Kwa Nini Tunamkubali au Kumkataa Mtu Bila Sababu?

Nadhani kumkubali kumkataa mtu ni mfumo wa kibayolojia wa ulinzi na usalama
Tunavoishi ubongo unatabia ya kurekodi matukio yote tunayopitia sura za watu,mienendo,masimulizi kutoka Kwa watu ,tabia na ubongo hutenganisha hayo yote kutokana na Imani binafsi ya mhusika kama salama na hatari .
Hivyo inapotokea unamchukia mtu bila sababu ni athari ya mfumo wa kibayolojia kukuambia huyo mtu ni tishio kwako au ni hatari kutokana na Imani binafsi japo yawezekana sio kweli huyo mtu ni hatari kwako ubongo hautaki kujichosha kuchambua Kila taarifa kutoka Kwa huyo mtu na mara nyingi ubongo hukosea Kwa kutoa maamuzi kutokana na patterns na sio uhalisia .
Ndomana wanasema usihukumu kitabu Kwa jalada hivyo taarifa ya ubongo inatakiwa iwe taarifa tu ya mwanzo kuhusu huyo mtu na sio final say.
Kwamfano Nina rafiki yangu mmoja kabla ya kuwa mwanangu sana tulikuwa tunapishana kma malori ikatokea tukakutanishwa kwenye jambo Fulani ikawa mwanzo wa urafiki,
Alikuja kunambia nilikuwa nakuona mtu Fulani tofauti na ilivyo kiuhalisia
 
Mkuu kwa muktadha wa mtu ulikutana naye hapo awali upo sahihi kwa asilimia zote

Hapa chukulia kwamba ndio kwanza unakutana na mtu kwa mara ya kwanza hakujui himjui,utasemaje hapo?
Kuna sehemu hujanipata vizuri,

Akili ya ndani ina nguvu sana. Ndiyo inayotunza kumbukumbu zote.

Moja ya kazi inayofanya ni association. Inapitia kumbukumbu zote na kutafuta patterns. Hili jambo ndo linampa binadamu uwezo wa kujifunza. Kama kwenye maisha yako kuna watu wenye tabia flani waliokuumiza, itahusisha tabia hizo na hisia mbaya.

Na inahifadhi vitu vingi sana, mpaka uzito wa sauti, sentensi mbalimbali nk.

Pia inahifadhi mambo unayochukia kuhusu wewe mwenyewe na mambo unayoyatamani. Haya yote yanaweza kuleta hali hii. Kwa taarifa zaidi soma kuhusu subconscious hate.
 
Mkuu umeongelea mambo mengi na mifano mingi sana,safi sana

Na kupitia maelezo yako majibu kama yanakuja kwanini huwa tunapenda mtu kumchukia bila sababu

Sasa ulipozungumzia kuwa kuna kemikali fulani huwa tunazi detect juu ya mtu fulani hapo sasa umegusa hisia ambazo tunazipata bila kujua msingi wake au sababu zake zinatoka wapi? Hapo majibu yanakuja

Au hoja yako ya pili,kwamba miili yetu huwa inaongea zaidi kama utakuwa makini kujua,hapo napo tunapata majibu pia kwanini huwa tunapenda au kuchukia bila sababu,sasa ni vile tunashindwa kuzielezea

Kwa maelezo yako haya kwenye pande hizi mbili nakubaliana na wewe
 
Mkuu Ertugrul Bey Kuna utatu muhimu sana lazima uzingatiwe ambao unahusisha ENERGY, FREQUENCY na VIBRATION.

Fikiria jinsi umbo la pembe tatu lilivyo just a Triangle kama kile kifaa kinawekwa gari ikiharibika na ikitokea limesimama barabarani.

Jaribu kutengeneza muunganiko na uhusiano katika huo wa utatu kwenye pembe tatu huku ukifikiria uhusiano wa hizo pembe tatu yaani nishati, masafa na mitetemo na jinsi zinavyoweza kufanya kazi.
 
Hapa nimekupata umerefresh my mind,haya ndio mambo yangu ya subconscious mind,jumba la kumbukumbu na maarifa kama yote
 
Kwamba bila angle moja kuwepo inakuwa tena sio umbile la pembe tatu kamilifu
 
Kwa hiyo hapa sababu tunayo mkuu si ndio
Kwamba tunavutana kwa frequency zetu zinazowiana

Hii kusema bila sababu sio sahihi si ndio?
 
Alooooo wasalimie kwa mrombooπŸ˜…πŸ˜…
 
Kwa kawaida jambo Hilo la kumchukua na kumpenda mtu bila sababu haiwezekani.
Isipokuwa unaweza kumpenda mtu ikiwa Kuna mambo 4 haya yametokea au mmeyapitia kati ya wewe na muhusika unaempenda au kumchukia.
1. Kuufanyia wema- kikawaida moyo wa binadamu umeumbwa kumpenda anaeufanyia wema kwahiyo mtu anapokufanyia wema unaweza kumpenda.
2.kukufanyia ubaya-moyo pia umeumbwa kumchukia anaeufanyia ubaya.
3.anae mchukia mtu hapendi mafanikio ya mwenzio au amezidiwa kitu kizuri na mtu, kikawaida moyo huanza kujiuliza maswali kwanini yeye na sio Mimi then chuki inaweza kuanza kati ya watu hao.
4. Kupata taarifa za kuwa mtu amekusifu Kwa uzuri au tabia nzuri au mtu Fulani anapenda mafanikio yao, basi kawaida moyo utamuona mtu huyo ni mzuri.
Nje na hapo labda anaemchukia mtu bila sababu awe ni mchawi
 
Shukran mkuu asante kwa maoni
Karibu tena
 
Mkuu this is such a wonderful explanation

Something to add, despite vibrations kuna psychological input pia..

Vibrationaly inatokea hivyo,

Na watu huwa hawajui vibrations zao, au core frequency zao. So wanachuki wa na watu bila kujua, kuwa kuna forces of limits within their very own psyche.

Ila ni kweli na yule aliye juu vibration low key lazima atachukizwa na low vibrational beings.

So it's all about leveling up your frequency na utafikia kuto kuchukizwa na watu

Mkuu Adverse Effect are you into any spiritual practice?

Chukua humu pia ShesRise_1
 
Wow wonderful
Umepiga je hapa😊
Shukran mkuu umeitendeha haki mada yangu πŸ”₯πŸ”₯
 
Wengine hufuata mkumbo tu. Na inaenda mbali zaidi kuwalazimisha na wenzao wamchukie huyo mtu. Yaweza kuwa mi nipo upande fulani koiyo ugomvi wenu usiathiri mahusiano ya wengine
Hii ni mbaya sana imevuka mipaka ya kusema fulani simkubali ila ni chuki ya wazi wazi mtu akikosana na mtu mwingine anataka na wewe urithi huo ugomvi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…