Kwa muda mfupi sana kiongozi wa Tanzania alipata maadui wengi sana

China na Tanzania kisera ni ardhi na mbingu usifananishe china na vitu vya kijinga kabisa mkuu
Wachina baada ya kuona population yao inavoongezeka kwa kasi, wakaja na sera ya kuzaa mtoto mmoja kwa kila wanandoa, lakini wakwetu sisi karuhusu wananchi wazaliane kwa kufyatua watoto kama matofali
 
Adakadabra nyingi tu ,tusiwe biased, tusiongee positive tuu as if hakuna negatives, huo ubadhirifu aliobaini CAG unatoka wapi kama wahusika wote wapo magerezani?
Yaani watakatifu ndio wamegeuka kuwa wabadhirifu?
Tuongee kwa kiasi wandugu.
 
Hata yeye hakutaka umpende...
Tuliomwelewa tulimpenda....

RIP mwamba
Motion ya huyo hayati wenu haikua na uelekeo wa kutupeleka uchina,ngoma ilikuwa inaelekea ZIMBABWE acheni kufananisha uharo na futari.
NIPO WAZI KABISA SIKUMPENDA JAMAA YENU HAKUWA KIONGOZI RAFIKI WA WATANZANIA.
 
Kabla huyu mwamba wenu hajaingia madarakani nilikuwa nikienda kumsalimia bibi kule nyanungu kwa kupita mbugani basi ilikuwa nalipa 30000 mpaka Tarime.
Alipoingia tu mwamba garama ikapanda ikafika 50000 eti wanaopita huko wote walipishwe kama watalii Wa ndani.
,utadhani anawakatia majani hao wanyama.kwa hili Mimi nkageuka kuwa adui wake.
 
JPM was kind of a leader.. Alikosea na Kuharibu reputation yake..
..Alipoendekeza ukabila.
..kuminya demokrasia
..kutotaka kosolewa
. ..Kuwachukia makabila ya kaskazini.
. ...Kukusanya kodi haramu kaskazini nakupeleka maendeleo chato wakati hakuna kodi inayokusanywa huko.
. ...Kuamuru critics wauawe.
. ....Kuwachukia wenye pesa hata Kama wamepata kihalali.
. ...Kuamini kwamba ninadamu wote wanatakiwa kuwa sawa kiuchumi wakati wamumbwa kwa uwezo tofauti wa kufikiri, bidii ya kazi, vipaumbele katika matumizi ya pesa wanazopata wakati wapo wanaospend vipato vyao na wengine wana invest nakuweka akiba ya baadaye.
. ...Kutokuwaamini watumishi wote wa serikali kwa Ku weka TISS kila sehemu ya kazi hata kama hawana uelewa wa kazi zinazofanyika sehemu husika.
. ...Kuvunja kifungu cha katiba kinachompa kila RAIA uhuru wa kwenda kokote anakotaka lli mradi havunji sheria. Hakuna kusafiri nje ya nchi bila kibali chake.
. ....Na mengine meeengi orodha ni ndefu.
 
Kila kitu tu kilipanda bei sio ilo tu wakati huo akuna ongezeko la mishahara, makampuni yanapunguza wafanyakazi, serikali Ajira hakuna.....uku serikali ikitangaza viwanda kuongezeka sjui maelfu mangapi nchini ndani ya miaka 5 😂😂😂😂
 
Kwa maelezo ya kipuuzi uliyotoa siwezi kusoma upuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…