Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Tambua kwamba kazi nyingi za kuwatetea waathirika mbalimbali, Lissu amezifanya bure bila kilipwa na hao watu.
Lissu anasema;
Sasa leo nataka nizungumze kuhusu mchango wangu wa kupigania haki za binadamu nchini Tanzania.
Ushahidi wa leo utasema ni kwanini nashitakiwa. Leo nashitakiwa kwa sababu ya msimamo wangu
Ni 'Political Prosecution' kwa sababu ya msimamo wangu katika kupigania haki na utawala bora. Siyo kwa sababu mimi ni Muhaini bali ni kwa sababu ya kazi niliyo ifanya na naendelea kuifanya
Sasa kwa kuanzia Waheshimiwa Majaji naomba niseme kwamba, nimetumia maisha yangu karibu yote ya utu uzima kupigania haki za watu. "Struggle for human rights and Struggle for democracy".
Sikuanza Juzi. Sikuanza tarehe 3 April Mwaka Jana. Waheshimiwa Majaji nilianza nikiwa Sekondari. Mwaka 1988 karibu nifukuzwe shule kwa sababu ya Kutetea Wanafunzi waliokuwa form 4 na mimi niko form 6
Na Majaji katika Mahakama ya rufaa na Mahakama kuu hii kuna Majaji niliosoma nao wanafahamu hili ila sito wataja. Niliponea chuchupu kufukuzwa shule,nilianzia huko.
Mwaka 1990 niliwa Jeshini ,tulikuwa tunaenda Jeshini, siku hizi sijui kama watu Wanaenda Jeshini. Tukiwa Jeshini Mwaka 1990 mjadala wa Vyama vingi ukaanza. Waheshimiwa Majaji Majeshi yetu haya Polisi,JWTZ na Usalama wa Taifa hawa Wote hawa walikuwa CCM. Na nina amini bado ni CCM, bado hawaja komboka.
Wote hawa ulikuwa uingii Jeshini kama huna kadi ya CCM.
Mjadala ulipoanza ukawa hapana Vyama vingi. Na mimi nilikuwa Service man kikosi namba 841 Itende, Mbeya. Niligombana na Majenerali wale waliokuwa hawataki vyama vingi na wengine waliokuwa Mapolisi wakina Mahita.
Niliwaambia kuwa kauli ya Mwalimu Nyerere kwamba wanaopinga Vyama vingi ni Wajinga nyie Majenerali hamjaisikia tena nikiwa ni Service man.
Nikagombana nao sana.
Rais Ally Hasssan Mwinyi alipoteua tume ya mfumo vya chama kimoja au vyama vingi vya siasa nchini Tanzania, inaitwa tume ya Nyarali kwa sababu Jaji Mkuu Francis Nyarali alikuwa Mwenyekiti wake. Tume iliundwa mwaka 1991 ilikuwa inahoji watu na mimi nilikuwa mmoja ya watu waliohojiwa
Nilikuwa ni mmoja ya watu waliotoa ushuhuda mbele ya Profesa Haroub Othuman ambaye alikuwa Mwanazuoni maarufu.
Secretary wa tume alikuwa baadae jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania January Msofe.
Kwa hiyo nimepigania mfumo wa mabadiliko kwa namna hiyo. Kwa kwenda mbele ya tume ya Rais kutoa ushuhuda.
Na mwaka 1992 niliacha kusoma chuo Nchini Uingereza nikaja kugombea kwa sababu siku zote nimekuwa 'Concerned' na maswala ya ustawi wa nchi hii.
Waheshimiwa Majaji kwa miaka yote iliyofuata mpaka leo nimepigania demokrasia ,katiba mpya, mfumo huru wa haki na uchaguzi
Sijawahi Kupumzika.
Nje ya Kupigania demokrasia Waheshimiwa Majaji nimepigania haki za Wananchi wa kawaida. Waheshimiwa Majaji mwaka 1997 serikali ya Rais Mkapa iligawa eneo karibu lote la Delta ya Mto Rufiji kwa Mwekezaji mmoja wa Ki IRISH ili alime kamba (Prons), wale wadudu wa baharini watamu watamu, enheeeee 'Kamba'.
Kamba ni Wadudu wa baharini lakini wanafugwa.
Waheshimiwa Majaji najua mmesoma kesi ya Reganald alikuwa anauzia nchi vifaa vya kijeshi chakavu. Sasa Mkapa na serikali yake wakampatia hekta elfu 20 ya Delta ya Rufiji ili afuge Kamba.
Kama hilo lingefanikiwa pasingekuwa na msitu wa Mikoko katika ile Rufiji tunayoiona leo.
Na kwa tafiti za kitaalamu ingedhuru maisha ya Watu laki moja.
Mimi pamoja na Wenzangu akiwemo Dr.Nshala, hawa ni Mashujaa mnatakiwa muwajue. Mimi na wenzangu tulisakamwa sana na serikali ya Mkapa na Mkapa mwenyewe na makamu wake Dr.Ali Juma.
Tukaitwa Wajahidini wa Kimazimgira.
Tukamkimbiza tule Mu- IRISH, tukaokoa msitu wa Mikoko wa Delta ya Rufiji
Hiyo ilikuwa 1997 na 1998.
Waheshimiwa Majaji siyo Rufiji tu, nimekuwa mstari wa mbele kupigania haki za ardhi za Wafugaji na Wananchi wanaoishi katika hifadhi za Wanyamapori kama Ngorongoro, Loliondo,Tarime, Meatu, Bariadi Mashariki, Maswa Mashariki na ukanda wote wa Mashariki ya Serengeti.
Mwaka 2023 nilikamatwa Karatu nikizuiwa nisiende Ngorongoro kuwaona Wamasai niliokuwa nawapigania tamgu Mwaka 1996.
Nimepigania Haki za Wananchi wa maeneo ya ukanda wa mashariki wa Ziwa Tanganyika kama Nkasi na ukanda wa Pwani wa Mkoa wa Kigoma
Maeneo ya Wavuvi wa Ukanda wote wa Ziwa Victoria kutoka ukanda wa ziwa Magaharibi mpaka wa Uganda pamekuwa na ukiukwaji wa kutisha wa haki za raia. Watu wanauwawa na vyombo vya Ulinzi, inatisha sana.
Lakini Waheshimiwa Majaji kipekee kabisa najulikana ndani na nje ya Nchi kwa kupigania maeneo yenye madini kama dhahabu. Kwa takribani miaka 10 kuanzia mwaka 1996, mimi ndiye niliyekuwa nazungumzia maswala ya madini katika nchi hii.
Maeneo ambayo serikali ya Mkapa iliwapa wawekezaji kutoka nje, Geita Gold Mining, maelfu ya Wananchi waliondolewa kwa nguvu. Nilikwepo wakati wanaondolewa.
Bulyang'ulu, August mwaka 2002 nilikwepo wakati panatokea mauaji wakati serikali ya Mkapa inawaondoa Wananchi kuwapa Wakanada. Ndo nikapata kesi ya kwanza ya jinai mwaka 2002.
Nilipigania kufanya kampeni ya kudai uchunguzi huru wa Kimataifa ya mauaji ya Wananchi wa Tanzania nchini Tanzania, Marekani na Canada, 'everywhere' na nikapata na kesi ya Jinai.
Eneo la Dusu, Nzega palikuwa na mgodi unaitwa Golden prime Mining wa Australia.Mimi nilikwepo kupinga hilo. Tarime, Nyamongo pia na Waheshimiwa Majaji Tarime ni Muhimu sana kwangu siyo kwa Sababu ni Ukweni, bali kwa miaka 3 niliwatoa watu 466 gerezani kutoka gereza la wilaya Tarime na gereza la Butimba Mwanza.
Watu walifungwa bure kwa makosa ya uongo kabisa ili wafungwe watu wapore ardhi yao. Niliwatoa watu 466 akiwemo Marehemu Chacha Wangwe ambaye baadae akaja kuwa Mbunge.
Tarime ikanipa kesi ya Jinai pia, wakati wa serikali ya Jakaya Kikwete. Baadae nitaeleza kuhusu hizi kesi.
Waheshimiwa Majaji, Buhemba ambayo sasa ni Wilaya ya Kahama, na Butiama, na Mererani wilaya ya Simanjiro, na Manyoni, na Ikungi Mashariki jimboni kwangu. Kote huko 'paligundulika' kuwa na Dhahabu ikaja kuwa ni maafa kwa Wananchi waliopelekewa hizo mali (na Mungu).
Kila mara panapokuwa na ukandamizaji wa haki za Wananchi nimejitahidi kuwa sehemu ya Mapambano ya Wananchi hao ya kupinga huo ukandamizaji.
Kauli mbiu yangu, Waheshimiwa Majaji (My moto) "Upinzani dhidi ya Ukandamizaji ni utiifu kwa Mungu" (Resistance to Oppression is obedience to God)
Msimamo wa maisha yangu haya umekuwa na gharama kubwa sana kwangu.
Origin Boniface Jacob
Edited by Christopher Cyrilo