Kwa sasa imani, matumaini na mapendo ya watanzania wengi ni CCM pekee

Katika watu wajinga na wewe umo bwashee.Hivi 2019 na 2020 kulikuwa na uchaguzi???Tuache unafiki.Bila unafiki maisha yatasonga tu.Unafiki unafaida kwa wanaonufaika tu.Na siku wanufaika wakikosa kuna tatizo ambalo hutakuja kulitatua kwa sababu unafiki unakuwa umeshapata mizizi.
 
Chama+serikali
Shuguli zote za kiserekali/taasisi zote Zinasimamiwa na kuongozwa,kuamuliwa na chama
Cha mapinduzi

Jeuri yao ndiyo iko hapo hawa

Ova
 
Pesa za kuwalipa kuandika ujinga kama huu huwa zinatoka wapi?
 
Mkuu tatizo mnakopa sana hela, hebu kopa akili kidogo alafu uje hapa ujibu sawali langu je, hayo matumaini ,mapendo na imani ya watanzania ipo kwenye chama au kwenye miradi aliyoiacha mwendazake pamoja na uchumi wa kati wa mtu moja mmoja ?
 
utofauti wa maoni na mtazamo juu ya mambo fulani sio unafiki hata kidogo, ispokua kama unataka kulazimisha wengine waamini unachoamini wewe, kitu ambacho si sahihi......

binafsi sibabaiki na kuitwa kivyovyote vile, kwasababu mihemko haiwezibadili ukweli amabao upo hadharani mchana kweupe kwamba imani , matumaini na mapendo ya waTanzabia walio wengi ipo CCM

na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ccm itaibuka na ushindi wa kishindo sana, na uchaguzi mkuu ujao baadae2025 pia. sasa hapo unafiki unatoka wap?
 
sasa kwanini asubiriwe hadi astaafu kama anajulikana? ukisubiri asataafu maana yake hukua unajua chochote dhidi yake....

na kama wanalindana na nyie watakatifu si mlindane kukabiliana nao.....

marekani kuna nini cha ajabu au cha maana kuiga?
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Mkuu acha bas.
Kwa mifumo iliyowekwa ni ngumu sana kumshitaki kiongozi akiwa madarakani.
Au hata hili mkuu hauling'amui!?
Wanyonge hawaushika mfumo mahakama hadi tume ya uchaguzi vyote havina uhuru bali vinaendeshwa na chama tawala.
Wekeni tume huru za kimahakama na za uchaguzi halafu muone kama hawatakula za uso hao viongozi.
Marekani kuna mengi ya kujifunza mathalan UHURU WA MAHAKAMA na UHURU NA USAWA WA UCHAGUZI.
 
Tutaona.
 
Mkuu tatizo mnakopa sana hela, hebu kopa akili kidogo alafu uje hapa ujibu sawali langu je, hayo matumaini ,mapendo na imani ya watanzania ipo kwenye chama au kwenye miradi aliyoiacha mwendazake pamoja na uchumi wa kati wa mtu moja mmoja ?
kukopa ni lazma tukope kama nchi,
ili kuimarisha huduma muhimu za kijamii kwa maslahi ya wananchi wote katika maeneo mbalimbali ya kisekta kama vile Afya, kwasababu bado kuna uhitaji mkubwa wa huduma hizo muhimu....

na kwasababu ya kuimarika sana kwa huduma hizo muhimu sana kwa wananchi mathalani maji, elimu, kilomo, fursa na mazingura bora ya biasahara, mapendo ya waTanzania kwa CCM yameongezeka mara dufu, imani na matumaini ya wananchi ni kubwa mno kadiri siku zinavyosonga
 
Chama+serikali
Shuguli zote za kiserekali/taasisi zote Zinasimamiwa na kuongozwa,kuamuliwa na chama
Cha mapinduzi

Jeuri yao ndiyo iko hapo hawa

Ova
huo ni upotoshaji,
hakuna jeuri yoyote kuongoza chama na serikali ya wananchi wenyewe
 
anaeona hivyo unavyodhani haviko sawa ni wewe, na wachache wenzio, tumieni namna ya kidemokrasia, kisheria na hata mass actions ili kushawishi wananachi walio wengi wawaunge mkono nyinyi muwe wengi zaidi dhidi ya waTanzania wanao ona mambo yako sawa

unalalamikia tume iliyoundwa na wananchi, mahakama ya wananchi n.k, si uwashawishi wabadili sasa?

otherwise utapiga makelele tu without impacts..
 
Kwani ni lini chama kingine kilishika nchi mpka useme iman na matumani kwa sasa ni ccm?
imani, mapendo na matumaini ya waTanzania kwa chama na serikali sikivu ya ccm, ni makubwa kupindukia, isivyo kawaida
 
Mkuu huu mjadala utasemaje napiga kelele tena!?
Una uhakika kama tume ya uchaguzi imeundwa na wananchi au CCM?
Usiseme mimi na wachache sema asilimia kubwa ya raia.
Hao raia wana ngao ipi ya wao kuweza kuitumia ili kuonesha ukweli!?
Halafu wakishaonesha ukweli mamlaka ipi itaufanyia kazi huo ukweli!?
Kama Tundulissu tu aliongea machache na kupigwa risasi raia wa kawaida wana sehemu ipi ya kuuonesha huo ukweli!?
Nasisitiza badilini katiba,wekeni mahakama huru na tume huru ya uchaguzi kesha mtaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ