Kwa sisi wanaume tuliooa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?

Kwa sisi wanaume tuliooa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?

Mwanamke akipata financial freedom lakwanza ni kuondokana na mwanaume maishani mwake. Hatari hawa viumbe. Ni kuwagegeda tuu
Mwanaume anaambiwa "una kila kitu sasa uoe", na mwanamke anaambiwa "una kila kitu kwanini ujifunge chini ya mwanaume?" mwanamke anaweza kuishi single na kuzaa na wanaume tofauti(secret fantasy ya ke wengi) na akiulizwa anajitetea hakubahatika kuolewa ila ukweli ni hataki kuolewa. Lakini mwanaume akiwa na 'unafuu' kidogo wa maisha halafu hajaoa atasikia kila aina ya maneno ya shombo. Binafsi naona ndoa inatakiwa itokane na upendo kati ya me na ke, na si kwa sababu za kiuchumi au presha ya jamii inayotuzunguka.
 
Binafsi Mke wangu ni Msaidizi wangu kwenye mambo mengi, mathalani;

Ananisaidia kusimamia baadhi ya miradi tuliyoanzisha pamoja (Nafanya hivi Kwa kujua kwamba nitawahi kufa kabla yake, hivyo Jukumu la kulea watoto litabaki kwake).

Anasaidia malezi ya watoto wetu

Anasaidia kunipa Utulivu wa mwili na akili

Haya maneno ya hekima kabisa Toka Kwa wazee.

Vijana wanaoa Kwa msukumo wa kupata tendo la ndoa, kosa kubwa sana hilo, hautaweza kuona thamani ya mke kama tendo la ndoa ndio kipaumbele chako.

Mke asipokua Rafiki Yako na msaidizi wako hata hayo mambo ya utelezi hayatakaa sawa.

Hatupishani sana Mzee mwenzangu, swala la malezi ya watoto, uangalizi na usimamizi wa baadhi ya mambo.
Kingine ananipa changamoto za kuendelea kupambana zaidi.

Kadri muda tunavyozidi kusogea, tendo la ndoa linakua sio kipaumbele sana.
 
Nakubaliana na hoja yako kuwa wengi wetu tulifikiri ndoa ni starehe tupu, lakini ukweli ni kwamba ndoa ina changamoto zake. Hata hivyo, hilo haliwezi kutupilia mbali mchango muhimu wa mke katika maisha ya ndoa. Kwa upande wangu, mke wangu ananisaidia kwa mambo mengi ambayo yamekuwa na thamani kubwa kwangu:

1. Kulea watoto: Yeye ndiye anayeshughulika na watoto wetu kuanzia kuwaandaa kwenda shule, kuwapeleka na kuwafuata, kuhakikisha wamefanya kazi zao za shule kwa usahihi, wamelala vizuri, na usafi wao uko sawa. Kwa ujumla, amebeba jukumu kubwa la ukuaji na malezi ya watoto.

2. Kusimamia miradi ya nyumbani: Nyumbani tuna miradi ya ufugaji wa kuku na ng’ombe, na mke wangu anasimamia yote kwa asilimia 100. Ana hakikisha kila kitu kinaenda sawa na hii imetusaidia sana kifamilia.

3. Utulivu wa akili na kimwili: Ninaporudi nyumbani baada ya changamoto za kazi, yeye anahakikisha kuwa akili yangu inatulia. Ananipa mazingira mazuri ya kupumzika na kuondoa msongo wa mawazo nilioupata kazini, hivyo kunisaidia kuwa na ufanisi zaidi.

4. Tulizo la kingono: Ninapohitaji kustarehe kimwili, mke wangu ananipa tulizo la kingono ambalo ni muhimu katika kudumisha uhusiano wetu wa kimapenzi.

Hivyo basi, ingawa ndoa ina changamoto zake, mchango wa mke wangu katika maisha yangu ya kila siku hauna kipimo.
 
Kupunguza makali unafanyaje?
Mwanamke ni kama mtoto ukileta u baby baby sanaa anakupanda kichwani ukiwa kauzu ni balaa kwa kifupi hayashauriki haya wala hayana mwalimu, kuna jamaa alikuja kuniomba ushauri huku anabubujikwa michozi mkewe ana gubu wakati huo mwenzae nna karibia wiki hatuongeleshani na wife ila wakija wageni tunapretend na jamaa ushauri nikampa safi akaondoka ana amani kumbe na mimi niko dhofulhali hapo
 
Uko sahihi, Je ni wake wote wanalijua hili na kulitekeleza? Kwa sababu huwa kuna migogoro ya ndoa kuvunjika na kugawana mali, mzee kutelekezwa na bibie kukimbilia kwingine n.k
unajua mke hana shida na mali, yeye anakuja kusimamia kile alichokikuta, ambaye anakuja kuchuma huyo ni mjasiria mali kuwa makini
 
Back
Top Bottom