Kwa sisi wanaume tuliooa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?

Kwa sisi wanaume tuliooa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?

Wanaume wengi hufa mapema sababu ya direct au indirect pressure toka kwa wake zao. Mwanaume akipata maendeleo kinachofuata ni ndoa ilihali mwanamke akifanikiwa kinachofuata ni talaka. Wanawake wengi wakiwa huru kiuchumi huwa hawana time na ndoa.
wanasema ndoa kwa mwanamke ambaye yupo vizur kiuchumi haina umuhimu kwasababu inaweza sababisha uchumi wake kutetereka kwa sababu baadhi ya wanaume huwabana nakuchungwa muda wote pamoja na wivu uliotukuka hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao
 
Ukijichanganya kwenye kupata mke mwema, kila siku utawaonea wivu mabachela. Wanaume tunakosea mwanzoni kwenye selection, mwanamke lazima umfanyie vetting na umpitishe kwenye mitihani midogo midogo, kupima level yake ya uvumilivu.

Ukitaka kujua huyu ndiye, mpime hofu yake kwa Mungu. Mpime nidhamu yake unapokuwa na fedha au unapopitia changamoto za kiuchumi na vilevile mpime kwa hela unayo mpatia,uone nidhamu yake tena sometimes muongezee, akitaka 30k,mpe 50k.

Kwangu mke mwema ni mwenye, hofu ya Mungu, anajua nini maana ya maisha/mwenye akili ya maisha.
 
Wengi tulikuwa tunatamani kuoa, tukiamini baada ya kuoa maisha yatakuwa full starehe na hakutakuwa na migogoro.

Wapo waliofanikiwa kwa kupata watu sahihi, mpaka wakikaribia kuzeeka sura zao zinakuwa zinafanana.

Pia wapo waliokosa watu sahihi, na kujikuta wameingia kwenye ndoa yenye changamoto; ambao ukikutana nao njiani, sura zao zimekuwa nzito na zimejaa majukumu mazito na ghadhabu za kuingia kwenye ndoa.

Na wengi tunaoteseka kwenye hizi ndoa ni wanaume, sema huwa tunavumilia ndio maana ata takwimu zinaonyesha wanaume wanakufa haraka kuliko wanawake.

Sasa tujiulize swali; Kwa sisi wanaume tulio oa, ukiacha tendo la ndoa, mke wako anakusaidia kwa lipi?​
Vip vingi mke wangu ambavyo ananipa ambavyo yamkini hakuna ndugu yangu yeyote angenipa

1.Kukubali kunizaliaaa ni kubwa sanaaa ambayo amenipaaaaa kuliko vyote
2.Kunilelea wanangu sio kitu kidogo
3.Kufanya tunakoishi paitwe kwa Nyumbani kwa Mzee Kibori Nangai

Hayo yote ni makubwa sanaaa kuliko hata Gamuuuuu Mkuu sijui wewe utafsiri vipi kuwa na mke ,Mkee ni zaidi ya gamu


Tuko tofauti kimtazamooo ,
 
wanasema ndoa kwa mwanamke ambaye yupo vizur kiuchumi haina umuhimu kwasababu inaweza sababisha uchumi wake kutetereka kwa sababu baadhi ya wanaume huwabana nakuchungwa muda wote pamoja na wivu uliotukuka hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao
Kwa maana hiyo ndoa ni kwa wanawake makapuku ili waweze kujiimarisha kiuchumi kupitia mwanaume?
 
kumbuka mtaani hayo maziwa unauziwa mkuu, ng'ombe wako hawezi kukuuzia maziwa, ukienda kununua nyama utanunua nyama tu kila kitu na bei yake, maini bei yake, utumbo bei yake, steki bei yake na nyama ya kindali bei yake. lakini ukifuga ukaamua kumchinja, unapata vyote bure,

Faida nyingine utapata mbolea, buree, ngozi bureee nadhani hapo utakuwa umeelewa umuhimu wa kufuga, kwa kujazia ukienda maeneo ya wafugaji nyama sio kitu cha ajabu sana, wakat huku mjini nyama inaliwa kwa bajeti kulingana na kipato cha mhusika
Wote wawili mnauziwa maziwa na nyama tofauti ni kwamba mmoja anauziwa direct mwingine anauziwa indirect
 
Binafsi Mke wangu ni Msaidizi wangu kwenye mambo mengi, mathalani;

Ananisaidia kusimamia baadhi ya miradi tuliyoanzisha pamoja (Nafanya hivi Kwa kujua kwamba nitawahi kufa kabla yake, hivyo Jukumu la kulea watoto litabaki kwake).

Anasaidia malezi ya watoto wetu

Anasaidia kunipa Utulivu wa mwili na akili
....kufa kabla yake?????!!!!!!!!!
Umeongea na Mungu
 
mtu ajipime kama anaweza kuvumilia wakati mwenza wake anapoanza kupoteza mvuto,maana ule mvuto wa mwanzo mwanzo huisha halafu mnaanza kuona mbona ni mambo ya kawaida haya,kwanini niendelee kukaa hapa,kama umefunga pingi za maisha ni kipengele kingine.
 
....kufa kabla yake?????!!!!!!!!!
Umeongea na Mungu
Nakupa mifano michache kusapoti hoja yangu;
Mwl Nyerere amelala Mauti, lakini Mke wake yupo hai
Mzee Ally Hassani Mwinyi, amelala Mauti, Mke wake yupo hai
Benjamin Mkapa amelala Mauti, Mke wake yupo hai
John Pombe Magufuli, amelala Mauti, Mke wake yupo hai

Hivyo nina matumaini nami nitaanza Kulala Mauti, kabla ya Mke wangu
 
Back
Top Bottom