Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Life is too short and sometimes is not fair ,tafuta kimwana for one nite only asubuhi utakuwa mtu mwingine ,laki moja inaumiza kichwa Kama mtaji
 
Jawilat wewe upo mkoa gani? na je ukiniuzia kwa bei hiyo na mimi ninauza kwa bei gani?
Ngoja nikuuzie shuka kwa jumla,ni za cotton kama upo maeneo ya mjini,upitishe katika maofisi,
 
Mie nipo singida,ila mzigo upo dar,huku nauza 35-30000
25000 nauza kwa mtu anaechukua nyingi.
Jawilat wewe upo mkoa gani? na je ukiniuzia kwa bei hiyo na mimi ninauza kwa bei gani?
 
mkuu anza biashara ya kununua na kuuza kuku wa kienyeji kutoka mikoani kuja mijini at a reasonable price..
 
Mie nipo singida,ila mzigo upo dar,huku nauza 35-30000 25000 nauza kwa mtu anaechukua nyingi.
nyingi zinaanzia ngapi. dada sema ni aina gani ya shuka na zinaquality gani, ( weka picha ndugu)
 
nyingi ni kwanzia 6,nashindwa kuupload picha,material ni cotton.
 
Hata mie umenivutia mkuu Jawilat maana hua ninafanya hiyo biashara ya mashuka ila yenyewe ni mtumba,naona kama yako hiyo ni nzuri zaidi,nakupm ili kujua njinsi ya kukupata
 
alivyokushauri ynaa siyo mbaya ni nzuri, ila ungekuwa dar ningekushauri kama ungekuwa na mtu anayeuza vyombo, siku hizi kuna watu wengi sana wanauza uza vyombo barabarani, ungempa hiyo hela kama kuongezea mtaji(ila uwe unamfahamu na awe mwaminifu) yeye atakuwa anakupa kila siku 5000 ambayo kwa mwezi kama sijakosea utakuwa na 150000,utamuongezea mtaji kidogo ili hata hela yako ya kupata inaongezeka kufikia 10000, mbayo kwa mwezi wa pili utapata 300000 waweza endelea kujipanga. mi niliwashauri wadada wangu wakazi kufanya hivyo ili kuweza kujiwekea akiba endapo atataka kuacha kazi apate kitu cha kwenda kuanzia mtaani nje ya mshahara wake. nawanafanyiwa vizuri sana na hao wakaka(nadhani hii kitu watu hawaifahamu)[/QUOT ni kitu kizuru je security ya huyo unaempa pesa itakuwa ni nini thats momey bro!

ni vp siku biashara ikiwa ngumu?je hiyo buku 5 anakupa au itategemea na mauzo?
 
Kwa haraka haraka fungua saloon ya kiume kwan utapata mashine moja na kioo kimoja...
 
kiko wapi hicho kijiji mkuu, ni songea hapa hapa, mbinga, au Namtumbo.

Namtumbo,ukifika pale junction ya kwenda namabengo unashuka unachukua boda hadi mdwema.Nauli hadi pale ni buku jero na kwenda huko ni buku 2.
 
Namtumbo,ukifika pale junction ya kwenda namabengo unashuka unachukua boda hadi mdwema.Nauli hadi pale ni buku jero na kwenda huko ni buku 2.

okay bro nimekupata kumbe sio mbali naweza kwenda na kurudi.vip hao kuku wanaweza niuzia kwa bei gani.
 
Back
Top Bottom