Kwa ulimwengu huu wa sasa Fani ya Procurement bado inafundishwa vyuoni kwa sababu gani?

Kama mtu anaweza akajiajiri katika fani ambayo hajasomea, kwanini tunapoteza muda huko vyuoni?
Unapoteza muda vipi? Nchi lazima iwe na wataalamu wa fani zote, unajua sisi wa Africa kutokana na ugumu wa maisha tunaamini elimu ni ajira, lengo la elimu ni kutengeneza wataalamu
 
Unapoteza muda vipi? Nchi lazima iwe na wataalamu wa fani zote, unajua sisi wa Africa kutokana na ugumu wa maisha tunaamini elimu ni ajira, lengo la elimu ni kutengeneza wataalamu
Hahahaaaaaa, mkuu, sasa mtaalam wa Petroleum Engineering anaendesha Bajaj kijiwe kimoja na yule wa kidato cha sita, huyo mtaalam ana faida gani kwa taifa?
 
Mkuu, huyo jamaa inaonekana ni mnufaika wa hizi corrupt systems za Afrika. We seriously need to change.
Tukizungumzia uhalisia wa mambo hasa sekta ya taaluma, bado tunachanga moto kubwa mnoo. Course nyingi zinaanzishwa kwetu lakini hazitumiki ipasavyo.
Ukisoma vitabu vya accounting vya wenzetu wa magharibi, utaona katika idara ya fedha kuna finance director, chini wapo accountant and tax personnel. Hizo course zote tumeletewa kwetu, applicability yake ndo kizungumkuti, makampuni mengi hayana tax department, majukum ya kikodi hufanywa na mhasibu. Hawa maelfu wanaosoma kodi wanaishia kufanya related task au kujikuta nje ya mfumo. Japo ni nje ya mada, ina-reflect na mada tunayojadili hasa kwa kada hiyo.
 
Asante kwa taarifa. All in all, procurement haisaidii self employment kwa fresh graduates.
Ndani yake unasoma kozi zinazokuwezesha ufanye self employment eg, entrepreneurship, strategic management, financial accounting
 
Baada ya kusoma mada na kutafakari kwa kina, ninaunga mkono hoja kwa 100%, hiyo kozi ya Procurement and supplying kwa inapaswa ifutwe kabisa hapa Tanzania kwenye vyuo vyetu. Haina maana yoyote kijana asiyekuwa na Connection ya wakubwa serikalini ya kuja kumpa ajira.
 
Mbona wanauhitaji sana mkuu. Mtu wa store anayecheza na stock ya store ni muhimu sana eneo lolote ambapo kuna store kama hotelini, mgahawa, gereji, hospital, popote pale ambapo kuna store.
Store anafundishwa mwanafunzi anaesoma accounting kuna topic kabisa na ipo deep Sana procurement ifutwe hii course
 
Uko sahhi San ingefundishwa kwa watu wa account au wale engineering wapate hyo Kaz Tena iwe very short sana haina maana nikisikia mtot anasoma procure au education natamani nimuambienkuwa aende hata veta tu akajifunze ufundi simu na ufundi uwashi au umeme wa manyumbani atapiga pesaa mnoo
 
Vipi kuhusu mining engineering, petroleum engineering, civil engineering, accountancy, taxation, public relations, nk wao wanajiajiri vipi
 
Procurement and Supply ilipaswa kuwa ni subcourse kwenye kozi zingine kulingana na kada husika na sio kuwa kozi kamili ya kuisomea na kupewa degree.
 
Sikubaliani na wewe kwa sababu, hayo yanaonekana yanawezekana kutokana na mfumo wa mazingira yetu, mfumo wa maisha usio rasmi.
Tuzungumzie taaluma katika maana nzima ya mtindo wa maisha katika mfumo rasmi. Hii haikubaliki.
Na ndio maana kwa mazingira haya yasiyo rasmi, ni kawaida kukita kijana wa mwenye MBA akiishi kwa kuendesha bajaji.
 
Procurement and Supply ilipaswa kuwa ni subcourse kwenye kozi zingine kulingana na kada husika na sio kuwa kozi kamili ya kuisomea na kupewa degree.
[emoji16][emoji16] una machungu either wewe ni supplier ulinyimwa tender, acha watu wapige 10%
 
Vipi kuhusu mining engineering, petroleum engineering, civil engineering, accountancy, taxation, public relations, nk wao wanajiajiri vipi
Soma mada na kuelewa, usikariri ndugu. Mleta mada amekuja kuzungumzia kozi moja mahususi ya Procurement and Supply. Zipo kozi nyingi za ovyo na zisizo na kichwa wala mkia hapa Tz kwa sasa, Procurement and Supply ni mojawapo katika hizo, tena huenda ni kinara.
 
Procurement and Supply ilipaswa kuwa ni subcourse kwenye kozi zingine kulingana na kada husika na sio kuwa kozi kamili ya kuisomea na kupewa degree.
Punguzenj chuki na watu wa procurement, ili kukufanya uendelee kuwa na machungu zaidi nj kwamba watu wa procurement wamezungukwa tu na pesa ,

Kuhusu kujiajiri msiwapeleke shule watoto ili muwafundishe kujiajiri huko majumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…