Pre GE2025 Kwa Mujibu wa Tundu Lissu, Majimbo Mapya hutengezwa kutoa fursa kwa watu fulani fulani nao wapate majimbo. Kama ni kweli basi tuna safari ndefu

Pre GE2025 Kwa Mujibu wa Tundu Lissu, Majimbo Mapya hutengezwa kutoa fursa kwa watu fulani fulani nao wapate majimbo. Kama ni kweli basi tuna safari ndefu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tuko live kwenye mkutano wa Viongozi wa Chadema na Jukwaa la Wahiriri wa habari.

Mambo yanayozungumzwa humo ni mazito sana.

Tundu Lissu anasema kuna hali isiyo na usawa ktk kugawa majimbo sehemu mbali mbali nchini.

Anatoa mifano kuwa Dar yenye wapiga kura zaidi ya milioni 3 ina majimbo Machache kuliko Njombe yemye wapiga kura wasiozidi laki sita.

Na baadhi ya mikoa imepewa majimbo mapya. Na anadai kuwa majimbo mengine ni matumizi mabaya ya fedha za kuendeshea lakini hayahitajiki ispokuwa yanawekwa ili kutoa fursa kwa watu fulani fulani.

Hii haipendezi kabisa ikiwa Watanzania tunalipa kodi kwa lengo wa kuendeaha shughuli za seeikali na maendeleo lakini zinaweza kuishia kuhudumia watu wachache. Hili serikali iliagalie upya.

Bonne jourrnée
Ifahamike wazi kwa waTanzania wote, kwamba majimbo ya uchaguzi nchini yataendelea kugawanywa kadiri ya mahitaji ya wananchi na kwa kadri inavyoonekana inafaa,

huo ni uamuzi wa wananchi,
na serikali sikivu ya CCM haitasita kutekeleza mapendekezo ya wananchi na hatimae kupata uwakilishi wa kutosha kwenye vyombo vya maamuzi na huduma za kijamii.

makelele na mdomo wa uropokaji wa vibaka na matapeli wa kisiasa haitazui mabadiliko hayo kufanyika 🐒
 
Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa kuna ulazima wa majimbo mapya kuongezwa. Naona ni kujiongezea mzigo wa gharama kama nchi. Hoja ya kupata wawakilishi wa wananchi ni nyepesi mno kwenye huu ulimwengu wa digitali. Kama ni kero za wananchi siku hizi zinaibuliwa na wananchi wenyewe na kuonekana nchi nzima kupitia mitandao. Ninaweza nikawa Mbamba bay nikajua kule Karagwe kuna sehemu hakuna daraja mtaani.

Pia kwa kigezo cha kujua tu kusoma na kuandika kama sifa za kuwa mbunge zinafanya bunge liwe sehemu tu ya kupitisha miswada ya sheria na sio kutunga. Wabunge wanaoweza hata kukosoa miswada wanayopelekewa bungeni ni wachache mno. Si huwa mnaona bungeni utakuta muswada wa sheria ya kuhusu michezo mbunge anasimama na kudai jimboni kwake kunatakiwa daraja..
 
Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa kuna ulazima wa majimbo mapya kuongezwa. Naona ni kujiongezea mzigo wa gharama kama nchi. Hoja ya kupata wawakilishi wa wananchi ni nyepesi mno kwenye huu ulimwengu wa digitali. Kama ni kero za wananchi siku hizi zinaibuliwa na wananchi wenyewe na kuonekana nchi nzima kupitia mitandao. Ninaweza nikawa Mbamba bay nikajua kule Karagwe kuna sehemu hakuna daraja mtaani
Umeongea pointi kubwa sana Mamasamia2025.

Kunaonekana kuna ulaji watu wanapeana. Wanafanya vitu ambavyo sio lazima na havina tija kwa wananchi.
 
Mikoa, wilaya mpya huzaliwa,kibamba limekua jimbo toka ubungo,hakuna tatizo hapo
Sio mbaya kigawa majimbo kwa kufata taratibu sahihi zilizowekwa na wahusika ila hili la kugawa majimbo ili fulani asikose ubunge ndio inaoleta shida.
 
Umeongea pointi kubwa sana Mamasamia2025.

Kunaonekana kuna ulaji watu wanapeana. Wanafanya vitu ambavyo sio lazima na havina tija kwa wananchi.
Mimi ni mtu mwenye akili nyingi sana. Kuwepo hapa JF najiona kama mamba kwenye kidimbwi yaani sienei. Spidi yangu ya Ferrari halafu nyie wenzangu mpo na baiskeli za miti
 
Bado mnamsilikiliza mropokaji?
Nashangaa, yako makimbo makubwa sana ki size bila kujali idadi ya watu sababu wawe watu 500 au alfu 10 mahitaji ni yaleyale. Dar ina watu wengi lakini eneo ni dogo mbunge anaweza kutemebea masaa tu kamaliza.
 
Nashangaa, yako makimbo makubwa sana ki size bila kujali idadi ya watu sababu wawe watu 500 au alfu 10 mahitaji ni yaleyale. Dar ina watu wengi lakini eneo ni dogo mbunge anaweza kutemebea masaa tu kamaliza.
Hayo madogo yenyewe wanayamaliza?
 
Back
Top Bottom