjui mahali pa kufungasha mzigo wala siri za hii biashara ila ndio biashara ninayoipenda sana.
Msaada wenu wakuu

Nakushauri ustick kwenye cheni na hereni
900k ni hela nyingi sana

Hereni mjini zinauzwa dosen kwa 7,000
Unaweka na sabuni Za Bei rahisi
Madodoki
Na vindala
 
nahitahitaji kuanzisha biashara ya juis za matunda,naomba msaada wa mchanganuo na location nzuri
 
nahitahitaji kuanzisha biashara ya juis za matunda,naomba msaada wa mchanganuo na location nzuri
Hii ni Moja ya biashara nzuri mno
.
Unaweza Kuanza kwa kutembeza mitaani au Kwenye maofisi, anza na dumu 2 zenye ladha tofauti, kuna mtu atataka umchanganyie, mwengine atapenda moja zaidi.
.
Pia jitahidi iwe na ubaridi vizuri maana ndio inayopendwa zaidi. .
.
Pia hakikisha usiuze juice iliyolala ili kuepusha mtu kuumwa tumbo.

MAMBO YA KUZINGATIA.

USAFI
Usafi binafsi kwako muuzaji, usafi wa vyombo na mahali unapoandalia juice.
.
SOKO
Soko ni Kubwa, mtaani, masokoni, kwenye maofisi, kwenye Migahawa na shughuli mbalimbali.

BEI
Tengeneza za kuanzia Tsh 500_5000 na zaidi ukijenga jina

MAHITAJI
Blender heavy duty ni zuri zaidi na litadumu, package nzuri, mirija, fridge, maji masafi, chujio, vyombo vinginevyo

TENGENEZA JUICE PENDWA
Juice pendwa ni Maembe, maparachichi, Passion, Ukwaju, Ubuyu, Rosella, juice ya Tende, juice pendwa ya miwa na Smoothies

CONSISTENCY (Usiache)
Fanya kwa muendelezo Mpaka ujenge jina.
.
PANUA SOKO, FANYA KWA UKUBWA.
Usiogope kuomba tenda kwenye Migahawa ya kuwa muuzaji wa juice. Migahawa mingi hawatengenezi juice, wewe nenda waombe kuuza juice kwa wateja wanaonujua chakula.
.
TENGENEZA JUICE KWA ODA.
.
Kwenye sherehe zote omba nafasi ya kutengeneza juice, iwe ni kipaimara au harusi omba nafasi. Kama sherehe ni kubwa omba wakulipe Advance kwanza.
.
Hii ni biashara nzuri unayoweza kuanza sasa na kuanza na kuanza kutengeneza faida.
.
Unatamani kujifunza kuhusu hii biashara kiundani? Kuna vitabu vya jinsi ya kutengeneza aina mbalimbali za juice, mbinu, mauzo na masoko.

........
Mawazo mbalimbali ya biashara pitia page yangu ya instagram ya @kelvinkibenje utashukuru
 
Back
Top Bottom