Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Rais anaweza kuitumia bully pulpit yake ku - discourage huo utambulisho anaopewa.

Hafanyi hivyo. Tafsiri hapo ni anapenda sifa za uongo uongo.

Hivi JWTZ nao wakiamua kumpa ujenerali wa heshima au ufield marshall wa heshima, napo ataanza kutambulishwa kama Jenerali au Field Marshall Samia Suluhu Hassan?
 
B kwahiyo bahati ya mwenzio unailalia mlango wazi na gubu, right?
 
Ni aibu sana washamsoma na mataifa mengi yatafanya hivyo mjiandae debe bila content hutika sana
 
Samia kafanya nini kwenye uchumi?

GDP yetu kaikuza kwa kiasi gani?

Kipato cha mwananchi kimeongezeka kwa kiasi gani?

Kaiondoa nchi kwenye utegemezi wa wafadhili?
 
Swala la kusoma Kupata PhD Inawezekana ni swala la utayari tu . So hapo umetumia dharau na kiburi Cha uzima swala la kusoma lipo overrated Sana Ila kila mtu anaweza kusoma akapata Elimu kubwa tu katika Maisha yake.

Ina maana wewe hujui Kuhusu siasa zetu za TANZANIA?
 
Usemacho ni sahihi Mkuu, tatizo la Viongozi wetu wanapenda Sifa za Kijinga.

Hukuona wakati ule wanavyalishwa Makombati ya Jeshi?

Mwenzao Nyerere alivaa wakati ule wa Vita vya Kagera

Wao wanavaa ili wapate sifa, na Machawa wao wanakuja kuwatetea kwamba ni lazima wavae as ni Amiri Jeshi Mkuu 🙌

Siasa imeingia hadi huko Jeshini, kwahiyo kwa Nature ya Viongozi wetu wakipewa hizo Sifa za U-Field Marshall lazima watazipokea na watakuwa wanatamba nazo Majukwaani.

Natamani tupate Rais asiye na hayo ma-Mind set ili tupige hatua za maendeleo, maana Machawa wanawapotosha Viongozi wetu hivyo kuishia kufanya Mark time
 
Nikupe mfano….

Kama Rais wa Tanzania anapewa udaktari wa heshima, basi hata marais wa Marekani hupewa udaktari wa heshima.

Lini umewahi kusikia au kuona Rais wa Marekani akitambulishwa kama Dr. Ronald Reagan? Dr. George H. W. Bush? Dr. Bill Clinton? Dr. George W. Bush? Dr. Barack Obama? Dr. Donald Trump? Au Dr. Joe Biden?
 
Mbona umemsahau MAGUFULI? Unajuwa unaweza ukaficha kitu fulani moyoni ila maandishi yakakuumbua! Inaonekana wewe ni katika ya wale wanaoamini kuwa ili uwe na uwezo wa kusoma au kuongoza nchi ni lazima uwe wa imani fulani, kitu ambacho hata sayansi inakataa! Bytheway what is Phd katika ulimwengu wa leo? Hata mtoto wangu anafanya, na hao walionazo mbona hatuoni matokeo? malalamiko kila kona mnasema nchi haiendi.
 
Mada haimzungumzii Magufuli.

Kama unataka nimzungumzie Magufuli, anzisha mada inayomhusu nami nitakuja kuchangia.
 
Huku kwetu tuna tatizo la ULIMBUKENI 🙌
 
Mada haimzungumzii Magufuli.

Kama unataka nimzungumzie Magufuli, anzisha mada inayomhusu nami nitakuja kuchangia.
Ila umezungumzia maraisi wenye uwezo wa kufanya PhD si ndio? wenye akili wamekushtukia!
 
Haa haa😂.

Lakini ndo hivyo tena, amepata.

Na unajua nini ndugu yangu Nyani Ngabu?

Katika maisha haya, kuna ku - hustle hata ukajistahilisha kupata (earn) kitu fulani mwenyewe Kwa juhudi zako.

Lakini kuna neema pia ya kustahilishwa pasipo wewe kufanya chochote cha ziada na ukapata kitu fulani. Hii hiitwa neema.

Mama Samia Suluhu Hassan amepata neema hiyo. It doesn't matter watu wengine wanaonaje na kuhisi vipi.
 
Samia kapata ‘Neema’ kupewa udaktari wa heshima?

Bure kabisa wewe akili yako.
 
Alafu Machawa wake hawajui ata masharti ya matumizi ya Honoris causa degrees.Hurusiwi kuitumia katika utambulisho wako kama wale Academician waliopata darasani na ndiyo maana ata kwenye CV Honoris causa degree aiwekwi kwenye list ya Academic Background ila inawekwa kwenye list ya AWARDS!
Eti Dr Samia Suluhu Hasan!!!🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…