Kwa sera za namna hii, Tanzania inaweza badilisha hali yake ya kiuchumi na kuwa taifa imara ukanda wa Kusini mwa Afrika ama inahtaji mageuzi zaidi?

Kama hapo umeshaona kazi haiendelei fikra lazima zije hela imeliwa ama hazipo na hii inapelekea haylta mwananchi kutokuwa mstari wa mbele kwenye kuinua uchumi wa nchi na kutojali nchi yake
Haijengwi na mkandarasi halipwi kwakua "hicho sio kipaumbele chetu"
 
Hari na molari ya wananchi kutafuta inawezaletwa ama kuongezwa kutokana na nini kinacho sikika masikioni mwao.

Media zikionesha uchapakazi wenye complexity yaani (miradi mikubwa na mizuri wananchi waliokuwa wanaitamani) basi wananchi watajua ama kweli hapa kama huyu tulie mkubali ana onesha juhudi hizi na mimi hebu niamke nikapambane maana tunapoenda ni kuzuri.

Ila ukilala ukiamka unakuta Yanga wamsema hili, msemaji wa simba kakanusha ukienda huku fulani katumbuiza huku huyu kafanya hili inapoteza hari ya wale wanaopambana.

Inatakiwa ifike hatua hata mfanya biashara akikatwa kodi basi anasema lakini inaenda fanya kitu na kimesha fanyika ila wakikatwa kodi sababu hawaoneshwi kwa wingi nini kina fanyika basi wanajua hela inaenda mifukoni mwa watu.

Kwahiyo dira kwa ujumla inatakiwa ibadilike sio kila kitu cha kuwaonesha watu na sio kila kitu cha kukiweka hewani tuweke hewani ufanisi wa kweli na unaofanyika na ulio fanyika utakao chochea hari ya wananchi kupiga kazi na kuwa na mtazamo mkubwa na mzuri kwa taifa.

Kuna baadhi ya nchi ukienda tv zao matangazo wanaonesha major and big projects zilizo kamilika na zinazo endelea ni feeling moja kubwa sana mpaka unasema daah hawa wamefika mbali ila sisi hakuna hili kwa wingi
 
Hatuna Sera yeyote ya maendeleo tuna Sera za kukandamiza Wananchi wawe masikini zaidi kwa kuwafanya watumie usafiri unaoweza kuwaua dakika yeyote Bajaji na Boda boda huku wakikandamiza vitu bora kuingia kwa gharama nafuu Tanzania..
 
Ahsante ssna Mayor Quimby ni kweli naelewa kinacho andikwa hapa huenda kikawa kigumu kwa watu na wanao endesha kulielewa na kulifanyia kazi lakini ukiongea una amsha uelewa wa watu hasa humu Jamii forum.

Ndio maana unaona kila siku zinavyo enda Jamii forum kuna ongezeko la mada zisizoleta tija kwa jamii japo zipo zenye mashiko ila ndio tumesha iita jamii tayari sio kila mtazamo wako utafanana na watu wote na kufanya watu wafikirie zaidi juu ya taifa na mipango endelevu ya Taifa.

Kuhusu swala la manunuzi kutoka nnje kwa wafanya boashara wa soko la ndani nadhani cha kwanza wenye dhamana wanatakiwa wajue wapi kunapo fanya hii hali ibadilike sababu kupanda kwa kiwango cha kubadili fedha kwa hela zote tuzitumiazo kutaleta maumivu ndani ya mwaka huu kabla haujaisha.

Yaani kutapelekea mfumuko wa bei kwa bidhaa za nnje na hii itafanya wazalishaji hata wa chakula wa ndani nao wazidishe bei.

Kulikata hilo kabla halijatokea na kuwa kubwa iangaliwe ni kwa namna gani exchange rates zinaweza pungua na hii usiwe ushawishi wa kisiasa yaani kuwalazimisha wenye taasisi za fedha kushusha kiwango cha rates wakati uhalisia sio hivyo hata bank kuu.

Wakiweza hiyo hali waangalie na ni kwa namna gani wanaweza kuzuia ubadilishanaji wa hizo fedha mtaani kusiwe na flow kubwa mtaani kuliko kwemye taasisi husika ( la muhimu na hatari hili).
Hii itapelekea taasisi kuwa na idadi kubwa kuliko mtu mmoja mmoja na hii itaweza ondoa ulipukaji wa bei ya fedha za kigeni sokoni.

Yapo mengi Siwezi andika yote lakini tukae kitaalamu na kiuweledi zsidi kama si hivyo basi wananchi watachukia na kutoa imani yao moja kwa moja
 
Asante kiongozi kwa andiko ..ila umesahau kwamba tuna kila kitu isipokuwa UONGOZI BORA!
Ahsante sana Mtemi Mbojo uongozi bora unatokana na malengo sera na mafundisho ya wanaopewa vijiti, naimani wanaweza kuwa vizuri zaidi kama wakikaa chini na wakongwe, na wenye nia nzuri ya sera na malengo kwa taifa, yakawekwa mezani basi kila aingiae atajua nini kazi yake.

Lakini tukifanya mambo pasipo sera, malengo na mpangilio tutakuwa tuna rusha ndoano kila upande tukidhani tutapata chochote kitu.

Mkakati uwepo wapi kunapatikana hiki kitu na tutakipataje kwa muda gani na kwa staili ipi ikisha tambulika basi mmoja anatoswa tuu kikubwa walio nyuma yake wamshikilie yeye vizuri au kamba ilio kiunoni kwake waishike vizuri ndani ya muda tutapata kila samaki tuliokuwa tunauhitaji nao
 
Bandiko zuri sana mkuu, lakini hili litafaa kama stories of change humu jamvini kwa ufupi tuna uhaba wa rasilimali watu.
 
Hatuna Sera yeyote ya maendeleo tuna Sera za kukandamiza Wananchi wawe masikini zaidi kwa kuwafanya watumie usafiri unaoweza kuwaua dakika yeyote Bajaji na Boda boda huku wakikandamiza vitu bora kuingia kwa gharama nafuu Tanzania..
Ni kweli Isanga inaonekana umeumia na kuvunjika imani lakini nauhakika wao pia wanatamani kufanya jambo zuri litakalo onekana lakini masikio ya wapokeaji huenda yanaenda kufa inakuwa ngumu kusikia kila mlio mzuri wao wataugeuza na kufikiri nu mlio utakao wapa maumivu zaidi.

Kikubwa ni kwa wenye nafasi kukaa chini na kufanya litakalo leta amani na kuonekana tena kwa watu wao
 
Bandiko zuri sana mkuu, lakini hili litafaa kama stories of change humu jamvini kwa ufupi tuna uhaba wa rasilimali watu.
Shukrani sana City of lies basi kama itawezekana modes walipeleke sehemu ambayo kutakuwa na mchango mzuri wa watu kikubwa taifa liende sehemu bora zaidi na tuwe na hali nzuri zaidi
 
Thread 'Vunja Statasi Kuo, (2025-2050) Ni Nyakati Za Mabadiliko Kuifikia Tanzania Tuitakayo' SoC04 - Vunja Statasi Kuo, (2025-2050) Ni Nyakati Za Mabadiliko Kuifikia Tanzania Tuitakayo
Nimepitia thread yako Smartkahn kuna point kabla ya nini kifanyike umeelezea watanzania ni greedy na hatuna nidhamu pamoja na unafki.

Greedy yaani tunatamaa zilizo pitiliza mpaka tunakosa utu, kuwa wanafki huenda upo ukweli sababu ya kukosa uelewa wa kuchambua mambo bila kukosoa mtu aliepo hiyo sehemu basi tunageuka kuwa wanafki na machawa.

Nadhani kuna muda hawa wenye dhamana wanatamani wakae chini na kujadiliana ya msingi na walio wazunguka ila walipo ongea mawili matatu na kugundua hawapo nafasi ya kuwashauri basi wao pia hawana budi kupokea sifa wapewazo lakini deep down wanaelewa kabisa hawa wana ninafkia ila ndio hivyo wahamasishaji na watu wa pembeni ya viongozi huenda wamekosa namna nzuri na yenye maana kwenye kuwapa ushauri kutokana na uelewa mkubwa na mpana wa mambo ya ndani mpaka ya kidunia yanavyo enda.

Ni mbaya sana.
 
Dira zenyewe ndio hizo watoa maoni wanasema ving'amuzi vya Azam viehuke bei πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Hayo yatie tunahitaji kuwa na viongozi wenye maono na sio kuuza nchi . Na njia mojawapo, hata kama wanasema , serikali haifanyi biashara lakini wanatakiwa kuelewa wa Tanzania wengi hawana mtaji, hivyo ni lazima tuanzie mahali Kwa Sirikali kuhodhi hizo biashara wakati wanakuza uwezo wa watu wake kumiliki hizo biashara/Viwanda nk Kwa kuuza shares kwa wananchi ili kurudisha huo mtaji Sirikali uliowekeza.

Ambao utaendana na kuweka uongozi Bora katika hayo makampuni na usimamizi uliotukuka sio wakiurafiki na kuchukkulia hiki si changu
 
Una mawazo mazuri sana tatizo ni wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data
 
Kwenye swala la maono na kuuza nchi huenda linawezekana kutatuliwa nadhani taasisi za kiulinzi inapofika nyakati na hata kabla ya vipindi vya uchaguzi itumike taaluma ya kuwachuja hao viongozi kwa maslahi ya taifa.

Yaani kiongozi achunguzwe asili, vyanzo vya mapato (hii tasaida hata wananchi kutokuwa na presha juu ya nafasi kwamba hatokuwa na ubinafsi) changamoto zake, yaani impact nchi iyakayo pata baada ya yeye kushika nafasi, itachangiaje na itachukuliwaje kitaifa na nnje ya mipaka, nguvu yake kimkakati katika kuliendeleza taifa hiki kitengo naimani kipo na kama kipo kina takiwa kifanye kazi nnje ya siasa japo haiepukiki lakini kuna muda inabidi.
 
Una mawazo mazuri sana tatizo ni wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data
Shukrani sana nikweli kabisa Benny Haraba huenda wapo wa namna hiyo lakini yakijadiliwa nadhani haitoweza kutokea viongozi wa namna hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…