Kwa Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda nani ananibishia kuwa EAC haiendi kufa na Wazungu kufurahia?

Kwa Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda nani ananibishia kuwa EAC haiendi kufa na Wazungu kufurahia?

Ndio muungano ndio nguvu yenyewe kuanzia kiuchumi na kijamii, ndio maana EAC inajitanua kila leo Congo iko EA , sudan ndani, somalia ndani baadae tutaihitaji ethiopia, eritria na djbout hapo tutabaki tunalilia kanda sasa ziungane SADC, EAC , COMESA, ECOWAS na kadhalika zije pamoja tuingie ndani ya AU iliyo kamili na kuondoa vikwazo kwa watu wa Africa lakini wavurugaji kama kagame wanatakiwa kuonywa sana maana wanatamaa za kupita kiasi
 
Na haya maugomvi yenu ya kijinga jinga mnawasingizia wazungu??
Hamna akili.
Tayari Tanzania, Burundi na Nusu ya Wakenya wanaisapoti Congo DR huku pia Uganda na Nusu ya Wakenya wakiisapoti Rwanda.

Wazungu ambao Siku zote hawataki Kuiona Jumuiya hii ya Afrika Mashariki ikistawi wamefanikiwa Kutugombanisha na kwa Uzuzu wa Wanaogombanishwa wamekubali Kuingia katika huu Mtego wa Kimkakati.

Hivi kwa Miradi mingi ya Kimaendeleo na Kimkakati Iiliyoko katika Jumuiya hii ya EAC mnadhani Congo DR na Rwanda (Wanachama wa EAC) zikiingia Vitani hawa Marafiki zao wakubwa Tanzania hatomsaidia Congo DR au Uganda haitomsaidia Rwanda?

Mnaacha kuwa Neutral katika huu Mzozo sasa Tanzania imeamua kuchukua upande kwa Kuisaidia Kisiri Congo DR kwa mategemeo ya kupata Tenda na Fursa nyingi za Kibiashara na hata Kumegewa kidogo Madini ya Congo DR Ili yawasaidie.

Na Uganda nayo vile vile (japo Kisiri) imeamua kuwasaidia Rwanda kwa ahadi ya Kufaidika na Madini ambayo kwa 60% yako upande wa Jirani na Taifa la Rwanda na chini ya Udhibiti mzuri wa Jeshi la Rwanda.

Saaa ni rasmi kuwa Vita ya Panzi huwa ni Furaha kwa Kunguru hivyo basi Mzozo huu wa Congo DR na Rwanda na kwa nchi za Tanzania na Uganda nao kuchukua upande wa Kuzisaidia ni Ushindi mkubwa kwa Wazungu ambao wametumia Akili Kubwa Kutugombanisha ili Jumuiya ya EAC isifanikiwe na waendelee Kutugawa ili tuendelee Kuwategemea huku Wao Wakitunyonya (hasa katika Rasilimali zetu) kutokana na Upan'gang'a (Upumbavu) tulionao.

Tulianza na Free Trade, kisha Customs Union, tupo njiani kwenda katika Monetary Union kisha tumalize na Political Federation ili EAC ikamilike kwa 100% ila kwa huu Upuuzi uliochanganyika na Unafiki wetu na Chuki zetu sioni Ukamilifu huu wa Kimalengo kwenda Kutimia na baadae kila nchi itaamua kuendelea na yake.

Wenye Akili tuliliona hili zamani mno.
 
Nadhani silaha anazopitisha hapa Ni zile common na ambazo kila nchi itakua nazo.

Kwa mfano wkt anapeleka silaha Mozambique,ametumia dege la C-130 Mali ya UAE na silaha nyingi anatumia dege hizo kuzibebea kuzifikisha nchini kwake,Amenunua drone zile za turkey Bayraktar TB2 zillikua 10 zimeletwa na dege la turkey.So nadhani labda inategemea na unyeti wa silaha na silaha.

View attachment 2403231View attachment 2403232

Ovious kila nchi inambinu za kusafirisha silaha zake lakini kwa baadhi njia ya maji ni common ndio unakuja hiyo ya midege mikubwa ya kijeshi kubeba silaha lakini napo ni sawa na silaha za maonesho ya jwtz kamwe hawaoneshi kila kitu kuna akiba kubwa iko kwenye maghala huko na makamanda wako well trained kwa matumizi ya silaha mpya kila wakati hivo sio kinyonge
 
Ndio Maana nimesema Silaha anazopitisha TZ au Kenya Ni zile Common.PK Ni mwanajeshi so anajua anachokifanya Maana Kama sisi layman tunaelewa haya, nadhani yeye anajua zaidi.
 
Fahamu kua udugu wa Rwanda na Uganda hua ni wakipekee ulianzia kwa RPG , rwegyema, kagame, mwasa na makamanda wengine kupigana msituni na kumweka museveni madarakani, na hawawezi kuachana, Baada ya pale museveni akawasaidia ndugu zake hao kushika madaraka Rwanda na ikawa hivo lakini Museveni mzee ana heshima ya kipekee kwa Tanzania licha ya kua trained Tanzania na undugu na familia ya mwalimu Nyerere na urafiki na wazee kama Butiku kamwe hawezi kuipiga Tanzania isipokua atajitahidi asuluhishe kama alivyokua akifanya mara zote inapotokea mzozo baina ya Dar na kigali, na historia ya maziwa makuu utaishangaa Rwanda na Burundi huongea Lugha moja na watu wa Ngara, kigoma lakini Baganda hushabihiana lugha na wahaya, lakini pia Nyankole na rwanda na kerewe na zinza huchangia baadhi ya maneno kwenye lugha zao kama ilivo masai Tanzania na kenya, jaluo Tanzania na kenya interection ni kubwa mno japo kagame anavuruga kwa wizi wake wa mali ya kongo
Rekebisha hii sentesi yako kwanza, Museven si kwamba hawezi kuipiga Tanzania kwa sababu hizo ulizoeleza hapo Bali uwezo huo hana.

Waunde Alliance Kagame na Museven kupigana na Tanzania cha kwanza tutaifuta Rwanda kwenye ramani ya dunia Pili tutamuondowa Museven madarakani na kumuweka Rais mwingine Uganda.

Huu ujinga wawafanyie Wacongo Man walioinvest kucheza Kwasakwasa tu, maana hata Che Guevara aliachana nao baada ya kuwaona wanaendekeza pombe, umalaya na kwasakwasa tu akaona hapa hakuna wanamapinduzi, akaondoka zake akarudi Dar akamuaga Nyerere akarejea Cuba.
 
Ndio Maana nimesema Silaha anazopitisha TZ au Kenya Ni zile Common.PK Ni mwanajeshi so anajua anachokifanya Maana Kama sisi layman tunaelewa haya, nadhani yeye anajua zaidi.

Sisi raia wa kawaida ambao hatuna hata mafunzo ya kijeshi yoyote tunafahamu kidogo sana mambo ya silaha na vita lakini PK ni mbobezi na hakuna mtu msiri kama PK kwenye medani yuko vizuri pamoja na ujinga wake
 
Uwezo wa Fdlr kuwa tishio kubwa kwa Rwanda ni wa kutiliwa shaka, nakubaliana kwa sehemu na wewe huenda uwepo Fdlr unatumika kama sababu ya kudumisha uwepo wa Rwanda huko Kivu na kuzuia kujitanua kwa ushawishi wa hasimu zake Uganda na Burundi.

Ila kitendo cha Drc kuruhusu majeshi ya Uganda na Burundi kuendesha operation huko Drc huku Rwanda ikiwekwa kando huenda imechangia kwa Rwanda kuanzisha upya huu uasi wa M23.
Ninakubaliana nawe hapa mkuu, ni hatari sana.
 
Na nani Kakudanganya kuwa Tanzania nayo kwa Msaada wa aliyekuwa Rais wa Congo DR Swahiba Joseph Kabila, Rais wa sasa Tshisekedi na kwa Maafisa, Wanajeshi wake walioko MONUSCO na Wafanyabiashara Wakubwa nao hawaibi Madini ya Congo DR?

Huna unachokijua tulia tukufahamishe.
hahahaha
 
Uwezo wa Fdlr kuwa tishio kubwa kwa Rwanda ni wa kutiliwa shaka, nakubaliana kwa sehemu na wewe huenda uwepo Fdlr unatumika kama sababu ya kudumisha uwepo wa Rwanda huko Kivu na kuzuia kujitanua kwa ushawishi wa hasimu zake Uganda na Burundi.

Ila kitendo cha Drc kuruhusu majeshi ya Uganda na Burundi kuendesha operation huko Drc huku Rwanda ikiwekwa kando huenda imechangia kwa Rwanda kuanzisha upya huu uasi wa M23.
Count Capone Bukyanagandi mtu chake zitto junior
hahahaha,juzi kati wakati felix anabadili majenerali ,nini ilikua maoni yako?
 
Umeandika kitu kwa Jicho la Tai Hasa Diplomasia lakini na medeni za uchumi kwa ustawi wa Jumuiya Yetu.. Wengi mmekulupuka pasi na kumwelewa mtoa hoja..
 
Ndio muungano ndio nguvu yenyewe kuanzia kiuchumi na kijamii, ndio maana EAC inajitanua kila leo Congo iko EA , sudan ndani, somalia ndani baadae tutaihitaji ethiopia, eritria na djbout hapo tutabaki tunalilia kanda sasa ziungane SADC, EAC , COMESA, ECOWAS na kadhalika zije pamoja tuingie ndani ya AU iliyo kamili na kuondoa vikwazo kwa watu wa Africa lakini wavurugaji kama kagame wanatakiwa kuonywa sana maana wanatamaa za kupita kiasi
Bila ile conflict Rwanda itakuwa bankrupt, maana wanavyowapa silaha wale M23 ni kwa ajili ya kuvuruga usimamizi na kuwezesha uchotwjicwa madini kwenda Rwanda, hii conflict ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Rwanda, bila hii vita Reanda itafilisika, hawawezi kukubali vita iishe
 
hahahaha,juzi kati wakati felix anabadili majenerali ,nini ilikua maoni yako?
Huenda alikuwa anajaribu kutafuta akili mbadala..

Kuna wakati raia wa Drc walimuona Kabila kama dhaifu na ameshindwa kukabili tatizo la ukosefu wa usalama na wengine kumuita kibaraka wa Rwanda na Uganda ila nadhani Sasa wameshapata majibu kuwa Kabila hakuwa sehemu ya tatizo ila hata yeye alipambana Sana kukabili tatizo.
 
Umeandika kitu kwa Jicho la Tai Hasa Diplomasia lakini na medeni za uchumi kwa ustawi wa Jumuiya Yetu.. Wengi mmekulupuka pasi na kumwelewa mtoa hoja..
Asante Mkuu na labda nikuambie tu kuwa GENTAMYCINE sijawahi hata Siku Moja kueleweka na Wapumbavu kadhaa ( kama siyo wengi ) hapa, ila huwa naeleweka vyema na upesi na Watu Intelligent ( Brainy ) kama Wewe na Wengine wachache sana.
 
Bila ile conflict Rwanda itakuwa bankrupt, maana wanavyowapa silaha wale M23 ni kwa ajili ya kuvuruga usimamizi na kuwezesha uchotwjicwa madini kwenda Rwanda, hii conflict ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Rwanda, bila hii vita Reanda itafilisika, hawawezi kukubali vita iishe
Hopeless Rwanda inaiba Madini ya Congo DR peke yake? Una uhakika kuwa Tanzania yako nayo hawaibi ( japo wanajificha katika Mgongo wa Kuwasaidia ) Congo DR Kijeshi na Kiusalama?

Kama Rwanda inaiba Madini ya Congo DR na je, zile Ndege za Ufaransa, Ubelgiji, Italy, Marekani na Afrika Kusini huwa zinabeba Makende yako 24/7 Kusafirisha Makwao? Huwa mnazishambulia hizi nchi kama mnavyoishambulia Kutwa Rwanda?

Wanafiki na Wapumbavu wakubwa.
 
Kwani Rwanda akiiba hayo madini anabaki nayo?, si anawateja wake wakubwa hao uliowataja wenye ndege zao hapo?
 
Suluhisho kikosi kazi kiingie misitu ya Congo Munusco ikapumzike imeshindwa Jukumu

Atajulikana anayewatuma wale waaasi

Inachosha Africa ya Waasi na makundi yanayotajwa ya kigaidi na jihadi zao za Kwenye machimbo ya Madini na Mafuta
 
Back
Top Bottom