Nilikuwa busy kiasi halafu usiwazungumzie wanachuoni wetu kama wanafunzi fulani wa day care, hao ni watu waheshimiwa na warithi wa mitume kwasababu mitume hawajarithisha dirham wala dinar bali wamerithisha elimu, na wapokezi wa hiyo elimu ni wanawachuoni wabobezi kwenye elimu hata allah جلّ و على akauunganisha ushahidi wake na wa malaika na wanawachuoni kuonesha hadhi yao na nafasi mbele zake.
"Ameshuhudia allah ya kwamba hapana muabudiwa wa haki isipokuwa yeye tu, na malaika na wenye elimu {nao wanashuhudia hilo}, hali ya kuwa yeye ni mwenye kusimamia uadilifu, hapana muabudiwa wa haki isipokuwa yeye mwenye nguvu na mwenye hekma.."
Qur'an 3:18
Kwa kukuweka sawa kuna madh-hab nne mbele ya ahlu sunnah nayo ni madh-hab ya imaam abuu hanifa, imaam maalik, imaam shafiiy na imam ahmad allah awarehemu wote, hawa wametofautiana katika mambo ya kifiqhi tu na wala hawajatofautiana katika itikadi, so ukitoa mifano ya mwezi na swala ya idi au mwezi wa kitaifa na kimataifa watakucheka watu wenye maarifa siku nyingine usirudie.
Tukirudi kwa ibliys alielaaniwa zimetujia khabari kwa wingi kwenye quran juu ya uovu wake na azma yake ya kuwapoteza wana wa aadam mpaka siku itakapofika ajali yake, wala hakuna faida kujua alikuwa muovu kabla ya kuamrishwa kusujudu kwani hilo halibadili chochote.