Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Maalim Seif siyo Wanachama tena

Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Maalim Seif siyo Wanachama tena

CCM na tume yake hupenda Uchaguzi uwe na sintofahamu kama kipindi kila Matokeo ya Tunduru kuletwa Tunduma
 
Kuna utofauti kati ya NGUVU wanachama na mwanachama.

WANACHAMA WALILIJADILI HILI NA NDIO WENYE CHAMA.
 
DU wapinzani watu wa ajabu sana, wenyewe wanajisikia raha sana wakivunja katiba zao kwa maslai yao binafsi alafu bila aibu utasikia tunataka katiba mpya, upinzani Tanzania utakaa sana.

Mara utasikia Rais hafuati katiba mara Rais anavunja katiba. Hongera mleta mada kwa kudadavua na kutuchimbia gimbi tutalipika na kulila.
 
Hili linashangaza! Siamini hii ndio katiba ya ACT (toleo la mwisho lililohaririwa). Angalia kipengele cha tano kina makosa mengi sana ya kiuandishi. Pia huo msitari wa mwisho uliokatwa hapo inaonekana una utaratibu maalumu wa kufukuza wanachama kupitia vikao maalumu vya chama! Hebu wekeni vipengele vyote.
 
Msajili na tume ya Uchaguzi kesho malizeni kila kitu, ondoeni ugombea hao waliojivua uanachama ACT wazalendo Zitto na Maalim Seif.
 
Akili zako ndio zinazokutuma labda mmtumie Msajili wenu tuu, ila akina Zitto na Maalimu walifuata sheria maana ilipitishwa na vikao halali vya chama
 
Katiba ya ACT wazalendo ibara ya 14 inamtaja mwanachama wa chama hicho kama alivyo Zitto na Shariff kwa mtu yeyote atakaye mpigia kampeni mwanachama wa chama kingine kama alivyofanya Zitto na Shariff watakuwa wamejifukuza uanachama wa chama hicho.

Kwa hili Zitto na sharifu hamna cha kuomba radhi mjiuzuru mapema sana

USSR

IMG-20201020-WA0008.jpg
 
Mimi kila siku nauliza hawa wanaojiita wapinzani huwa wanapinga nini? Maana upande A wakifanya kosa hupiga kelele ila upande B nao wakifanya kosa hilohilo wanatetea.
 
Lakini Zitto na Seif wamesema wanamuunga mkono Lissu na si Chadema! Hiko kipengele kimetaja chama ..
Mkuu rejea tena kipengele namba nne kwenye kiambatanisho kilicholetwa na mleta mada. Imeelezwa hata kuunga mkono mgombea wa chama kingine wakati ACT nao wameweka mgombea ni kufutwa chamani!!! Aisee Zitto kamzamisha Seif hivi hivi!!!
 
Nimebahatika kuiona katiba ya ACT toleo la 2015 mahali fulani. Kipengele cha sita kinasema:
6. Uamuzi wa kumfukuza mwanachama yeyote hautakuwa na nguvu hadi pale uamuzi huo utakapokuwa umewasilishwa kwa maandishi.
Nani na kikao gani cha kutoa uamuzi wa kuwafukuza uanachama Zitto au Seif ndani ya ACT kwa maandishi?

Pia kipengele hicho cha kufukuzwa uanachama kipo mahsusi kwa 'mwanachama' na sio uamuzi wa 'chama' kama huo? Pia inaonekana kuna kanuni za kutekeleza haya maswala zilizotungwa na halmashauri kuu ya ACT! (wanajua kanuni zao?).

Inaonekana ni zoezi gumu kutekelezeka!
 
Umeambiwa swala la ushirikiano lilijadiliwa katika vikao vya chama na si kuwa mwanachama mmoja kajiamulia mwenyewe kumuunga mgombea wa chama kingine. Kwa hiyo hili swala lilikuwa maalum na kifungu hicho hakija kiukwa.
Ndilo jibu lenyewe.
Umesema vizuri.
 
Ndugu zangu,

Katiba ya ACT Wazalendo inapinga mwanachama kumuunga mkono mgombea asiye mwanachama wa ACT.

Fuatilia mwenyewe hapa chini,Bernard Membe akitumia vema turufu anaweza kuwavua uanachama hawa "wavamizi" ndani ya ACT.View attachment 1606498

Kwa kweli mna hangaika. Mtapitia hata katiba za ndoa za watu binafsi kutafuta mnapoweza kutumia ili Maalim asichukue nchi. Wizi mliomfanyia miaka yote akiwavumilia bado tu mnataka kumfanyia hata akiwa past 77?

Aibu kwenu!

Ya Lipumba Mutungi hayakutosha sasa mna brew mapya? Au ndiyo lile nao la dak ya 89?

Fahamuni 27 na 28 ziko karibu na Fatou Bensouda tayari ana taarifa zenu zote.
 
Back
Top Bottom