Kwa sasa sipo tayari kuolewa, nahitaji kufanya mambo yangu

Iyo iyo pressure ndio desperate yenyewe ninayoiongelea kuhusu hao wazungu achana nao wewe sio mzungu, wewe muafrika ishi kwa kanuni za afrika na hao wazungu waache waishi kwa kanuni za kizungu
 
Mkuu ujue unapojadili mada kama hizi jitahidi usijiongelee wewe binafsi bali ongelea uhalisia uliopo kwenye jamii, hivi katika hali ya kawaida tu ni wanaume wangapi ambao wameoa na wanafanya hayo majukumu wengi huwa wanadai wameoa ili iweje hata humu wanaume wengi husema hawako tayari kufanya hayo majukumu hata iweje, wakati huo huo wanataka wake zao wawasaidie kutafuta pesa na kuhudumia familia na wakitoka huko kwenye mihangaiko wafikie majukumu ya jikoni na baadaye ya chumbani, na wanawake wengi tu walio kwenye ndoa hayo ndio maisha yao sasa wewe hao wanaume unaosema wanafanya kazi za nyumbani sijui ni wa wapi, hebu waambie wajitokeze tuko tayari kujichanga kuwajengea masanamu
 
Iyo iyo pressure ndio desperate yenyewe ninayoiongelea kuhusu hao wazungu achana nao wewe sio mzungu, wewe muafrika ishi kwa kanuni za afrika na hao wazungu waache waishi kwa kanuni za kizungu
Mjomba una uwezo mdogo sana wa kujenga hoja hapa tunaongelea uhalisia wa wanawake wote duniani msilazimishe tuwaongelee wa kiafrika tu ambao wote tunajua wazi ni mitazamo ya jamii ndio inayowasukuma kutaka kuolewa kwani hao wa kizungu siyo wanawake, sasa mtu akishafanya jambo fulani kwa msukumo wa watu waliomzunguka basi huwezi kusema hiyo ni asili bali ni mentality iliyosababishwa na external forces na kama ingekuwa ni asili basi ingekuwa kwa wanawake wote duniani, lakini wakati huo huo ninyi wanaume ambao wala hamna pressure yoyote mna uwezo kuoa hata uzeeni au hata msioe kabisa cha ajabu bado mnaoa tena wengi wanaanza kuwaza ndoa wakiwa bado vijana kabisa ilihali ukiona mwanamke anawaza ndoa ujue ni either ameshazalishwa au umri umeshaenda au maisha magumu
 
Tupo afrika tunaongelea uhalisia kwenye jamii ya kiafrika sio jamii ya kizungu., unataka kuendelea kupelekewa moto mpaka ukifika miaka 50 ndio uoelewe nenda kaishi kwa wazungu ambao kwao iyo sio ishu ila wanaume waafrika hatuoi makapi
 
Tupo afrika tunaongelea uhalisia kwenye jamii ya kiafrika sio jamii ya kizungu., unataka kuendelea kupelekewa moto mpaka ukifika miaka 50 ndio uoelewe nenda kaishi kwa wazungu ambao kwao iyo sio ishu ila wanaume waafrika hatuoi makapi
Basi ndio msilazimishe kwamba uhitaji wa ndoa ni asili ya wanawake kwa sababu ukishaongelea wanawake basi usibague wa jamii fulani, hata hawa wanawake wa kiafrika siku jamii ikiacha kuwapa pressure basi tarajieni kusumbuliwa zaidi ya hapa na wanaume wengi wanalijua hilo ndio maana wanaendelea kuwapa pressure, mnasema hamuoi makapi kwani hawa wanawake tunaowaona wanaolewa kila siku wote ni mabikira au mnajitoa ufahamu tu ninyi endeleeni kujifajiri huku mitandaoni ilihali uhalisia ni tofauti eti bikira bikira mzitoe wapi wakati mlishaziharibu wenyewe ninyi mlidhani kwamba mtaumbiwa nyingine
 
Mwanamke ndie yupo desperate na ndoa kwa sababu demand yake kwenye soko la mahusiano inawahi sana kushuka, mwanamke akifika miaka 30 tayari ashakua makapi tofauti kabisa na mwanaume. Suala la pressure kila jinsia inakumbana nalo katika angle tofauti hata ukija upande wa ku-maintain costs za mahusiano wanaume tunapewa pressure tunaambiwa "tafuta hela", "no money no honey" n.k mwanamke akiwa broke na mwanaume akiwa na hela mahusiano yatadumu ila mwanaume akiwa broke mahusiano hayawezi kudumu hata kama mwanamke ana hela za kuyadumisha kwaiyo kila jinsia inakumbana na pressure katika angle tofauti, vilevile mnavyodhalilisha na kuwaona takataka wanaume wasiokua na hela(hii inawapa wanaume chachu ya kutafuta hela) ndio ivyo ivyo mkubali na nyie kuitwa makapi(hii inawapa chachu ya kujitunza na kufanya maamuzi makini mnaingia kwenye mahusiano na mtu)
Hao wanaolewa na nice guys(idiots) au wanaume wasiojua historia zao, hakuna mwanaume makini ataoa mwanamke ambae anajua kabisa alikua malaya.
 
Ni kweli wanawake wana uwezo wa kufanya multitask kuliko wanaume.

Wanaume wanahitaji ndoa kuliko wanawake, mwanamke anaweza kuishi maisha yake yote bila kuolewa na akafanya vyema.

Wanaume ni wabinafsi sana, wanawake wana roho nzuri sana na huruma.

Wanaume hawawezi kufanya majukumu ambayo wanawake wanafanya kama kazi za nyumbani kupika, usafi n.k

Wanaume hawana msaada wowote kwa wanawake zaidi ya kuwatumia kwa ngono na kuwatumikisha kama watumwa.

Nimekuelewa mkuu.
 
Naona umeamua kifunika kombe mwana haramu apite. Uyo jamaa anapenda sana ligi sijui analipwa kubishana na watu.
 
Ndoa zenyewe zipi sasa, za kuviziana na kuchepuka. Ndoa zilikuwa zamani. Za sasa stress tupu.
 
Wanawake wengi wakishazaa na kukuza watoto, hawahitaji tena ndoa. Wanataka kuwa huru na kujiamulia mambo yao. Kinachowakalisha kwenye ndoa ni security tu la sivyo, hakuna ambaye angetaka ndoa.
 
Wanataka kuwa huru na kujiamulia mambo yao.
Hapo kwenye kujiamlia mambo yao ndipo kunakuaga na makandokando, ukiona kauli iyo kutoka kwa mwanamke "nahitaji muda kujiamlia mambo yangu" ujue ndio wale wale tu.. wewe mambo gani ya maana hauwezi kujiamlia ukiwa ndoani? Hivi umwambie mumeo unataka kufanya kazi, kufungua biashara n.k unataka kusema mumeo atakunyima uhuru wa kufanya ivyo? Hayo mambo yenu mnayodai mnataka kujiamlia ndio yale yale tu uhuru wa partying, kudanga, kurudi home muda wowote bila kubanwa na yoyote
 
Ndio ukweli wenyewe huo. Nayaona mengi huku mtaani, watu hawataki kubanwa, especially wikifikia umri fulani. Kudanga ni tabia ya mtu
 
Mwanamke yuko desperate na ndoa kwa sababu ni mitazamo ya jamii ndio imemfanya awe hivyo hata hiyo kuona kwamba akishafika miaka 30 anakuwa makapi nayo ni mitazamo ya kipumbavu tu ya wanaume wa kiafrika na siyo kwa dunia nzima, sasa kumbe umeshakubali kwamba wanawake kuhitaji ndoa ni kwa sababu ya msukumo wa jamii na siyo asili kama ambavyo ninyi mnadai mnatafuta pesa kwa msukumo wa jamii sasa muda wote huo ulikuwa unabisha nini ilihali ninyi wanaume mnaoa bila huo msukumo wa jamii, halafu mbona wanaume kibao tu wanaona single mothers hakuna cha nice guys wala nini hao mnaowaita nice guys ni wanaume ambao wameamua kuacha kuishi kwenye fantasy na kuja kwenye reality wamekubali kwamba kama mnataka wanawake wajitunze basi hiyo inamaanisha hata wanaume nao wanatakiwa wawe tayari kujitunza vile vile
 
Bahati nzuri au mbaya hiki ulichoandika ndio uhalisia kwenye dunia ya leo, wala usifikiri kwamba umeandika kunifurahisha mimi, hiyo ndio hali halisi iliyopo kwa wanawake
Naona umeamua kifunika kombe mwana haramu apite. Uyo jamaa anapenda sana ligi sijui analipwa kubishana na watu.
Tatizo lenu hamtoi maelezo ya kueleweka halafu mnataka watu wakubali kirahisi tu, watu wakiwabishia mnaishia kuwaita wabishi na wajuaji mara sijui wanalipwa kubishana kumbe ni ninyi ndio hamna hoja, toeni hoja na majibu ya kueleweka na yaliyonyooka siyo mnawalazimisha watu wakubaliane na upumbavu unaoendelea kwenye jamii kwa kisingizio cha 'nature'
 
Wewe haupo tayari kwa majadiliano ya hoja wewe akili yako ishajiandaa kupinga yaani haijalishi mtu ataongea nn unachoangalia wewe ni angle ya kupinga tu., haiwezekani watu wote unaobishana nao kila siku hakuna hata mara moja ushawai kuona point yaani uwe mtu wa kupinga pinga tu hakuna siku hata moja ulishafika muafaka na mtu ndio maana mwamba uko juu kaamua kufunika kombe mwanaharamu apite. Hakuna mwanamke mwenye maadili au nia ya kudumisha ndoa yake atazisikiliza sound zako wataishia kukujaza upepo tu hapa hapa lakini hawawezi kuapply kwenye ndoa zao wanajua kitakachofuata, hakuna mwanaume timamu anaweza kukubaliana na huu upuuzi unaoubiri humu kila siku
 
Shida unahisi au kudhania kuwa hapa tunashindana hoja jambo ambalo si kweli. Kimsingi hapa unabishana na ukweli ambao muda huuleta katika maisha ya kila mtu kulingana na sababu zake.

Mwanamke ndie anayehitaji ndoa kwasababu ya benefits zake na sio kwasababu ya ndoa jina. Wewe kama unabisha bisha kwa sababu umeamua kuleta ligi ila huo ndio ukweli ambao utakuja kuprove hata ubishe vipi.

Ndoa si jambo wala haja ya mwanaume na ndio sababu ambaye huwa anajutia mara nyingi ni mwanaume siku za baadae.

Wanawake huanza kuona sababu au umuhimu wa ndoa age ikienda sababu hawana sababu za kuwavutia wanaume.

Unavyosema kila mtu ana muda wake wa kuingia Ndoani una maanishaje ati?

Unaongelea ndoa jina au ndoa taasisi?

Mwanamke wa miaka 30+ unaolewa na nani katika umri huo ambae atakuwa alikuwa amekaa tu akikungojea uje aishi na wewe?

Na tutakupeleka hospitali kweli kwa utakachoshuhudia. Kwanza hautakuwa hapa kubishana maana utakuwa tayari umeshajionea ukweli na upo huko uraiani unaishi life lako.

Kuna watu tulikuwaga nao hapa JF tukibishana hizi hizi mada miaka ya 2012 na 2013 hapo. Leo wapo kimya huwaoni tena sababu umri umeshakwenda wamejionea sasa uhalisia na wanajua sasa Maisha sio maigizo ya bongo movie.
 
Wewe bila wanaume kupambana na majambazi utakuwa salama wewe?

Nyoka akiingia ndani utamuua wewe?

Gari kuimaintain utaweza hiyo kazi , yule fundi mudi pale gereji ni mama yako mdogo yule au ni mwanaume?

Shida unaleta ligi na ubishi jambo ambalo halina msaada katika mjadala ili tuweze kuelewana.

Ukisema majukumu hayo ni mambo ya ndoa kitu ambacho ninyi wanawake ndio mnakihitaji kwa nguvu na kwa damu na jasho. Ingekuwa hamuhitaji Ndoa then usingesema kuna kuhudumiwa sasa mtu unakiri ndoa haina faida kwa mwanamke ina faida zaidi kwa mwanaume the how the hell mwanaume analipia 290% ya bills za mke, familia na ukoo wako?

You have to be serious.
 
Kipindi cha 26-32 yupo anatembea na boss ofisini kwao amehongwa gari na nyumba kapangishiwa wakija wanaume wenye nia ya dhati anawalinganisha kiuwezo na boss wake mwishowe anawapiga chini.Akishafika 35 anaanza kuweweseka muda umeenda ndipo anakubali yeyote yule anayekuja kumtongoza mwisho wa siku anaangukia kwa viserengeti boys .
Na sio boss tu naiclude na masponsor wengine wanaomuweka mjini
 
Unafanya swala la Ndoa lionekane personal au la mtu binafsi wakati ni swala la ustawi wa kijamii na swala la kitaifa.

Usidhani wanaume tunawabembeleza kwamba nje ya ndoa hatupati tunachotaka. Ni kazi ya wanaume kulinda ustawi wa jamii.

Wewe unaongea hapa ila unaishi chini ya mbawa za baba yako anakulinda na unafaidika na benefits za taasisi ndoa,mama yako angekuwa analeta habari kama zako sidhani kama ungekuwa hapo kuongea haya unayosema hapa. Unaponda kitu ambacho benefits zake kinakufaidisha wewe tena ukiwa mtoto au uzao wa taasisi ndoa.
 
Oohh kwahiyo kumbe lengo lako unataka na mimi nifunike kombe mwanaharamu apite hata kama naona kabisa kuwa yanayoandikwa humu ni tofauti na yanayofanyika kwenye uhalisia, kama ambavyo wewe unaona kuwa hao wanawake wananijaza mimi upepo na hawafanyi haya ninayoyasema basi vivyo hivyo hata hao wanaume huwa wanakujaza upepo kujifanya eti hawaoi makapi sijui masingle mother ilihali kila siku wanawake wa aina hiyo wanaolewa, mnataka kusema kwamba hao wanaume wanaooa wanawake wa aina hiyo hawapiti humu mitandaoni au hao wanaume wanatoka sayari gani ujue uzuri ni kwamba mimi sisikilizi porojo za mitandaoni huwa naangalia yanayofanyika kwenye maisha halisi tu ndio maana huwa naandika uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…