Kwa sasa jukumu la kusomesha watoto apewe mwanamke pekee, wanaume tunadharaulika sana watoto wakifikia kilele cha mafanikio

Ndio mnajengewa nyumba halafu sisi tunaambiwa nyumba yetu ya kudumu no kaburi eti!!!
Mkikubaliana na Ukweli wa toka dahari kwamba hakuna jambo linatokea bahati mbaya hapa duniani, mtachagua njia sahihi ya kupita na kupitisha kizazi chenu cha kiume.

Life will never be fair, and that’s the best part!
 
Exactly mkuu,una hoja usikilizwe
 
Kutimiza wajibu wako kama baba wa familia hilo ndio jambo la msingi bila kujali yajayo.
 
Umeandika kwa machungu sana. Pole sana kwa yaliyokukuta
 
sitii neno apa,,time will tell.
 
Safi sana. Tunaanza kuwabadilisha ubini sasa. Kama baba yake ni john nundu mtoto ataitwa jina la umamani. Anaelipa ada ndo anaemiliki mtoto ili msuse kwa haki🤝
Labda tuangalie kwa uchache mahitaji ya familia.
1. Chakula na mavazi

2. School fees.

3. Umeme luku.

4. Bill ya maji

5. Ulinzi shirikishi.

6. Tozo ya takataka.

Sasa kwakuwa sasa hivi wanawake wana ajira zao, hivi hapa ukilipa school fees halafu baba akacover hizo item 5 ndio zinakupa akili ya kumbadili mtoto ubini?

Tena hapo sijaingiza kodi ya nyumba kwa waliopanga nyumba.
 
Kwahiyo school fees unaongelea ya shule za kata au??

Wanaume mnasusa watoto wenu ili mumkomoe mwanamke? Mambo yasiwe mengi kama ameweza kulipa ada, basi tozo za takataka 3000 kwa mwezi hawezi kushindwa kupata. Matumizi ya umeme watapunguza kwanza mda wa kuangalia tv mnapata wapi mnashinda makazini na shuleni.

Inshort
Wanaume mshapoteza mamlaka ya uanaume maana saizi familia nyingi walipaji ada ni wanawake mkubali mkatae. Mmekaa wakata viuno tu
 
Mwanaume unalilia upendo wa watoto wako? Unataka kudekezwa kama wanavyomdekeza mama yao? Wanaume tumeumbiwa mapambano toka utoto hadi uzee, hakuna kuonewa huruma unavuna ulichopanda, hicho unachovuna ndicho ulichopanda, usilalamike na kutaka kuonewa huruma.
 
 
Kwenye psychology kuna aina tofauti za malezi. Vile utakavyomlea mtoto wako ndio mbegu flani unaipanda kwake. Malezi yetu kwa watoto ni mbegu ambayo matunda yake ndio tutakayo yavuna uzeeni.
 
Watoto ukitaka wakudharau na kukutenga wakikua basi mtese mama yao, ujanani hukujali wanao waliishi vipi ni kutoka alfajiri kurudi usiku wa manane uko bwax na matusi ovyo ovyo leo umezeeka watoto wakupende hiyo vipi?? Hawakukuzoea tangu watoto ukubwani watakuwaje close
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…