Kwa Tukio lililomtokea Mama yangu 2009, Nimetokea kuuheshimu sana Ukristo na Wakristo wote

Kwa Tukio lililomtokea Mama yangu 2009, Nimetokea kuuheshimu sana Ukristo na Wakristo wote

Jibu swali acha kurukaruka kama maharage.
MUNGU HAWEZI KUFANYA AMBACHO MTOA MADA AMEANDIKA?
mi ni muumini wa YESU KRISTO sio wa mwamposa kwanza simfagilii kiviile lkn hata ingekua kweli haimuusu mtu.

Kama wewe unae mungu wako basi acha kuponda Mungu wa wenzio. Pita zako hivi uende kwenye majukwaa ya waabudu mizimu wenzio kimyakimya.
Mungu yuko mmoja tu aliyehai. Hao manabii wenu ni matapeli tu. Najuwa huwezi kukubali wala kuelewa umekwishatekwa vibaya
 
Ila imani ni kitu cha msingi sana haijalishi kama ni muislam au mkristo, msingi wa maisha ni kuamini.
 
Bro inaonekana kichwa yako ina shida. Sasa unachopenda ni nini? Watu kuponywa na nguvu za Mungu au huo uchawi wa kinaijeria unaouona una nguvu? Kwahiyo Mungu ashindwe kuponya ila uchawi wa kinaijeria uponyaji? Nashauri, sio kila thread unatakiwa ucomment. Nyingine pita pembeni kwani unazidi onyesha uchi wa akili yako.

Kuhusu wagonjwa Ocean Road na Muhimbili, toka enzi za Adam hadi wakati wa Yesu na Mitume Magonjwa yalikuwepo na Mahospitali na matabibu walikuwepo mbona hawakuzunguka huko Mahospitalini? Ebu acha ujuaji, issue zingine ziache zikupite tu mkuu.
Mnatapeliwa tu ila hamna mtu anaponywa kwenye hayo makongamano yenu.
 
Ni meishia kusoma pale nilivo ona kwamba ulipeleke maombini, ni ka kuona kijana mpuuzi, ingekua hivo hata kwenye theater za hospitali kungekua na maombezi tu,........mtoto wakiume anae amini maombezi ya walokole ana vyashilia vya jinsia ya kike. "Soul diseases are treated spiritually and physical diseases are treated biologically" don't mixup things plz nyie walokole mna kua na wrong absolute belief kitu ambacho ni hatari katika jamii zetu za kiafrica
Hamnaga maombezi hapo hao matapeli tu.
 
Sasa ninyi kama Familia nzima mnatafakari nini juu ya huyu Yesu KRISTO?
Kumbuka siku ya Hukumu ataidai familia huu muujiza aliofanya lakini hamkuamini na kumpokea kama BWANA na Mwokozi wenu,(Warumi2:4-6)
 
Nakumbuka kuna mtoto mmoja wa shemeji yangu alizaliwa na spinal bifida/mgongo wazi alikuja tokea lushoto akawa anatibiwa operation muhimbili, sasa nahisi alikua na matatizo mengine pia. Sasa ikawa utaratibu wangu kuwa namwombea.

Aiseeh kuna siku nilimwombea na niliona kabisa nguvu za Mungu zimeshuka niliyaombea maji roho ya Mungu na damu ya Yesu zikatua kwenye maji niliona nguvu kabisa na nilivomaliza nikamnawisha yale maji usoni na kichwani na mtoto akalala usingizi mzito pale pale dk 0 nikajua nguvu ya Mungu inafanya marekebisho kwenye mwili wake maana hata mwili wa mtoto ulikua unajaa kama puto na macho yalianza kubadilika rangi na masikini nilikua nikikabeba kananiangalia sana sana kwa huruma..kumbe kalikua kanaona msaada wa Mungu utapitia kwangu.

Baada ya kupata usingizi mzito mara tu baada ya maombi yale. Ndani ya wiki mtoto alianza kubadilika na kuchangamka akarudi hali ya kawaida.
Sasa yule binti kuna siku alienda kwa mganga huko kijini kwao sasa alipofika pale akaambiwa huyu mtoto Kuna mtu alimwombea na nguvu za Mungu zilimwokoa na huyo mtu ana nguvu za Mungu.mshukuru sana aliyemwombea aliokoa maisha ya mwanao.

Nguvu za Mungu Zipo! Usibeze Imani wala dini ya mtu. Hukumu ina Mungu mwenyewe.
 
Ndio adanganye kwamba alikuwa muislamu [emoji28][emoji28][emoji28]uongo mbaya pale kwa Mwamposa wote wanasema ni waislamu.!!
waislam pia wana matatizo kijana,ni miongoni mwa raia 60mln wa tz,wanakula ugari na dagaa kama wakristo.

kwani familia ngapi zina mseto wa dini mpaka wewe umkatalie mletamada utadhani hakuna kitu cha namn hiyo???

halafu ulivyo wa ajabu jamaa hajasema kabadili dini,si yeye,nduguze wala baba yake,amesisitiza tu kuwaheshimu wakristo.unaumia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa ninyi kama Familia nzima mnatafakari nini juu ya huyu Yesu KRISTO?
Kumbuka siku ya Hukumu ataidai familia huu muujiza aliofanya lakini hamkuamini na kumpokea kama BWANA na Mwokozi wenu,(Warumi2:4-6)

Mathayo 7:21-29​

21. “Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.

22. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’.

23. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’
 
Ukimtukana mtu kafiri unatakiwa ujue kuwa hakuna mwislam aliyekufa akarudi kukupa taarifa kuwa huko peponi wapo watu wa aina gani ukishalijua hilo basi heshimu sana imani za wengine Maisha baada ya kifo ni Siri kubwa na mitihani ya maisha ndio inatufanya tujue ukweli hukusu hzi Din
Barikiwa sana sana Dogo. Mungu ni wa kwetu sote, MUNGU hana dini, ni wa kwetu sote. aione FaizaFoxy kwa file
 

Mathayo 7:21-29​

21. “Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.

22. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’.

23. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’
Mbona hilo andiko halihusiani na andiko nililtoa hapo kwenye maelezo ya ushuhuda? Harafu '' SI KILA aniambiaye" hakuwa na maana kuwa "WOTE waniambiao Bwana Bwana" hawataingia katika ufalme wa mbinguni!
Ndiyo kusema WAPO WANIAMBIAO Bwana,Bwana WATAINGIA KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
Lakini fahamu kwa Wema aliowatendea Mungu katika familia kwa kumponya huyo mama,kama hamtatubu dhambi kwa jina la Yesu,Mungu atawadai siku ile ya Hukumu,(Warumi2:4-6)
 
Back
Top Bottom