Asante studio. Kwa upande wangu nilivyosoma mada na maoni ya watu wengi humu, nimederive kwamba kiburi kinatokea kwenye fullness, completeness, satisfaction.
Mahali popote pale ukiwa juu yani ukiwa nafasi ya juu everywhere iwe kwa sifa za watu ama uwezo ama afya ama uchumi ama elimu ama kipaji..etc ni rahisi sana kupata kiburi. Hivyo independence ama kujiamini na kiburi kuna a very thin line.
Shetani alikataa kusujudu kwa sabbu alijiona tayari yuko level za juu. Wengi wetu kiburi tunakipata kutoka katika ile feeling ya independence. Nesi atakipata kwa sabbu anaona yeye kashazalisha wengi ama kuhudumia wengi na amepata mafanikio..wewe na shida zako leo unamletea afu yuko fresh kiafya, kiuchumi, kielimu, kiakili. Kama ana Roho wa Mungu sawa, lakin kama ndo leader wa kuzimu kashampa cheo chap tu lazima uipate pate. Hasa kama wewe ni level ya chini yake.
Similarly sehemu yoyote ile. Tunakuwa na kiburi kwa sabbu afya, akili, uchumi ,watoto, ndoa, familia ziko vizuri. So unaona ninyenyekee ili iweje?Niwe mpole ili nini labda? Nimsaidie kisa nini? Sisemi kwamba its always kiburi maana kuna muda tunahitaji mipaka baina yetu na watu lakini mipaka inapokuwa mikubwa hugeuka kuwa kiburi hasa kama unamuwekea muumba wako akupaye uzima mipaka na kutotaka kujishusha.
Na kiburi mara nyingi huondoka kwa kuserve wengine. Popote pale ukitaka uwe na mafanikio lakin usiwe na kiburi give out. Iwe ni muda wako, kipaji chako, sadaka, nguvu zako, kushiriki na wenzako katika mambo mbalimbali. Na zaidi ibada ya kweli kutoka moyoni. Itakusaidia sana kuweza kukishinda kiburi. Nimejaribu kuandika kwa mtazamo wangu, am open to more info..