Maana nachoona hapa ni upiganiwaji wa kuchukua Dola na si kwa maslahi mapana ya Taifa.
CHADEMA anaombea kuwepo na katiba mpya huku akiamini ndo itakuwa rahisi kwa yeye kuchukua nchi, CCM naye anahofia katiba mpya akihisi ndo itakuwa upenyo wa yeye kupoteza madaraka.
Ila ukifatialia kwa ndani utagundua hii vita ya katiba ni vita ya wanasiasa kuhombania kupata madaraka mwananchi anatumika kama kiunganishi tu kufika nchi ya ahadi.
Kama kuna mtu anaamini uwepo wa katiba mpya ndo utaleta mabadiliko chanya kwa taifa hili anajidanganya maana katiba mpya inaweza kuwepo na viongozi wakashindwa kuiheshimu wakaendelea kuikanyaga na hakuna kitakochotokea.
Mm ningeona mikutano hii ya katiba mpya inafaa endapo mijadala yake ingefokasi zaidi katika maendeleo yatakayotokana na katiba na si kwa sababu ya kuchukua dola.