Baada ya kumaliza chuo tu.
01.Kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni receptionist Zanzibar.
Niliacha kwasababu niliona ni kazi ya kunyenyekea sana watu, ukiona mzugu umpokee umchekee upokee mabegi meno nje kifupi kazi ya kunyenyekea mtu siwezi hasa hawa wazungu wa hotelini(nikaacha kazi)miezi miwili
02.kazi ya pili, nilikuwa mkufunzi chuo cha maendeleo ya jamii(private) hapa niliacha kwa sababu mbili
Moja mshahara laki mbili hakuna mkataba
Mbili wanafunzi wana sauti kuzidi mwalimu Yani chuo kinasikiliza wanafunzi sana kuliko waalimu ulifelisha msala,pia chuo kipo kijijini ambapo nimezaliwa kujuana kwingi nikaacha kazi nilikaa miezi Tisa
Kazi ya tatu, ni afisa masoko natembea mikoa mbalimbali kuuza bidhaa X
Kwanini nataka kuacha?
01.nataka kutafuta fani mana nina amini maisha bila fani huwezi kufanikiwa(kuweka degree pembeni.)
Naona umri unaenda mshahara mdogo.
03.Boss anatabia ya kufukuza wafanyakazi wapo wengi wazuri zaidi yangu walifukuzwa(mimi nafuata)
Boss pia hayuko serious na kazi anaendeshwa na hisia
Ila kubwa kabisa nataka kutafuta fani au ujuzi sio kuajiliwa.
Kazi ingine niliacha ni udereva Bajaj, kwanini? Huwezi kujenga future kwa Bajaj,kutunza pesa ni ngumu, risk kubwa sana barabara ukizingatia sikuwa na ndugu yoyote Dar.
Nikaacha
Je kwa tabia hizi nina matatizo au nipo sahihi
Naomba ushauri