Kwa Tanzania maisha ya kijijini ni magumu zaidi kuliko mjini kwa ujumla

Kuna Kijiji tulienda singida manyon alahaula!!!! Watu wanaishi maisha magumu kupitiliza hebu fikiria tunafika stand konda anatuuliza vipi mnapenda huko mbona hamjabeba maji
Maji tuliyoyakuta et tunawapisha ng'ombe wanywe ndo sisi tuchote tukatumie eeeh nikaapa sitorud Tena kule
 
Kwahiyo kama ungekua umeajiriwa je?
Kwani uko maji ya kisima hakuna?
 
Hapo kwenye mifugo mingi lakini nyama kuliwa kwa manati ni ukweli mtupu, kuna kijiji nilienda aise mifugo kama yote lakini nyama hamna kabisa labda mfugo upate ajali na wenyewe usipowahi huambulii kitu
Sasa mkuu labda wateja hakuna ndiyo maana hakuna nyama zinazo uzwa lakini sehemu kama hizi utakuta kwenye familia nyama wanakula tena zinakua za wanyamapori, kwasababu Mfugaji kuchinja Ng'ombe wake kwaajili ya kula nyumbani ni ngumu. Wewe na mke wako na watoto 3 unaweza kuchinja Ng'ombe kwaajili ya mboga?
 
Kuna mtu hajui zaidi ya hapo ,so sio lazima wote wanataka maisha fulani ...Bado unaaminisha kutumia elfu saba kwa siku ni umaskini, wazungu wajanja sana.
Wazungu siyo wajanja wao maisha yao na sisi ni tofauti wao wanachojua bila pesa hakuna kupata huduma ya chakula na maji na hospitali, walitakiwa wajue siyo kila jamii inatumia pesa kila siku kupata chakula, kuna familia Asubuhi Mama anazunguka nyuma ya nyumba achimba viazi vya kula Asubuhi na mchana anakimbizwa kuku anachinjwa na jioni anachuma mate mbele siku imeisha na stoo kuna kunia za mahindi na mpunga unga ukiisha wanaenda kusaga mahindi.
 
Ndugu hayo maji ya kisima yangekuwepo tungengoja ng'ombe wanywe? Usafiri Hadi jmosi labda uwe na boda wako wa kutoka center aje akufate lasvo ngoja jmosi noha ije Iwabebe kuwapeleka centre
Mgeishi tu mambo mazuri yanakuja taratibu sehemu yoyote bila mungiliano na wageni mambo yanakua magumu, Sehemu yoyote bila kuwa na mzunguko wa pesa hiyo sehemu kuchangamka ni ngumu, ni sawa na Kizimkazi kule baada ya miaka 10 kutapooza, Kijijin kinachangamka kwa Mzunguko wapesa na siyo kwa kujenga maghorofa na majumba na wenye majumba wanaishi mijini na shuguli zao za kiuchumi zipo mjini.
 
Ni kweli, maisha ya kijijini si kama ya mjini. Ila ngoja nikuambia kuhusu vijiji vya kilimanjaro naona hujawahi kufika ukanda wa moshi chini nyanda za tambarare kata za kahe na arusha chini/tpc. Kuna vijiji kule utadhani havipo moshi labda vipo simanjiro manyara kumbe vipo mkoani kilimanjaro. Kule chini hali ni mbaya si kama uchagani milimani. Vijiji vya milimani vimechangamka, kuna miundombinu mizuri tangu zamani. Vijiji vya chini kule TPC nyumba za bati tu ni za kuhesabu, usafiri ni wa kubangaiza na kuungaunga
 
Kuna Kijiji tulienda singida manyon alahaula!!!! Watu wanaishi maisha magumu kupitiliza hebu fikiria tunafika stand konda anatuuliza vipi mnapenda huko mbona hamjabeba maji
Maji tuliyoyakuta et tunawapisha ng'ombe wanywe ndo sisi tuchote tukatumie eeeh nikaapa sitorud Tena kule
Oaaaa ni nomaa aseee kuna vijiji wanakunywa maji pamoja na ng'ombe had na mbwa kisima kimoja ,koo maisha ya vijijn ni magumu baraha
 
Kuna watu huwa waanamini maisha ya vijijini ni mepesi na bora kuliko mjini, sijui hizi fikra zinatokana na nini ila kwa ukweli ukiacha vijiji vichache vya mikoa kama ya Kilimanjaro, Njombe, Mbeya labda na vya mikoa mingine michache maisha kwa ujumla wake vijijini ni magumu sana kuliko mjini.

Umaskini wa mahitaji ya msingi ya kibinadmu ulioko vijijini ni mkubwa sana na wa kutisha kuliko mjini na hapo bado hatujaongelea huduma mbovu za kijamii na miundombinu kama hospitali, maji, barabara na umeme. Kuna vijiji unakuta watu wanatumia maji ya dimbwi kwa pamoja na wanyama na hapo hapo wanafulia na kufanyia shughuli nyingine. Kijijini unaweza kukuta mifugo mingi ila nyama kuliwa ni kwa manati.
Mkuu vijijini hata chakula ni shida kubwa sana. Yaani hadi unashangaa sijui tulilogwa.

Bei za Nyama ni kubwa sana kuliko mjini.

Ukiongelea Manufactured products ndio balaa.

Mimi ntaendelea kuhangaika na jua la mjini.

Kingine kijijini hata ukiwa na hela unakuta umapauka sana.
 
Nakubaliana na wewe Kwa 7% tu

Mkuu ukweli ni kwamba vijiji vingi havina huduma za kijamii kama maji,barabara umeme na hospital zipo mbali pamoja na shule hii ni kweli kabisa.

Napingana nawewe Kwa kusema maisha ni magumu. Hii siyo kweli.

Kila mtu huishi kulingana na manzigira mkuu chukulia sisi kipindi tunachunga huko kijijini maji anayokunywa ng'ombe ndo maji ninayo kunywa Mimi na siwazi kitu na Wala siugui kumaliza miaka3 sijawahi kukanyaga hospital ni kawaida.

Kijijini wanaishi maisha Yao ukikuta Kijijin kwenye familia hakuna hata kuku huo mji ni WA mjinga ASIYE jielewa.

Kuna baadhi ya miji maji hufika Hadi 1000 Kwa dumu kubwa lita20 Wakati kijijini ukiamua kuishi maisha Bora inawezekana Kwa kuchemsha maji ya kunywa ambapo Huwa ni meupe kama mvua japo si salama.

Upande wa chakula huwezi linganisha na mjini hata siku Moja

Mfano kijijn ni ngumu sana kwenda kununua mboga za majani gengeni basi utakuwa mvivu wa kutupwa!!

Ulaji wa nyama ni kweli hawali labda itokee sikukuu au wageni Kwa jirani.

Lakini hukohuko Huwa wanakula nyamafu ikitokea Kwa jirani amekufa mnyama hupeana Bure.

Hata Huko mjini ulaji wa nyama watu hutoboa hadi wiki2 hajala nyama.

Maisha yangu Kwa % nimeishi kijijini hakuna kitu na miss kama maisha hayo hayana ugumu kabisa na watu wamelemaa Kwa mseleleko wa maisha.

Kijijini kula mboga isiyo ungwa siyo kwamba ni mateso ni kitu walichozoea mara nyingi huweka karanga au maziwa ukikuta ni wafugaji!!

Vitu pekee vinaleta ugumu ni miundo mbinu na mahitaji ya muhimu kama nilivyotaja huko juu

Kifupi tunaishi kulingana na mazingira mkuu
 
Kuna watu huwa waanamini maisha ya vijijini ni mepesi na bora kuliko mjini, sijui hizi fikra zinatokana na nini ila kwa ukweli ukiacha vijiji vichache vya mikoa kama ya Kilimanjaro, Njombe, Mbeya labda na vya mikoa mingine michache maisha kwa ujumla wake vijijini ni magumu sana kuliko mjini.

Umaskini wa mahitaji ya msingi ya kibinadmu ulioko vijijini ni mkubwa sana na wa kutisha kuliko mjini na hapo bado hatujaongelea huduma mbovu za kijamii na miundombinu kama hospitali, maji, barabara na umeme. Kuna vijiji unakuta watu wanatumia maji ya dimbwi kwa pamoja na wanyama na hapo hapo wanafulia na kufanyia shughuli nyingine. Kijijini unaweza kukuta mifugo mingi ila nyama kuliwa ni kwa manati.
Ulivyoandika tu vijiji vya Kilimanjaro, Njombe na Mbeya nimeacha kusoma maana unaandika mambo ya kufikirika. Huko Kilimanjaro ht hujawahi fika, Kilimanjaro maisha yangekuwa marahisi wachaga wanazurura kutafuta nini mikoa ya watu? Hakuna mkoa mgumu hasa uchagani kuishi kijijini km Kilimanjaro. Njombe na Mbeya ipi unazizungumzia? Uzi wako wote umekosa hoja ni porojo tu.
 
Kuna vijiji hakuna huduma yeyote vumbi limetanda hewani siku nzima halishuki chini!!
Hakuna maji
Hakuna umeme
Hapalimwi chochote
Hakuna hospital
Hakuna barabara
Soko kilometers 20
Skul kilometers 10
Huko ni mbali kiasi kwamba hata mvua haifiki
Hv we unaota au umechanganyikiwa? Ulizaliwa na kukulia wapi? Yaani kufika tu mjini ndio umeanza kutukana hivyo? Kiufupi huna akili.
 
Kuna Kijiji tulienda singida manyon alahaula!!!! Watu wanaishi maisha magumu kupitiliza hebu fikiria tunafika stand konda anatuuliza vipi mnapenda huko mbona hamjabeba maji
Maji tuliyoyakuta et tunawapisha ng'ombe wanywe ndo sisi tuchote tukatumie eeeh nikaapa sitorud Tena kule
Na hiyo Manyoni ndio wilaya mojawapo yenye afadhali Singida sasa!
 
Nakubaliana na wewe Kwa 7% tu

Mkuu ukweli ni kwamba vijiji vingi havina huduma za kijamii kama maji,barabara umeme na hospital zipo mbali pamoja na shule hii ni kweli kabisa.

Napingana nawewe Kwa kusema maisha ni magumu. Hii siyo kweli.

Kila mtu huishi kulingana na manzigira mkuu chukulia sisi kipindi tunachunga huko kijijini maji anayokunywa ng'ombe ndo maji ninayo kunywa Mimi na siwazi kitu na Wala siugui kumaliza miaka3 sijawahi kukanyaga hospital ni kawaida.

Kijijini wanaishi maisha Yao ukikuta Kijijin kwenye familia hakuna hata kuku huo mji ni WA mjinga ASIYE jielewa.

Kuna baadhi ya miji maji hufika Hadi 1000 Kwa dumu kubwa lita20 Wakati kijijini ukiamua kuishi maisha Bora inawezekana Kwa kuchemsha maji ya kunywa ambapo Huwa ni meupe kama mvua japo si salama.

Upande wa chakula huwezi linganisha na mjini hata siku Moja

Mfano kijijn ni ngumu sana kwenda kununua mboga za majani gengeni basi utakuwa mvivu wa kutupwa!!

Ulaji wa nyama ni kweli hawali labda itokee sikukuu au wageni Kwa jirani.

Lakini hukohuko Huwa wanakula nyamafu ikitokea Kwa jirani amekufa mnyama hupeana Bure.

Hata Huko mjini ulaji wa nyama watu hutoboa hadi wiki2 hajala nyama.

Maisha yangu Kwa % nimeishi kijijini hakuna kitu na miss kama maisha hayo hayana ugumu kabisa na watu wamelemaa Kwa mseleleko wa maisha.

Kijijini kula mboga isiyo ungwa siyo kwamba ni mateso ni kitu walichozoea mara nyingi huweka karanga au maziwa ukikuta ni wafugaji!!

Vitu pekee vinaleta ugumu ni miundo mbinu na mahitaji ya muhimu kama nilivyotaja huko juu

Kifupi tunaishi kulingana na mazingira mkuu
Vijiji vingi tu familia hazifugi kuku wala hazilimi mboga za majani, kama hujui Tanzania utapiamlo na udumavu uko vijijini zaidi kuliko mijini.
 
Kuna watu huwa waanamini maisha ya vijijini ni mepesi na bora kuliko mjini, sijui hizi fikra zinatokana na nini ila kwa ukweli ukiacha vijiji vichache vya mikoa kama ya Kilimanjaro, Njombe, Mbeya labda na vya mikoa mingine michache maisha kwa ujumla wake vijijini ni magumu sana kuliko mjini.

Umaskini wa mahitaji ya msingi ya kibinadmu ulioko vijijini ni mkubwa sana na wa kutisha kuliko mjini na hapo bado hatujaongelea huduma mbovu za kijamii na miundombinu kama hospitali, maji, barabara na umeme. Kuna vijiji unakuta watu wanatumia maji ya dimbwi kwa pamoja na wanyama na hapo hapo wanafulia na kufanyia shughuli nyingine. Kijijini unaweza kukuta mifugo mingi ila nyama kuliwa ni kwa manati.
Nyama mpaka christmas au idd na pasaka nk
 
Kuna Kijiji tulienda singida manyon alahaula!!!! Watu wanaishi maisha magumu kupitiliza hebu fikiria tunafika stand konda anatuuliza vipi mnapenda huko mbona hamjabeba maji
Maji tuliyoyakuta et tunawapisha ng'ombe wanywe ndo sisi tuchote tukatumie eeeh nikaapa sitorud Tena kule
Ajabu mbunge wao utamsikia mama hatukudai aiseee
 
Hv we unaota au umechanganyikiwa? Ulizaliwa na kukulia wapi? Yaani kufika tu mjini ndio umeanza kutukana hivyo? Kiufupi huna akili.
Kuna tusi wapi au unawashwa pahala, kusema kuna vijiji havina huduma ni tusi??? Punguzeni uchawa pelekeni huduma nzuri vijijini!

Usikariri kuwa kila mtanganyika ni lazma azaliwe kijijini, punguza mafuta kichwani!!
 
Sasa mkuu labda wateja hakuna ndiyo maana hakuna nyama zinazo uzwa lakini sehemu kama hizi utakuta kwenye familia nyama wanakula tena zinakua za wanyamapori, kwasababu Mfugaji kuchinja Ng'ombe wake kwaajili ya kula nyumbani ni ngumu. Wewe na mke wako na watoto 3 unaweza kuchinja Ng'ombe kwaajili ya mboga?
HApo wanaofuga kuku ndio huchinja sana sema vijijini kula kuku sio ajabu sana na huwa wana winda pia
 
Back
Top Bottom