Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Mkuu kwa muktadha wa mtu ulikutana naye hapo awali upo sahihi kwa asilimia zoteNdio. Akili zetu hufanya kazi kama miili yetu ya nyama. Kama mnakumbuka kwenye biolojia, ukipata magonjwa, seli zako huhifadhi kumbukumbu ya magonjwa yako ili iwe rahisi kupambana nayo baadaye.
Akili yako ya ndani(subconscious mind), hukumbuka wale waliokufanyia mabaya kipindi cha nyuma. Sasa unapokutana na mtu mwenye tabia hizo au zinazokaribiana, akili inamgomea ili kujilinda.
Pia akili ikiona ishara nzuri, nayo inajirahisisha.
Safi kabisa!Ukisoma na kuijua sayansi ya Quantum physics inaweza kutoa majibu.
Kuna viumbe hai na viumbe visivyo hai katika mazingira yanayotuzunguka.
Chochote kilichokuwepo aidha unakiona au haukioni kwa macho kinakuwa kipo katika mtetemo/vibration.
Hata matter ambayo ipo kwenye solid form Imetengenezwa na particles na molecules ambazo kwa kiasi na kiwango fulani Kuna movements au vibration.
Binadamu, wanyama, wadudu n.k wanaishi katika energetic field Fulani ambayo inawasaidia ku interact.
Hizo energetic field zinakuwa katika frequency au masafa tofauti.
Masafa katika level za energy field yamegawanyika katika high frequency , low frequency & medium frequency.
Hii ina maana kwamba ili uweze kufikia high frequency lazima uwe katika mitetemo au high vibration pia, halikadhalika kwa low frequency unakuwa katika low vibes na hivyo hivyo kwenye masafa ya kati.
Tuje kwenye swali lako, kwanini unakuta unamkataa mtu au unamkubali mtu/kitu/ jambo? Bila sababu yoyote.
Kama ilivyo redio inavyofanya kazi kwenye masafa hivyo hivyo katika maisha ya nishati mambo hapo hivyo
Ukitaka kusikiliza TBC lazima itakulazimu u tune masafa ya TBC, pia ukitaka kusikiliza Radio One, Clouds, Wasafi ni mchakato huo huo.
Kwa binadamu/mnyama ambaye yupo kwenye masafa ya juu lazima automatic atavutia/attraction ya wenzake wenye mtetemo unaofanana au kushabihiana.
Kama upo kwenye masafa ya juu ambayo ni upendo, amani, furaha utavutia aina ya nishati kama yako.
Ukiwa kwenye mtetemo wa kati ni hivyo hivyo pia kwenye masafa ya chini kama wivu, chuki, hasira, aibu n.k utavutia wa design hiyo pia.
Kwa hiyo kinachofanya umkubali mtu au kumkataa ni masafa/frequency mitetemo/vibration na nguvu ya uvutano/ attraction au nguvu ya kupingana/repell.
Naunga mkono ukitoa hapo kwenye mapepoMengine ni mapepo.
Wengine ni opportunists.
Wengine ni wafuata mkumbo.
Wengine hata wao wenyewe hawajielewi.
Hapa tukubaliane kutokukubaliana, hapa nakutana na mtu hanijui na simjui hay sababu zinatoka wapi?Kusema humkubali mtu bila sababu hiyo mimi sikubali lazima sababu ipo tu
Kuna mantiki hapaMara nyingi watu ha wataki watu walio wazidi kitu fulani maana wa kumpelekesha hata kuwepo
Shukran babuKuna kitu kinaitwa hisia
Kupitia hisia, unaweza kumchukia mtu na wakati mwingine kumpenda
Wanawake wanaweza wanaangalia filamu na kujikuta wanampenda mwigizaji fulani kupitia scene aliyofanya
Wakati mwingine kumchukia mwingine kwakuwa scene yake haijawavutia
Wengine huwa wanamchukia mtu kutokana na maneno ya kuambiwa/kusikia
Mathalani kupitia Siasa, Kuna watu wamejengwa kumchukia Tundu Lissu na wengine kumchukia Edward Lowassa
Hii hata kwenye familia, mtoto anaweza kurithi chuki za Mama yake dhidi ya baba yake
Kwamba nilipokulea wewe, baba yako hakuwajibika hata kidogo yeye alikuwa busy na michepuko
Mtoto unakuwa na kuibeba chuki hii then unaihamishia kwa baba yako
N.k n.k
Chunguza lazima kuna sababuNina experience na hii kitu tena sio mara moja au mbili ni mara nyingi tu
Kwakweli binafsi naona huwa hamna sababu ya msingi,mnajikuta tu kama kipande flan cha puzzle ambacho kimekuja kukava nafasi ambayo imeachwa wazi na kukava kikamilifu, nadhani kuna kitu cha siri ambacho huenda bado hakija kuwa wazi kwenye utambuzi wetu
Na upande wa kutomkubali mtu nayo nina uzoefu nayo pia,yeah unajikuta tu unaona huyu mtu kama sio hivi, yani ni kama umbali wa mashariki na magharibi,hata ukiulizwa mbona humkubali hiyu mtu,unabakia huna majibu
IgweeeeeeeHapo kwenye kumchukia mtu bila sababu, sababu ipo ila mhusika anajua ni sababu ya kifala ndo mana anashindwa kuisema mana ataonekana Ana matatizo ya akili
Sawa diha makinika kuna ma great thinker hapaNipo hapa kusoma tu.
Nipo mdada mkubwaIgweeeeeee
Upo lakini kijana mdogo?
Issue ni deep 😅🙌🏼
Inakuaje kuajeHata mimi hua inatokea tu...
Kuna sababu trust meSipingi mawazo yako,lakini hapa kumbuka hamfahamiani na mtu,maana mkianza kufahamiana ndio Kuna mambo utayajua labda kupitia vitendo vyake au maneno yake
Ila hapa ni kama ile tu unakutana na mtu kwa mara ya kwanza lakini hisia zako chap tu zinakwambia huyu mtu mbona kama sie vile
Kanuni ya nishati law of conservation of energy inaeleza nishati haiwezi kuharibiwa wala kutengenezwa kamwe ila inaweza ikabadilishwa kutoka aina moja au nyingine.Ila
Hii point nimejaribu kuapply kwenye like unlike poles attract like poles repel haileti?
Why
Ni sahihi kabisa ukiwa positive kwa kila kitu ambacho unakutana nacho kwenye maisha yako,utaona funzo kwa kila kitu,kila kitu kina sababu ya uwepo wake, ni Mimi na wewe kuona hekima ya kitu hichoBado nina swali kwanini wanasema kila mtu tunayekutana naye ana sababu maalum kwa maisha yetu either kuwa funzo etc.. unakuta izo frequency ndo zinamvuta au nini au imeandikwa ukutane naye bila ata izo frequency kuendana
Mwaga vitu mkuuKanuni ya nishati law of conservation of energy inaeleza nishati haiwezi kuharibiwa wala kutengenezwa kamwe ila inaweza ikabadilishwa kutoka aina moja au nyingine.
Kabla ya kuja kwenye sumaku na kuongelea hizo like poles na unlike poles inabidi ujikumbushe jinsi gani na namna gani mvutano na kukingana kunavyotokea. halafu itakuwa rahisi kufanya transformation.
Safi kabisa!
Kwenye Quantum Mechanics pia kuna kitu kinaitwa entanglement. Kila particle ina pacha wake na hizi particles zimegotana (entangled) na zinawasiliana papo kwa papo bila kujali umbali uliopo kati yao. Mawasiliano haya yanatawaliwa na mitetemo (frequency) inayofanana. Kwa hiyo, katika ujumla wake, unaweza kumkubali mtu aliyeko Marekani huko wakati wewe uko huku Tandahimba ndani ndani bila sababu yo yote. Kumbe mko katika mgotano na mnatetema katika masafa yanayofanana.
Kuna watu ukimuona tu yaani inakuwa rahisi sana kumkubali na kumzoea. Yaani utafikiri mmeshafamiana kwa muda mrefu. Hata hapa JF. Unaona ID tu ya mtu na nguvu fulani inakuambia kwamba huyu ni mtu poa sana na unamkubali tu otomatikale. Na mwingine ukiona tu ID yake unaboreka hata bila sababu. Kumbe hampatani katika ulimwengu wa roho ambao Quantum Mechanics inatwambia ni mpishano tu wa masafa ya mitetemo ya nishati zenu. Mitetemo hiyo ikigotana, mambo yote safiiii!
➡️➡️➡️ Kama wewe ShesRise_1. Mimi nakukubali sana tu japo sikufahamu. Inavyoonekana nishati zetu zinatetema katika masafa yanayofanana. Pengine mimi na wewe tumo katika mgotano yaani sisi ni soulmates 😂😂😂🏃🏿♂️🏃🏿♂️🏃🏿♂️
Safi kabisa!
Kwenye Quantum Mechanics pia kuna kitu kinaitwa entanglement. Kila particle ina pacha wake na hizi particles zimegotana (entangled) na zinawasiliana papo kwa papo bila kujali umbali uliopo kati yao. Mawasiliano haya yanatawaliwa na mitetemo (frequency) inayofanana. Kwa hiyo, katika ujumla wake, unaweza kumkubali mtu aliyeko Marekani huko wakati wewe uko huku Tandahimba ndani ndani bila sababu yo yote. Kumbe mko katika mgotano na mnatetema katika masafa yanayofanana.
Kuna watu ukimuona tu yaani inakuwa rahisi sana kumkubali na kumzoea. Yaani utafikiri mmeshafamiana kwa muda mrefu. Hata hapa JF. Unaona ID tu ya mtu na nguvu fulani inakuambia kwamba huyu ni mtu poa sana na unamkubali tu otomatikale. Na mwingine ukiona tu ID yake unaboreka hata bila sababu. Kumbe hampatani katika ulimwengu wa roho ambao Quantum Mechanics inatwambia ni mpishano tu wa masafa ya mitetemo ya nishati zenu. Mitetemo hiyo ikigotana, mambo yote safiiii!
➡️➡️➡️ Kama wewe ShesRise_1. Mimi nakukubali sana tu japo sikufahamu. Inavyoonekana nishati zetu zinatetema katika masafa yanayofanana. Pengine mimi na wewe tumo katika mgotano yaani sisi ni soulmates 😂😂😂🏃🏿♂️🏃🏿♂️🏃🏿♂️