Kwa tabia hii una tofauti gani na Ibilisi?

Aliumbwa na moto alafu akapewa adhabu ya kwenda motoni kwake hiyo ni adhabu kweli?
Ameumbwa kutokana na ndimi za moto, ila yeye sio moto au sio mwenye maumbile ya moto. Ni kama sisi tulivyoumbwa kwa udongo (asili yetu ni Aadam aliyeumbwa kwa udongo) ila kwani sisi ni udongo? Maumbile yetu si unaona yalivyo? Kisha tukaumbwa kutokana na maji maji dhalili kabisa, kwani sisi ni maji?

Pili, tukienda kwa akili yako hiyo hiyo kuwa itawezekana vipi Iblisi aungue na moto ilhali kaumbwa na moto. Chukua tu mfano wa binadamu ambaye kaumbwa kwa udongo, lakini udongo huo huo unaweza kutumika kumuadhibu na kumdhuru. Ukichukua dongo gumu lililokomaa ukampiga nalo mwanadamu kichwani litamuumiza bila shaka bali linaweza kumdhuru. Binadamu mpaka wanakufa kwa kuporomokewa na madongo na ilhali wameumbwa kwa udongo. Na pia akaumbwa mwanaadamu kutokana na maji maji, na maji yanaweza kutumika kumdhuru.

Iblisi kaumbwa kwa moto na ataadhibiwa kwa moto wa Jahannam ambao moto mkali mno na haufikiwi na moto wa kawaida. Ukizingatia pia Iblis yeye sio moto (kama binadamu alivyo sio udongo) japo wameumbwa kwa vitu hivyo. Allah ni Muweza juu ya kila kitu.

Na Allah ni Mjuzi zaidi.
 
Swadakta mkuu umesema vyema sana
 
جزاك الله خيرا
 
Yaishe nimekuelewa
Nitabadirika
 
malaika huwa hasemehewi . wewe ungekuwa huli, hunywi,hulali,huchoki,hunahisia za mapenzi,huna haja na hela, huoi, haufi, nk utafanya dhambi gani sasa?
Hapo ukifanya dhambi ni kufuru na ujuaji tu maana vishawishi huna, umesahau pia hawajaumbwa na tamaa.
 
ما شاء الله، جزاك الله خيرا.
لو ما رأيت هذا، لناديتك لتكتب شيئا[emoji16] بس كنت قد عزمت ذلك.
 
و أنتم فجزاكم الله خيرا
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…