Kwa tulipofikia mikutano ya siasa kwa nchi yetu haina tija zaidi ya kucharuana tu! Pigeni marufuku hii mikutano uchwara!

Kile kilikuwa chuma na nchi ilitulia
 
Wasiipige mikutano marufuku. Acha mvua inyeshe ili 2025 tujue panapovuja ni wapi i.e. tujue pumba ni akina nani na mchele ni nani
Ingekuwa ni hivyo uchaguzi wa 2015 ndio ulikuwa wao lakini walichemka
 
Mungu anaenda kukufuta ndani ya uso Dunia , tunza hii, hii nchi sio ya baba au mama yako, kiapo ni kiapo iwe kwa miungu ,Mungu , au makabaliano yoyote katika nchi mfano katiba ,

Mungu hawezi ruhusu mtu mjinga kati ya nyoyo 60ml kuangamiza Taifa lake , tunza hii
 
Hiki ulichokiandika ndo kinapaswa kupigwa marufuku na kukemewa na wote wenye akili timamu, wapenda amani, haki, wajibu na maendeleo.
 
Kile kilikuwa chuma na nchi ilitulia
Huwezi kusema nchi ilitulia wakati watu walikuwa wanauliwa na kutupwa baharini wakiwa ndani ya viroba, wabunge walikuwa wanapigwa risasi bungeni na wafanyabiashara walikuwa wananyang'anywa fedha zao.

Huwezi kusema kile kilikuwa chuma wakati alikufa kwa mafua ya corona. Ile ilikuwa ni walking carcass tu
 
Tatizo ni wewe hujui Siasa! Hiyo ndio Siasa Kaka. Ulitegemea siasa iwe Sawa na lecture room,ulitaka siasa iwe Sawa na semina? Hiyo ndio Siasa..unasema hili,mwenzio anakuja kusema lile ulilosema kwa namna nyingine ...wananchi wanaachiwa jukumu la kutafsiri.
Nakuhakikishia kwamba kama siasa zilivyokua zinakwenda wakati wa Jakaya zingeendelezwa na JPM nchi yetu isingekua hapa ilipo leo.
 
Mfano wa mambo matatu yenye kwako ambayo ungependa yazungumziwe na vyama vya siasa ni yapi??
Alitegemea kusikia neno anaupiga mwingi kalikosa kila mkutano ni spana tupu, mbaya zaidi watu wanalipa nauli zao bila kusombwa hili jambo limemkwaza sana mwananzengo.
 
Hata kama kusingelikuwa na mikutano ila bandari zetu zisingeliuzwa na hazitauzwa
 
Badili katiba. Unaogopa nn mikutano? Au we Ni wale wa mchongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…