Kwa niliyoyashuhudia katika Uchaguzi huu, Poleni viongozi wa Upinzani

Maumivu ya Lisu ni ya taifa kama wameweza kumuumiza mtu kama yeye hawashindwi kwa kabwela yoyote. Hivyo lazima tupambane kwa umoja.

Hoja yako ya kwanza ni kweli kabisa walipaswa kuongoza watu kupigania mazingira ya siasa kwanza. Kwani mpaka sasa katiba bado ni mbovu. Na nimeapa uchaguzi huu mwisho kushiriki ikiwa mazingira hayatakuwa fair. Nilikuwa nisishiriki ila nineshiriki kwa sababu ya damu ya Lisu iliyomwagika kuonesha kuwa napinga dhuruma na kuchagua haki. Na hili litanisimamia kiroho kwa muda wote Magu akiwa madarakani mabaya yake hayatanipata na uzao wangu na mazuri yake tutagawana na waovu sawa.
 
Hahahahaha kwahiyo Wewe uliesema Airforce one ndio ndege kubwa kuliko zote duniani ndo una IQ kubwa? Kwakwakwakwa!
 
Watanzania wengi ujinga umekita mizizi ndo maana licha kusoma elimu ya kukariri lakini uwezo wa kupambunua mambo ni mdogo sana
Nimeshangaa sana kukuta kituo kimoja kura zilizoharibika zinafika 40!! Kama hata kupiga kura tu ni mtihani mengine?
 
Nimekuja mbio kutaka kujua madudu uliyo yashuhudia. Tafadhali tumegee kidogo mkuu
 
Yule kiongozi mkubwa kabisa anayetishia wananchi waliochagua wabunge na madiwani wa upinzani yeye ana IQ ya level gani? Naomba kueleweshwa.
 
Kiongozi mbona naona unatumia lugha kali sana kwa wananchi na kukata tamaa!
 
Watanzania hawawezi kuahatarisha maisha yao kumpigania Amsterdam
 
Sio suala la kuwashawishi kwa maneno tu bali kwa kuwaletea wanamuziki ka kina diamond bure, kuwapa fedha buku tano, kuwatisha kupitia ujinga wao kuwa tutakuwa kama libya. Hiki ni kitu ambacho mtu mwenye akili hawezi kufanya ili kumshawishi mtu.
Kwa kifupi "watu humchagua kiongozi anaefanana na wao!!"
 
😂😂😂Lissu atamjazia mtu inzi mda siyo mrefu
 
Nakubaliana na wewe watanzania ni ajabu sana sitegemei kuona wakilalamika tena maisha magumu..
 
Sheria mama, Katiba, inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa sana ili kuweka mifumo huru na imara ya uchaguzi ambapo maamuzi ya wananchi yanaweza kuheshimiwa na sio vinginevyo.
 
Leo niliamua kupiga kura muda ya jioni kwa lengo la kwenda kuona picha halisi. Nilifika kituo ni saa 9:25 alasiri ikiwa imebaki do 45 kipenga kipulizwe. Ninashukuru nimekuta wakala wote wa CCM na Chadema tu. Msimamizi alikuwa friendly sana. Wakati anafungua faftari kutafuta jina langu nilishikwa na butwaa kuwa turn up ilikuwa ndogo. Yaani tick ni chache mno. Nikamuuliza vipi mbona muda unaisha na watu bado? Naye anasema hajui. Jioni hii nimeshapata taarifa Diwani ni CCM na Mbunge na Uraia wameongoza CCM. Kesho ndiyo nitapata kura halisi kwa wagombea.
 
Ndio maana hujawa na hautokuwa kwa akili na ufahamu ulionao sahau. Subiria kuitwa kwenye vikao vya chama na kuondoka na buku mbili.
Mkuu mambo yanakera kinoma Yani tunamalizana sisi kwa sisi afu baadae watu wanalalamika kuwa hali ngumu
 
Na mm ninakir kabisa ni mtanzana mjinga mm pamoja na familia yangu
Eti nikapige kura kwa faida ya nani?

Nikatumike kama karai kwa maendeleo ya familia nyingine
Awe Gwajima au mdee akiwa mbunge mm ninapata faida gani?

Watanzania wanajiuliza maswali kisha bushit ngoja niende kwenye mishe mishe zangu huyo Halima Mdee atapigiwa kura na ukoo wake au familia yake kwa sababu watakuwa na faida au maslahi kwa familia zao
Halima nimemuweka kama kielelezo tu lakini hii inawahusu wabunge wote , madiwani wote hata urais
Watanzania uwa atupigi kura kwa sababu…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…