Ni sawa kuwa na wasiwasi maana ni kitu kipya na haukijui lakini bado haitoi tafsiri kuwa ni alien ama sio alien!..
Mi ni moja kati ya mtu ambae nina shauku yakutaka kujua ukweli kwamba kuna viumbe wengine zaidi yetu, ila ukiangalia nakufatilia dhana nzima ya ulimwengu na namna unavyofanya kazi unapata jibu kuwa kwa asilimia takribani 60 kuna viumbe huko kwengineko!.
Ila hilo halitoshi kuwa jibu la swali je, kuna viumbe wengine zaidi yetu..?
Kwa ulichokiona wewe ni chombo na wala sio viumbe, na hicho chombo huenda ni binadamu amekitengeneza au hajakitengeneza!. Hayo yote ni majibu swali ni vipi tutapata jibu la uhakika................?????????
Maana ya uthibitisho unaoutaka wewe ni kwamba Hadi uone Kwa macho yako kabisa kitu ambacho hakiwezi kutokea kirahisi hivyo so nakubali na kuielewa hoja yako but kwangu Mimi binafsi nilichokiona Nina 100% hajatengeneza Binadamu, Ile n kazi ya non Human intelligence...
Inakuwa ngumu mtu kukubali sababu anataka aone na Hilo wala sio shida ni nature Tu ya Binadamu...
Baada ya lile tukio nikagundua pia kuna credible peoples ambao wametoka na Ku disclose hizo issues.
Luis Elizondo, David Grusch,Jay Stratton,Dr. Hal Putof, Dr. Eric Davies, Christopher Melon, Avi loeb, Dr.Gary Nolan hawa ni baadhi ya wataalamu, Maafisa wa zamani na wa sasa ambao walishiriki Kwa namna moja ama nyingine katika UAP task force...Even Yule Dr.Edger Mitchell.
Hizi issues za UAP uthibitisho wake ni testimony tu za watu waliohusika kuona au kushiriki kwenye hizo issues, hakuna uthibitisho wa kuona wa recovered material au bodies ambazo unaweza kuona, mfano Hadi sasa licha ya pressure kubwa inayowekwa bado Unelected government officials wamekataa Ku declassified taarifa na Mimi nawaelewa kwanini wanakataa licha ya kwamba wenzao waliostaafu au kutoka katika utumishi wamesema wazi.
Kama former US president Barrack Obama amesema kuwa Aliens "are real" but hata yeye amefichwa ndio utaona namna gani hii issues ni kubwa Sana...
Kuambiwa Kwa mdomo kuwa kitu fulani Kipo na hujawahi kukiona, kukubaliana nacho ni ngumu Sana ni sawa na waumini wa dini na Imani mbalimbali....