Kwa nini nyama choma nyingi bongo ni ngumu sana?

Kwa nini nyama choma nyingi bongo ni ngumu sana?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Ni aina ya mifugo au watu hawajui kuchoma nyoma ? Nyama choma inatakiwa iwe laini uweze kuila hata kwa kijiko



​
 
Umewahi kula nyama ya namna hii
 

Attachments

  • downloadfile-10.jpg
    downloadfile-10.jpg
    61.5 KB · Views: 19

Ubunifu ni mdogo sana kwa wapishi wetu Nyama nzuri na laini inatakiwa ilale na viungo kwenye fridge usiku wa kuamkia kabla haijachomwa. Wengi hawafanyi hivyo.
Sahihi.Hakuna kitu kinanikera kama kuweka nyama mdomoni halafu nakutana na ile harufu kama nyama mbichi.Hawajiongezi ndiyo maana wanatubariki na vitambi vya minyoo tu.
 
Inasemekana watz wengi mnakula misuli badala ya kula nyama.
Kwa maneno mengine mnakula nyama isiyo na ubora ndio maana mnakutana na changamoto za aina hiyo.
Wengi wa wachoma Nyama hawajui ni Sehemu ngani ya Ng'ombe inakua na Yama laini, Wachoma mishkaki wao wanaenda kwenye Butcher na kununua Nyama steki na kwenda kutengeneza mishkaki
 
Inasemekana watz wengi mnakula misuli badala ya kula nyama.
Kwa maneno mengine mnakula nyama isiyo na ubora ndio maana mnakutana na changamoto za aina hiyo.
Uko sahihi! Misuli ya ng'ombe au mbuzi kuwa nyama ni process. Hiki linaanzia tangu anavyofugwa, anavyosafirishwa kwenda machinjioni, anavyochinjwa na misuli inavyobadilika kuwa nyama. Wakazi wa Dar tunakula misuli hatuli nyama. Misuli ya mnyama aliyechinjwa inatakiwa ifanyiwe aging yaani kabla haijapelekwa kwenye cold room au buchani, ikae angalau saa 8 ikiwa imening'inizwa. Hapo ndipo utapata nyama.
 
Back
Top Bottom