Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kuna watu huwa waanamini maisha ya vijijini ni mepesi na bora kuliko mjini, sijui hizi fikra zinatokana na nini ila kwa ukweli ukiacha vijiji vichache vya mikoa kama ya Kilimanjaro, Njombe, Mbeya labda na vya mikoa mingine michache maisha kwa ujumla wake vijijini ni magumu sana kuliko mjini.
Umaskini wa mahitaji ya msingi ya kibinadmu ulioko vijijini ni mkubwa sana na wa kutisha kuliko mjini na hapo bado hatujaongelea huduma mbovu za kijamii na miundombinu kama hospitali, maji, barabara na umeme. Kuna vijiji unakuta watu wanatumia maji ya dimbwi kwa pamoja na wanyama na hapo hapo wanafulia na kufanyia shughuli nyingine. Kijijini unaweza kukuta mifugo mingi ila nyama kuliwa ni kwa manati.