Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Ninge anza na kufuga kuku wa nyama 100 na baada ya wk mbili nigeingiza batch ya pili tena kuku 100, na balance ya hio laki 5 naitumia kwa, chakula, matibabu
 
nige anza na kufuga kuku wa nyama 100 na baada ya wk mbili nigeingiza batch ya pili tena kuku 100, na balance ya hio laki 5 naitumia kwa, chakula, matibabu

Wazo zuri endapo tayari ana mabanda. Kifaranga cha nyama roughly 1,600 tzs. 100 ni 160,000. Kuna vyombo vya chakula na maji, madawa nk
 
Niwazo zur lkn kuna garama kama kuanda banda vyombo vya kulishia vtmn na dawa pia so unafkir mtaj wake utajtosheleza???
 
Tatizo waa sio mtaji, tatizo ni je una spirit ya ujasiriamali? Tatizo kubwa huwa sio mtaji ila mtaji unatumika kama ngao,
 
Ndugu wanaJF hasa vijana wenzungu tulio mtaani.

Nahitaji mtu aniandikie kwa umahiri kabisa business plan ukipewa mtaji wa shilingi laki tatu utafanya biashara gani? ukimaanisha mtaji wako ni shilingi laki tatu, bainisha mapato yako yatakua yapi, matumizi na faida yako kwa muda wa mwaka mmoja.

Mshindi nitampa hizo laki tatu kwa maandishi bila rehani yoyote na baada ya mwaka arejeshe pesa zangu hizo hizo laki tatu. Shindano hili ni la kweli halina mezengwe yoyote.

Tuma business plan yako sasa.
 
Tanzania sijui kwa nini hakuna watu wa kununua business ideas na kuingia ubia na hao wenye hizo ideas.Kuna watu wana hela hawajui wafanye nazo nini Na kuna watu wana mawazo mazuri mno ya biashara na uwezo wa kuzifanya biashara ila hela hawana.

Njia nzuri ni kuingia ubia na mwenye wazo na kuwa partner naye na kufanya naye biashara.Baadhi ya watanzania wana tabia ya kuchukua mawazo ya watu na kutimuka kwenda kuyafanyia kazi.Bahati mbaya huyo aliyetimka nalo wazo utakuta mara ingine huko mbele anakwama sababu lile wazo lilitakiwa mwenyewe mwanzishaji awepo anayejua ukifika kona fulani ukate lori kona vipi.

Wengine hasa wanafunzi vihiyo wanatabia ya kuomba waandikiwe business plan kwa ajili ya masomo vyuoni kwa madai kuwa ukiandika inayokubalika watakulipa utaandika utaambiwa imekataliwa kumbe mwongo anataka asilipe wakati kafanikwa.Sidhani uko katika kundi hilo na sidhani ni mmoja wa wale watafutao wazo wakafanye nalo biashara wenyewe!

Nashukuru kwa moyo wako wa kutaka kusaidia watanzania lakini njia bora ni kuingia nao ubia.Ukimpa hela tu utakuwa hujamsaidia sana aweza enda honga kimada zote.Kumsaidia msimamie afanye na mwambie awe akilipa hiyo hela kila mwezi kidogo kidogo.

Wafanyabiashara wa kabila la wakinga ni wazuri sana wa kuanza nao biashara hizo za mitaji ya laki tatu na wanauwezo wa kuifanya ikue haraka taabu hawapendi mikopo na hawapendi ubia na wasiokuwa wakinga wenzao na wengi hawajasoma hivyo kuandika hizo business plan hawawezi ila kwa biashara za hiyo laki tatu wanaweza sana tena sana tena kwao hiyo yaweza kuwa nyingi mno.

Anyway kama pengine unahitaji tu business plan kwa sababu uzijuazo kuna waandishi wa business plan kibao mjini wa kulipia waone wakuandikie.Ukishawalipa wakikuandikia huwadai hawakudai biashara imefungwa uko huru kutumia hiyo business plan upendavyo.
 
Ndugu wanaJF hasa vijana wenzungu tulio mtaani.

Nahitaji mtu aniandikie kwa umahiri kabisa business plan ukipewa mtaji wa shilingi laki tatu utafanya biashara gani? ukimaanisha mtaji wako ni shilingi laki tatu, bainisha mapato yako yatakua yapi, matumizi na faida yako kwa muda wa mwaka mmoja.

Mshindi nitampa hizo laki tatu kwa maandishi bila rehani yoyote na baada ya mwaka arejeshe pesa zangu hizo hizo laki tatu. Shindano hili ni la kweli halina mezengwe yoyote.

Tuma business plan yako sasa.

BUSSINESS PLAN

JINA: MAKUA
MAHALI: DAR ES SALAAM

JINA LA BIASHARA:

MMILIKI: MAKUA

AINA YA BIASHARA: MITO & PILLO SALES

MAHALI ILIPO BIASHARA: MAGOMENI-MWEMBECHAI

MTAJI: TSH 300000

MCHANGANUO WA BIASHARA
1: Kitambaa cha kushonea mito na pillo mita 9 @10,000*9= 90,000/=

2: shiti za nusu inch 5 3500*5=17500/=

3: krashi/pamba kilo 35 2000*35=70000/=

4: uzi wa kushonea namba 3p @1500*2 =3,000

5: zipu mita 150 @400*15=6000

6: gund tsh. 3500

7: fundi mto mmoja tsh. 1500 *20=30000/=

Jumla 300,000/=

Nitapata mito 20 size 20 na pillo (mito midogo) 10

Mto mmoja tsh. 15,000*20=300,000/=

Pillo tsh. 7500*10=75,000

Kila baada ya wiki mbili natarajia kumaliza mito yote hivya nitapata tsh. 375,000
Faida itakuwa 75,000 kwa miezi miwila ambayo sawa na tsh. 150,000 kwa mwezi
Sawa na tsh. 1,800,000 kwa mwaka.

Nimejaribu kufanya hivyo.
 
Last edited by a moderator:
BUSSINESS PLAN

JINA: MAKUA
MAHALI: DAR ES SALAAM

JINA LA BIASHARA:

MMILIKI: MAKUA

AINA YA BIASHARA: MITO & PILLO SALES

MAHALI ILIPO BIASHARA: MAGOMENI-MWEMBECHAI

MTAJI: TSH 300000

MCHANGANUO WA BIASHARA
1: Kitambaa cha kushonea mito na pillo mita 9 @10,000*9= 90,000/=

2: shiti za nusu inch 5 @3500*5=17500/=

3: krashi/pamba kilo 35 2000*35=70000/=

4: uzi wa kushonea namba 3p @1500*2 =3,000

5: zipu mita 150 @400*15=6000

6: gund tsh. 3500

7: fundi mto mmoja tsh. 1500 *20=30000/=

Jumla 300,000/=

Nitapata mito 20 size 20 na pillo (mito midogo) 10

Mto mmoja tsh. 15,000*20=300,000/=

Pillo tsh. 7500*10=75,000

Kila baada ya wiki mbili natarajia kumaliza mito yote hivya nitapata tsh. 375,000
Faida itakuwa 75,000 kwa miezi miwila ambayo sawa na tsh. 150,000 kwa mwezi
Sawa na tsh. 1,800,000 kwa mwaka.

Nimejaribu kufanya hivyo.

Kuna watu wanawaza pesa muda wote, safi sana aisee. I like this.
 
Jaman naombeni msaada ni biashara gani nifanye na wapi inalipa
 
Swali lako ni la kijumla mno. Hujaeleza ujuzi/uzoefu wako, mtaji wako, mazingira yako - sio rahisi kukupa mawazo. Jieleze zaidi.
 
Karibu tufanye forever living business kwa kuanzia mtaji wa laki 3 na sabini na tano
 
Ni nertwork business inayolipa sana kama ua ready unaweza kunipm au kunicheki kwa maelezo zaidi 0717115421
 
biashara zetu hapa ni
bodaboda
Mpesa/Tigo Pesa
Ufugaji Wa Kuku
chagua mwenyewe hapo ipi inafaa
 
Fanya biashara ya kununua meli Japan uje kuuza huku
 
Salamu wakuu!
Mimi ni mwanafunzi wa jinsia ya kiume katika chuo kimojawapo Tanzania.
Nafanya digrii ya Biashara.

Natamani kutumia muda wangu wa ziada kujitafutia kipato kwa kujishughulisha na biashara.

Kwa kuanzia,nina sh. Laki na nusu.
Naomba mwenye ushauri wa biashara gani naweza kufanya anishauri.
Pamoja sana.
 
Back
Top Bottom