Hili tatizo sio la kisiasa mkuu ..
Usitumie mihemko, Hilo jengo halijajengwa jana ..
Mjinga wewe kudhani kuwa sio tatizo la kisiasa..!
Hawa viongozi wanaotunga sera za ujenzi na kufanya maamuzi wametoka wapi kama sio kupitia michakato ya kisiasa...?
Wewe unadhani ni kina nani wanaopanga na kupitisha bajeti za mapato na matumizi ikiwemo bajeti ya kuimarisha taasisi za uokozi kuhakikisha Zina vifaa vya kuokolea wakati wa majanga kama sio wanasiasa hawa walioko madarakani wakiwemo wabunge...??
Ni mtu mwenye akili zilizokufa tu kudhani kuwa hayo ni mapenzi ya Mungu kutaka watu wafie kwenye jengo lililojengwa chini ya kiwango na binadamu kwa sababu ya rushwa...!!
Ndiyo, rushwa. Kwa sababu inawezekana kibali cha ujenzi kilipatikana kwa rushwa, consultant kwa sababu ya rushwa alikuwa anaziona kasoro za kujenga chini ya kiwango mapema, lakini hakuchukua hatua kuepusha janga kama hili kwa sababu tu alipewa kitu kidogo kumfumba mdomo...
Rushwa, rushwa, rushwa ndilo tatizo....................!!!!
Na hili linaanzia kwenye michakato ya kupata viongozi tunaowaweka kufanya maamuzi na kusimamia mipango na sera zikiwemo za ujenzi....
Kama kiongozi aliipata nafasi hiyo ya uongozi kwa njia ya rushwa, usitegemee akafanya maamuzi sahihi ktk kusimamia ustawi wa watu anaowaongoza...
Kiongozi wa namna hii hana tofauti na jambazi mwizi na muuaji...
KWA HIYO: Siasa na wanasiasa ndiyo wanaamua kila kitu katika maisha yako....
Wanaamua hali ya uchumi wa nchi, ujenzi na makazi ya watu, elimu, maji, umeme, ujenzi wa barabara, muabudu au msiabudu nk
Kwa hiyo acha kuwa mjinga. Jielimishe Ili uyajue sawasawa mambo haya...!!!